Na Janeth Raphael - MichuziTv 

BENKI ya CRDB kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (OR-MV) imesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuwawezesha vijana wa vyuo vikuu na vyuo vya kati kupitia majukwaa ya vijana yanayojulikana kama Campus Connect.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha uendeshaji wa makongamano ya Campus Connect na kuwafikia vijana zaidi ya 300,000 ndani ya kipindi cha miaka mitano, kwa kuwajengea uwezo katika maeneo ya ubunifu, ujasiriamali, biashara, vipaji pamoja na matumizi ya fursa mbalimbali za kiuchumi.

Hafla ya uwekaji saini wa makubaliano hayo imefanyika leo, Novemba 9, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, jijini Dodoma, ikiwa ni hatua inayodhihirisha dhamira ya CRDB katika kuchangia maendeleo na uwezeshaji wa vijana nchini.

Kupitia ushirikiano huo, vijana pia wataunganishwa na fursa za mitaji na masoko, hatua itakayowawezesha kubadilisha mawazo na bunifu zao kuwa biashara na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, amesema uwezeshaji wa vijana unapaswa kuanza mapema wanapokuwa vyuoni ili kuwajengea maarifa, uelewa na ujasiri wa kujiajiri badala ya kutegemea ajira rasmi pekee.

Amesisitiza kuwa jukwaa la Campus Connect linapaswa kuwa mfumo endelevu wa kuwafuatilia na kuwaendeleza vijana kuanzia wanapokuwa vyuoni hadi wanapohitimu na kuanza maisha ya kujitegemea, ili kuhakikisha wanatumia ipasavyo maarifa na fursa wanazopatiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Benki ya CRDB amesema ushirikiano huo unaongeza nguvu katika kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kifedha mapema, kuwawezesha kubuni mawazo, kuanzisha biashara na kutumia kikamilifu fursa za kujiajiri. Amesema kupitia ushirikiano huo, CRDB itaendelea kuwa sehemu muhimu ya safari ya kuwaibua na kuwawezesha vijana, ili waweze kukuza shughuli zao za kiuchumi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.








Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima kununua Mbegu za mazao ya bustani hususani parachichi ambazo zina stika maalum za TOSCI, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora na kuhakikisha wakulima wanapata miche inayokidhi viwango.

Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanunuzi kutambua miche bora kwa urahisi kupitia nembo ya TOSCI, pamoja na kujikinga na kununua miche isiyokidhi viwango vinavyotakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TOSCI wakati wa maonesho ya jukwaa la kwanza la HortiLogistica Africa yaliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Nyasebwa Chimagu, amesema matumizi ya stika hizo ni sehemu ya mikakati ya taasisi hiyo ya kuimarisha usimamizi wa ubora wa mbegu na miche ya mazao mbalimbali ya bustani.

Amesema kuwa upatikanaji wa miche bora ni muhimu katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima, huku ukichangia kuimarisha ushindani wa mazao ya horticulture katika masoko ya ndani na kimataifa.

Aidha, amewahimiza wakulima na wadau wengine wa sekta ya horticulture kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu ubora wa mbegu na miche ya mazao ya bustani, pamoja na kufahamu aina za mbegu zinazokidhi mahitaji ya masoko ya kimataifa.

TOSCI imesisitiza umuhimu wa wanunuzi kuwa makini wakati wa kununua miche kwa kuhakikisha wanapata miche yenye stika na utambulisho unaotambulika na taasisi hiyo, ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza tija katika kilimo.

Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima kununua Mbegu za mazao ya bustani hususani parachichi ambazo zina stika maalum za TOSCI, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa ubora na kuhakikisha wakulima wanapata miche inayokidhi viwango.

Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanunuzi kutambua miche bora kwa urahisi kupitia nembo ya TOSCI, pamoja na kujikinga na kununua miche isiyokidhi viwango vinavyotakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TOSCI wakati wa maonesho ya jukwaa la kwanza la HortiLogistica Africa yaliyofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Nyasebwa Chimagu, amesema matumizi ya stika hizo ni sehemu ya mikakati ya taasisi hiyo ya kuimarisha usimamizi wa ubora wa mbegu na miche ya mazao mbalimbali ya bustani.

Amesema kuwa upatikanaji wa miche bora ni muhimu katika kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima, huku ukichangia kuimarisha ushindani wa mazao ya horticulture katika masoko ya ndani na kimataifa.

Aidha, amewahimiza wakulima na wadau wengine wa sekta ya horticulture kutembelea banda la TOSCI ili kupata elimu kuhusu ubora wa mbegu na miche ya mazao ya bustani, pamoja na kufahamu aina za mbegu zinazokidhi mahitaji ya masoko ya kimataifa.

TOSCI imesisitiza umuhimu wa wanunuzi kuwa makini wakati wa kununua miche kwa kuhakikisha wanapata miche yenye stika na utambulisho unaotambulika na taasisi hiyo, ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza tija katika kilimo.


Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) imeshiriki katika Maonesho ya Tisa ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE) jijini Shanghai, nchini China, kwa lengo la kutangaza Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kuwaunganisha wanunuzi wa kimataifa na fursa za biashara ya mazao ya Tanzania.

Katika maonesho hayo ya siku tano (Novemba 5-10, 2026), WRRB imeeleza jinsi mfumo huo unavyowezesha uhifadhi wa mazao katika maghala yenye leseni, utunzaji wa ubora wake na uuzaji wake kwa uwazi.

Akizungumza alipotembelea banda la Tanzania katika maonesho hayo, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shabaan, amepongeza ushiriki wa Tanzania, hususan wa taasisi za serikali, akisema maonesho hayo yanazipa taasisi hizo fursa ya kutangaza huduma zinazotolewa nchini.

Amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutumia maonesho hayo kujitangaza kimkakati na kufikia wanunuzi wa kimataifa wanaotafuta bidhaa za Tanzania.

Aidha, Mwakilishi wa kampuni ya Chengdu Jintao Yunhui International Trade Co., Ltd. ameonesha kuvutiwa na ufuta mweupe wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa mazao yanayouzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.



Na Mwandishi Wetu, Korogwe

WANAFUNZI wa Kike katika Shule za Sekondari nchini wametakiwa kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kuwawezesha kupata ufadhili wa Samia Suluhu ambao utakuwa chachu kwao kuweza kufikia ndoto zao za kielimu.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Kampuni ya Shemnyama African Association Business Consultancy and Insurance Agency Rajab Shemnyama ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa maafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Ambapo alisema kwamba masomo ya sayansi yatawawezesha kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kutokana na utandawazi uliopo

Alisema wanafunzi wanapaswa kutumia fursa za elimu kwa kujituma katika masomo ili shule hiyo iweze kuzalisha wataalamu wengi katika fani mbalimbali.

Pia, alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akiwataka wanafunzi kuitumia kujifunza na kuongeza maarifa badala ya kujihusisha na mambo yanayoweza kuathiri maadili na maendeleo yao.

Aliwaasa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na tabia hatarishi zinazoweza kuhatarisha afya na mustakabali wao, huku akisisitiza umuhimu wa kujitambua na kulinda heshima zao.

Aidha, alisema elimu inapaswa kwenda sambamba na ujuzi wa ziada utakaowawezesha vijana kujiajiri na kujipatia kipato, hasa kutokana na changamoto ya ajira inayoweza kuwakabili baada ya kuhitimu.

Alisisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kushiriki katika matamasha na shughuli za ujasiriamali ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi.

Akizungumzia suala la chakula shuleni, Shemnyama aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana, akieleza kuwa njaa huathiri umakini na uwezo wa kufuatilia masomo darasani.

Pia, aliomba uongozi wa shule kuimarisha miradi ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kilimo, akibainisha kuwa sekta hiyo inaweza kuwa chanzo cha fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana.


"Lakini pia kupitia Kampuni Yetu hii tutatoa madaftari kwa ajili ya watoto wasiokuwa na wazazi (Mayatima) kwa lengo la kuwapunguzia makali "Alisema

Alisema amezipokea changamoto zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kutafuta namna ya kuzitatua.

Katika maafali hayo ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa maktaba ya Shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.



Mchango huo umetangazwa na Rajabu Shemnyama, ambaye ni mhitimu wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne, akisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za shule kuinua kiwango cha ufaulu na kuondoa daraja sifuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2026

Shemnyama alisema ameamua kuchangia maendeleo ya shule hiyo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu, akibainisha kuwa yeye ni zao la shule hiyo na anajivunia kuona mabadiliko yaliyofikiwa tangu alipokuwa mwanafunzi.

Alisema maendeleo ya elimu yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, hivyo kuwataka wahitimu na watu wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo kujitokeza kuchangia kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika shughuli za maendeleo, ikiwamo kuchangia madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.


Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Old Korogwe, Bilali Shemkai, alisema shule hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayepata daraja sifuri katika matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2026.

Alisema juhudi hizo zimeanza kuonyesha matokeo kutokana na kupungua kwa idadi ya wanafunzi waliopata daraja hilo kutoka 38 mwaka 2023 hadi 20 mwaka 2024 na 10 mwaka 2025.




Alisema mbali na kuondoa daraja sifuri, shule hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 ina jumla ya wanafunzi 520, wakiwamo wasichana 284 na wavulana 236, pamoja na watumishi 32, wakiwamo walimu 31 na mtaalamu mmoja wa maabara.

Ina vyumba 14 vya madarasa na maabara tatu, ambapo maabara za Kemia na Baiolojia zimekamilika, huku maabara ya Fizikia ikiwa bado haijakamilika.

Pamoja na kuwa na huduma za maji, umeme na barabara, shule hiyo pia ina mradi wa kilimo unaohusisha uzalishaji wa mahindi na majaribio ya kilimo cha mpunga kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa chakula.




Hata hivyo, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula cha mchana, hali inayoufanya uongozi kuendelea kuwahamasisha wazazi kushiriki katika uchangiaji wa chakula.

Kupitia utaratibu uliowekwa, kila mzazi anahamasishwa kuchangia kilo nane za mahindi, kilo mbili za maharage na Sh4,000 kwa kila muhula kwa ajili ya chakula cha wanafunzi. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa na changamoto kutokana na mwitikio mdogo wa baadhi ya wazazi.

Changamoto nyingine ni uchakavu wa baadhi ya vyumba vya madarasa na mazingira ya nje ya shule, ambayo wakati mwingine yanaweza kuathiri utulivu na maandalizi ya wanafunzi kitaaluma.

Kutokana na hali hiyo, shule imekuwa ikishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na kata kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri usalama na maendeleo ya wanafunzi.

Uongozi wa shule hiyo unaamini kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, wahitimu na wadau wengine wa elimu utasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kufanikisha malengo ya kuinua ufaulu.









Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro Dkt. Abdul-Razaq Badru jana usiku tarehe 9 Novemba. 2026 alitua kwenye kambi ya timu hiyo inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA mkoani Morogoro kukagua hali ya kambi hiyo na maendeleo ya wachezaji.

Mara baada ya kukutana na wachezaji hao Dkt.Badru ametoa maelekezo ya wanamichezo wa Ngorongoro kutumia fursa hiyo Kama mojawapo ya kujifunza mambo mapya kutoka taasisi nyingine.

“Tumieni michezo kuitangaza Ngorongoro, chezeni kwa nguvu zenu zote Ila mkumbuke michezo ni furaha na amani na muwe tayari kupokea aina yoyote ya matokeo,”alisema Dkt.Badru.

Afisa Michezo wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Yotham Gitige alimshukuru kamishna kwa ziara hiyo na kusema kuwa imewatia moyo katika ushiriki wao kwenye michezo hiyo.






Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA) Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Novemba, 2026 kabla ya kuondoka kuelekea Jijini Antalya, Uturuki, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko yaTabianchi (COP31).










 

MASHABIKI wa soka la wanawake wanatarajia kushuhudia burudani nyingine ya kuvutia katika michuano ya UEFA Women's Champions League, wakati BK Häcken ya Sweden itakapokuwa mwenyeji wa Chelsea Women ya England, Jumanne, Novemba 10, 2026, kuanzia saa 21:00 usiku. Ni mchezo unaobeba ushindani mkubwa huku kila upande ukiwa na dhamira ya kuonyesha ubora wake katika jukwaa kubwa la soka la wanawake barani Ulaya.

Chelsea inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na hadhi ya moja ya timu zenye ushindani mkubwa katika soka la wanawake barani Ulaya. Kikosi hicho kinajivunia uzoefu wa kushiriki michezo mikubwa, uwezo wa kucheza kwa kasi na kutumia nafasi zinazopatikana, jambo linalokifanya kuwa mpinzani mgumu kwa Häcken.

Kwa upande wa BK Häcken, kucheza nyumbani ni nafasi muhimu ya kuonyesha uwezo wao mbele ya mashabiki wao. Timu hiyo ya Sweden itahitaji kutumia vizuri mazingira ya nyumbani, kucheza kwa nidhamu na kutumia mashambulizi ya haraka ili kuisumbua safu ya ulinzi ya Chelsea.

Katika hatua ya mashindano, Chelsea inaingia ikiwa na matokeo mazuri zaidi baada ya kukusanya pointi saba katika michezo yake mitatu ya mwanzo, ikishinda miwili na kutoka sare moja. Häcken, kwa upande mwingine, imekusanya pointi moja pekee baada ya kupoteza michezo miwili na kutoka sare moja, hivyo ushindi katika mchezo huu ni muhimu kwa matumaini yake ya kupanda kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na vita kubwa ya kiufundi, hasa eneo la kiungo na safu za ushambuliaji. Chelsea itahitaji kutumia kasi na uzoefu wake kutengeneza nafasi za mabao, huku Häcken ikitarajiwa kupambana kwa nguvu, kulinda lango lake na kutumia kila nafasi itakayopata mbele ya mashabiki wake.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa hiyo, usikose kufuatilia dakika 90 za ushindani kati ya Häcken na Chelsea katika UEFA Women's Champions League. Je, Chelsea itaendeleza ubabe wake na kuondoka na pointi tatu au Häcken itatumia faida ya uwanja wa nyumbani kufanya maajabu? Jiandae kuwa mshindi kwenye mechi hii ndani ya Meridianbet leo na Jisajili sasa!

MASHABIKI wa michezo wanapenda mashindano yenye ushindani, msisimko na zawadi kubwa, lakini safari ya burudani haipaswi kuishia uwanjani pekee. Sasa Meridianbet imekuja na habari njema kwa wapenzi wa michezo ya kasino kupitia mchezo mpya wa Gates of Meridian, uliobuniwa na Expanse na kupatikana rasmi kuanzia Novemba 2, 2026. Huu ni mwanzo wa safari mpya yenye matukio ya kusisimua, ambapo kila hatua inaweza kufungua ukurasa mwingine wa burudani.

Gates of Meridian unakukaribisha katika ulimwengu wa kipekee uliojaa fursa mbalimbali za kufurahia mchezo. Kama ilivyo katika mashindano makubwa ya soka, ambapo kila dakika inaweza kubadilisha matokeo, mchezo huu unakuja na vipengele vinavyoongeza msisimko katika kila hatua. Miongoni mwa vinavyokuvutia ni mizunguko ya bure, bet za bonasi ambazo zinaongeza ladha tofauti katika safari yako ya kucheza.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini burudani haiishii hapo, Gates of Meridian pia unakuletea mashindano ya Tournaments, ambapo unaweza kushiriki katika ushindani pamoja na wachezaji wengine. Pia kuna Multi-Level Progressive Jackpots na Mystery Jackpot zinazoongeza mvuto wa mchezo. Hapa, kila mchezaji ana nafasi ya kufurahia safari yenye matukio mbalimbali, huku Happy Hour ikiweka ladha nyingine ya kipekee katika uzoefu wa mchezo.

Kwa upande mwingine, Meridianbet imehakikisha kuwa wachezaji wanaendelea kupata uzoefu wenye manufaa. Hapa kuna vipengele vinavyoongeza chaguo za burudani na kufanya Gates of Meridian kuwa zaidi ya mchezo wa kawaida. Ni ulimwengu unaokupa sababu nyingine ya kufurahia kila hatua unapokuwa ndani ya mchezo huu mpya.

Usibaki nyuma wakati milango ya burudani imefunguliwa. Gates of Meridian inapatikana kipekee kupitia Meridianbet tangu Novemba 2, 2026. Tembelea Meridianbet, jisajili, ingia kwenye ulimwengu huu mpya wa Expanse na ugundue vipengele vyake vya kusisimua. Meridianbet, burudani yako inaanza hapa.
Jiji la Dodoma limetakiwa kuimarisha maandalizi ya ardhi, mifumo ya kiutawala na taratibu za utoaji wa huduma ili kuwezesha wawekezaji kupata maeneo na kuanza utekelezaji wa miradi katika ujenzi wa mji wa kisasa wa Hombolo.

Wito huo umetolewa Novemba 9, 2026, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba kati ya Jiji la Dodoma na kampuni ya kimataifa ya usanifu majengo na mipango miji ya Heerim Architects and Planners, kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mpango kabambe wa mji huo.

Senyamule amesema maandalizi yanapaswa kuanza mapema ili kuhakikisha maombi ya wawekezaji wanaohitaji maeneo yanashughulikiwa kwa haraka, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa timu maalumu itakayoratibu changamoto na kusimamia hatua mbalimbali za mradi.

Amesema matarajio ni kuona mradi huo ukitekelezwa kwa vitendo na kuleta mabadiliko yanayoonekana kupitia majengo na miundombinu, badala ya kubaki katika mipango ya maandishi, huku akisisitiza utekelezaji wake kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amesema hakuna mpango wa sasa wa kutenga ardhi kwa matumizi mengine yanayoweza kuathiri maandalizi ya mradi huo, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wataalamu wa ardhi katika kupanga matumizi ya eneo hilo.

Amehimiza wananchi na wadau wa maendeleo ya ardhi kufuata taratibu zilizowekwa na kutumia fursa zitakazojitokeza kupitia mradi huo kwa manufaa yao na kukuza uchumi.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko, amesema ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha mradi huo, ambao unatarajiwa kuchangia kuipa Dodoma taswira mpya ya mji wa kisasa.

Mwenyekiti wa Heerim Architects and Planners, Young-in Jung, amesema mpango huo unalenga kuendeleza mji wa kisasa, kijani na janja (Smart City), utakaokuwa na huduma na miundombinu ikiwemo viwanja vya ndege, vituo vya mikutano, hoteli, maeneo ya makazi na biashara, amesema hatua ya awali itahusisha upembuzi yakinifu na maandalizi ya mpango kabambe wa matumizi ya ardhi utakaoweka msingi wa utekelezaji.






 
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha na Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kuhusu Maridhiano ya Zanzibar baada ya mazungumzo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Novemba, 2026.







Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kuhusu Maridhiano ya Zanzibar, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 09 Novemba, 2026.