Wananchi wa kijiji cha Makhoromba wilayani Karatu hivi karibuni wanatarajiwa kupumua baada ya kumalizika kwa ujenzi wa uzio wa umeme unaofanywa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 72 ili uweze kukamilika.
Lengo la ujenzi wa uzio huo ni kuondoa migogoro baina ya wanyamapori wakali na waharibifu dhidi ya wananchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM inayosisitiza umuhimu wa wananchi kulindwa.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Victoria Shayo, amesema ujenzi huo unafanyika ili wananchi katika eneo hilo na mali zao waweze kuwa salama.
Ziara hiyo imehitimishwa kwa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika kulinda na kutunza mazingira pamoja na kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwani uwepo wake utawazuia wanyamapori wakali kutotoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...