Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Alex Lobora, amesema ujenzi wa makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni mkakati wa kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori unaoongozwa na sayansi.
Dkt. Lobora ameyasema hayo wakati wa ziara ya wajumbe wa Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori (TWPF), ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuridhia sehemu ya fedha za mfuko wa TWPF na Hazina kutumika katika ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na ofisi na maabara ya kisasa.
Naye mwenyekiti wa bodi ya TWPF, Prof. Jafari Kideghesho, amepongeza usimamizi wa mradi na kuitaka TAWIRI kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Eblate Mjingo, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo, akisema jengo hilo litakuwa nyenzo muhimu katika kuimarisha tafiti zenye tija kwa uhifadhi na utalii endelevu.
Ujenzi wa jengo hilo la ghorofa tatu, unaoendelea Njiro, Arusha, umefikia asilimia 41 na unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 8.9 hadi kukamilika.



.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...