Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imekutana katika kikao chake maalum leo Jumamosi tarehe 28 Juni 2025, kufuatilia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi ndani ya CCM. 

Kikao hicho kilipokea na kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za zoezi hilo la uchukuaji wa fomu za kuwania uteuzi wa kugombea nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola, lililoanza rasmi leo kwa mchakato wa ndani ya CCM, katika maeneo yote nchi nzima. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali, ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu hizo za kuwania kuteuliwa ndani ya CCM, imeanza leo tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na itahitimishwa tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.
Ratiba hiyo itahusisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi nafasi za; Ubunge wa Jimbo, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ubunge wa Viti Maalum, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum, Udiwani wa Kata au Wadi na Udiwani wa Viti Maalum. 




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...