Na Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Tanzania imetambua na kuthamini mchango wa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kwa kipindi cha miaka 60.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakati akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanza kwa mpango wa kuleta wataalamu wa kujitolea kutoka Japan nchini Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bw. Mwandumbya amesema maadhimisho hayo ni fursa muhimu ya kutambua urafiki, mshikamano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Japan, pamoja na kuthamini mchango wa wataalamu wa kujitolea kutoka Japan katika kusaidia juhudi za maendeleo ya Taifa, hususan katika ngazi za jamii.
Amesema katika kipindi cha miaka 60, wataalamu kutoka Japan wamechangia maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, kilimo, mafunzo ya ufundi na maendeleo ya jamii kupitia uhamishaji wa maarifa, teknolojia na uzoefu, pamoja na kujenga uwezo wa taasisi na watumishi wa Kitanzania.
“Mchango wa wataalamu kutoka Japan hauishii katika kutoa huduma za kitaalamu pekee, bali pia umeimarisha uhusiano kati ya wananchi wa Tanzania na Japan kupitia kubadilishana tamaduni, maarifa na uzoefu, hali iliyosaidia kujenga urafiki na mahusiano ya kudumu kati ya wananchi wa mataifa hayo mawili”, amesema Bw. Mwandumbya.
Aidha, Bw. Mwandumbya amesema Serikali ya Tanzania inathamini pia mchango wa ushirikiano wa maendeleo unaotolewa na Serikali ya Japan kupitia JICA, ikiwemo mikopo yenye masharti nafuu, misaada na ushirikiano wa kiufundi.
Amebainisha kuwa hadi sasa Tanzania imepokea mikopo yenye masharti nafuu kutoka Japan yenye thamani ya zaidi ya Yen bilioni 147.30 na misaada inayozidi Yen bilioni 176.76, huku Watanzania zaidi ya 22,000 wakinufaika na fursa za mafunzo ya kitaalamu nchini Tanzania na Japan.
Amesema misaada na mikopo hiyo imechangia uwekezaji katika sekta za usafiri, nishati, maji, kilimo, afya, elimu na maendeleo ya rasilimali watu, hatua zilizosaidia kuboresha utoaji wa huduma za umma, kuongeza uwezo wa uzalishaji na kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji endelevu wa uchumi.
Akizungumzia mwelekeo wa ushirikiano huo, Bw. Mwandumbya amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Japan na JICA katika maeneo ya kipaumbele yakiwemo miundombinu ya usafiri, maendeleo ya rasilimali watu, uhamishaji wa teknolojia, ubunifu, maendeleo yanayozingatia mabadiliko ya tabianchi, viwanda na uimarishaji wa uwezo wa taasisi.
Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, amesema wataalamu wa kujitolea kutoka Japan ni nguzo muhimu katika kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya wananchi wa Tanzania na Japan.
“Nanajivunia kuona wataalamu wakiendelea kuhudumu nchini Tanzania, kufanya kazi kwa karibu na wananchi, kujenga mahusiano ya kijamii na kukuza uelewa wa tamaduni za mataifa hayo mawili kupitia kubadilishana uzoefu”, amesema Mhe. Balozi Mikami.
Naye Makamu wa Rais wa JICA, Bw. Hiroyuki Kobayashi, pamoja na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania, Dkt. Katsuya Kuge, wamesema shirika hilo litaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika maendeleo ya rasilimali watu kupitia programu mbalimbali, ikiwemo mpango wa wataalamu wa kujitolea.
Wamesema JICA inaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali, ikiwemo usafiri na usafirishaji wa mizigo, pamoja na kutekeleza miradi inayochangia kufikia malengo ya Dira 2050, ambayo yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Makatibu Tawala wa Mikoa inayopokea manufaa ya miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa ushirikiano na JICA, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bw. Richard Kayombo, amesema ushirikiano na Japan umekuwa na manufaa makubwa kwa jamii kutokana na wataalamu wa Japan kuishi pamoja na Watanzania, kufanya kazi kwa karibu na wananchi, kujifunza lugha ya Kiswahili na kuelewa tamaduni pamoja na mazingira ya maisha ya Watanzania.
Ameeleza kuwa mwingiliano huo umewezesha kubadilishana maarifa, uzoefu na ujuzi, sambamba na kuimarisha uelewa na urafiki kati ya wananchi wa Tanzania na Japan.
Ushirikiano kati ya pande hizo mbili ulianza rasmi mwaka 1966 baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya mpango wa JOCV, huku kundi la kwanza la wataalamu wa kujitolea kutoka Japan likiwasili nchini mwaka 1967.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akieleza mchango wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV) katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa JOCV, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, akieleza namna wataalamu wa kujitolea kutoka Japan walivyo nguzo muhimu katika kuimarisha urafiki na mahusiano kati ya Tanzania na Japan, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, kabla ya kuanza kwa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akipata maelezo kuhusu historia ya Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, ambaye aliwahi kujitolea nchini Tanzania kama Mwalimu katika eneo la Ujiji, mkoani Kigoma, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, pamoja na viongozi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), kabla ya kuanza kwa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
.jpg)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Hiroyuki Kobayashi, wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kujitolea kutoka Japan wanaohudumu katika sekta mbalimbali nchini Tanzania, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa Japan Overseas Cooperation Volunteers (JOCV), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...