
mwalimu akicheza bao na mmoja wa wazee wa butiama huyu mzee ali hassan mwinyi, mama maria na kaka yake chifu burito wakishuhudia. napost picha hii nikiwa njiani kumtembelea mama maria, na kuona butiama ilivyo bila mwalimu. vile vile kesho jumamosi kanisa katoliki linamtukuza mwalimu (canonize) ikiwa moja ya hatua za awali za kumfanya mtakatifu. nimekosa usafiri hivyo siwezi kuwahi kwani shughuli hiyo yafanyika butiama saa nne jumamosi nami natua saa nane. hata hivyo kama kuna swali mtu angependa nimuulize mama maria aseme leo, ijumaa, nitamuulizia.
Michuzi umenikumbusha mwaka 1999 ambapo nilikuwa Butiama kwa miezi miwili kikazi, sikuwa na habari kabisa na mambo ya ku-blogu ama sivyo ningeondoka na wasifu wa mama Maria, lakini kwa vile umeomba utusaidie..., basi naomba unihojie wasifu wake kwa ujumla.
ReplyDeleteAsante kwa msaada.
Mimi naomba umuulize msimamo wake kuhusu takrima katika chaguzi zetu anazichukuliaje?.
ReplyDeleteDennis
Safari njema lakini ukifika jaribu kumuuliza anaionaje Tanzania ya sasa bila kuwepo kwa Mwalimu, Rushwa iliyogeuzwa takrima na jinsi vigogo wanavyomiliki mali lukuki huku wakisahau kwamba kuna watu wanashindwa angalau kupata mlo mmoja kwa siku.
ReplyDeleteJe angekuwepo Mwalimu anadhani ingekuwaje kwani ni yeye pekee alikuwa karibu na Mwalimu kwa miaka mingi, walikaa Ikulu miaka 24 na baadaye wakahamia nyumbani Butiama hadi kifo kilipomchukua Mwalimu na kwamba nadhani hata maneno ya mwisho aliyoyasema Mwalimu kabla ya kifo chake kule London anakumbuka vyema, tafadhali naomba katuulizie haya.
WAKATABAHU
michuzi mbona upo kama haupo?
ReplyDeletehivi kweli jamani, naibu waziri wa mambo ya ndani, Masha, kwenda kufungua duka la nguo la kipanya ndiyo kazi hiyo?
ReplyDeleteAu Naibu Waziri, Joel Bendera kwenda airport kumpokea Mr Cooper kutoka Marekani ndiyo kazi? Jamani, viongozi wa Tanzania wanaelekea wapi?
Hawa wanstahili kufukuzwa, maana hata wajibu wao hawaujui. JK fukuza kunguni hawa haraka.