Wakazi takribani 1,000 wa Kitongoji cha Saburi, Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli, Arusha, wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yao na mwekezaji (Akram Aziz) wakidai kuwa ardhi wanayoishi iko hatarini kuchukuliwa.
Kilio hicho kimekuja kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, aliyetoa maamuzi ya kuwapatia wananchi hao ekari 100, uamuzi ambao wameuelezea kutoridhishwa nao kabisa wakidai kuwa hawajapewa haki yao stahiki.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi hao, Mariam Faustine amesema mgogoro ulifikia hatua ya mvutano Oktoba 2, mwaka huu, baada ya watu wasiojulikana kufika eneo hilo wakiwa na magreda , Silaha kwa lengo la kubomoa nyumba za wananchi.
Wananchi hao wameeleza kusikitishwa na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa ya kusitisha shughuli za maendeleo katika eneo hilo, wakisisitiza kuwa wameishi hapo kwa muda mrefu na zaidi ya Miaka 30 wanaamini kuwa wana haki ya kisheria ya kumiliki ardhi hiyo.
Naye Sara Alaisi amesema hawajaridhishwa na uamuzi wa kuwapatia ekari 100 pekee, huku wakimuomba Rais Samia kuingilia kati ili suala hilo lipatiwe suluhisho la haki.
Awali, RC Makalla alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maamuzi yaliyotolewa yanatekelezwa.
Wananchi hao sasa wanaiomba Serikali kuu kuangalia upya suala hilo ili kulinda haki zao na kuepusha uwezekano wa kupoteza makazi yao.
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...