LICHA ya kushindana katika soko la biashara ya mafuta nchini, kampuni zinazojihusisha na biashara hiyo zimekutana kupitia bonanza la michezo lililoandaliwa na Umoja wa Wauza Mafuta Tanzania (TOAMAC), kwa lengo la kuimarisha mahusiano na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi wake.

Bonanza hilo limewakutanisha wafanyakazi kutoka kampuni zinazowakilisha takribani asilimia 97 ya soko la uuzaji wa mafuta nchini, likitoa fursa kwa washiriki kukutana nje ya mazingira ya kikazi na kushiriki shughuli za kimichezo.

Akizungumza katika bonanza hilo, Makamu Mwenyekiti wa TOAMAC, Imani Mtafya, amesema pamoja na kampuni hizo kushindana kibiashara, zina masuala mbalimbali yanayozihitaji kushirikiana katika kuendeleza sekta hiyo.

Amesema michezo ni mojawapo ya njia zinazoweza kujenga mahusiano baina ya wafanyakazi wa kampuni hizo, huku ikiwafundisha misingi ya nidhamu, ushirikiano na ushindani wa haki.

Mtafya amesema misingi hiyo ni muhimu si katika michezo pekee, bali pia katika mazingira ya biashara, ambako ushindani unapaswa kwenda sambamba na kuzingatia usawa na haki kwa washiriki wote wa soko.

Kwa upande wake, Raphael Mgaya amesema bonanza hilo limefanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa umoja huo, likiwa na malengo ya kuimarisha afya za wafanyakazi na kujenga mshikamano miongoni mwa wadau wa sekta ya mafuta.

Amesema afya ni sehemu muhimu katika utendaji wa kazi na shughuli za biashara, hivyo wafanyakazi wanapaswa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kushiriki michezo.

Bonanza hilo lilihusisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, voliboli na tenisi, pamoja na mazoezi ya viungo yaliyowashirikisha washiriki.

TOAMAC ina wanachama wapatao 22 hadi 23, ambao ni kampuni zinazojihusisha na biashara ya mafuta nchini.











Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...