Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana kulinda amani na usalama wa Tanzania wakati nchi ikijiandaa kupokea wageni wa kimataifa kwa ajili ya shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchini.

Rais Samia ametoa wito huo leo, Novemba 20, aliposalimia wananchi wa Bomang’ombe, wilayani Hai, akiwa njiani kuelekea mjini Moshi.

Amesema idadi ya watalii wanaoingia nchini na mikutano ya kimataifa inayofanyika Tanzania ni kielelezo cha nchi kuendelea kuwa salama.

“Ombi langu kwenu ni amani na utulivu kwa nchi yetu,” amesema Rais Dkt. Samia.

Ametaja michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027, na mashindano ya urembo wa dunia mwaka 2027 kuwa miongoni mwa matukio yatakayoleta wageni wengi nchini.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amesema Serikali imetenga tena fedha za kujenga soko la kimataifa wilayani Hai.

“Ninataka niwahakikishie, tunakwenda kujenga soko la kimataifa ndani ya wilaya hii,” amesema Rais Dkt. Samia, na kuongeza kuwa soko hilo litawapa wakulima sehemu ya uhakika ya kuuza mazao yao.

Rais Dkt. Samia yupo mjini Moshi, katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Shule ya Polisi mjini humo.

Vilevile, ameahidi kurejea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara rasmi ya kikazi, ambapo atatembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...