Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation imetoa msaada wa vifaa vya elimu kwa Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi, iliyopo Wilaya ya Ubungo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika sekta ya elimu.
Msaada huo unajumuisha kompyuta 30, vifaa vya UPS 30, televisheni moja yenye ukubwa wa inchi 75 pamoja na madawati 90, ambavyo vinatarajiwa kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji shuleni hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Vodacom Tanzania Foundation, Uendelevu na Ubia, Pauline Alexander Koola, amesema Vodacom inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kijamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya jamii, hususan katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, ameeleza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuboresha huduma za kijamii, akitambua mchango wa Vodacom katika kuimarisha mazingira ya elimu.
Msaada huo unatarajiwa kuwanufaisha wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi na Ufundi Mbezi kwa kuboresha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kuongeza fursa za wanafunzi kujifunza kupitia teknolojia.















.jpeg)

.jpeg)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Salum Mnuna,akizungumza wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mjini Singida.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
