mwalimu akicheza bao na mmoja wa wazee wa butiama huyu mzee ali hassan mwinyi, mama maria na kaka yake chifu burito wakishuhudia. napost picha hii nikiwa njiani kumtembelea mama maria, na kuona butiama ilivyo bila mwalimu. vile vile kesho jumamosi kanisa katoliki linamtukuza mwalimu (canonize) ikiwa moja ya hatua za awali za kumfanya mtakatifu. nimekosa usafiri hivyo siwezi kuwahi kwani shughuli hiyo yafanyika butiama saa nne jumamosi nami natua saa nane. hata hivyo kama kuna swali mtu angependa nimuulize mama maria aseme leo, ijumaa, nitamuulizia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi umenikumbusha mwaka 1999 ambapo nilikuwa Butiama kwa miezi miwili kikazi, sikuwa na habari kabisa na mambo ya ku-blogu ama sivyo ningeondoka na wasifu wa mama Maria, lakini kwa vile umeomba utusaidie..., basi naomba unihojie wasifu wake kwa ujumla.

    Asante kwa msaada.

    ReplyDelete
  2. Mimi naomba umuulize msimamo wake kuhusu takrima katika chaguzi zetu anazichukuliaje?.
    Dennis

    ReplyDelete
  3. Safari njema lakini ukifika jaribu kumuuliza anaionaje Tanzania ya sasa bila kuwepo kwa Mwalimu, Rushwa iliyogeuzwa takrima na jinsi vigogo wanavyomiliki mali lukuki huku wakisahau kwamba kuna watu wanashindwa angalau kupata mlo mmoja kwa siku.
    Je angekuwepo Mwalimu anadhani ingekuwaje kwani ni yeye pekee alikuwa karibu na Mwalimu kwa miaka mingi, walikaa Ikulu miaka 24 na baadaye wakahamia nyumbani Butiama hadi kifo kilipomchukua Mwalimu na kwamba nadhani hata maneno ya mwisho aliyoyasema Mwalimu kabla ya kifo chake kule London anakumbuka vyema, tafadhali naomba katuulizie haya.

    WAKATABAHU

    ReplyDelete
  4. michuzi mbona upo kama haupo?

    ReplyDelete
  5. hivi kweli jamani, naibu waziri wa mambo ya ndani, Masha, kwenda kufungua duka la nguo la kipanya ndiyo kazi hiyo?

    Au Naibu Waziri, Joel Bendera kwenda airport kumpokea Mr Cooper kutoka Marekani ndiyo kazi? Jamani, viongozi wa Tanzania wanaelekea wapi?

    Hawa wanstahili kufukuzwa, maana hata wajibu wao hawaujui. JK fukuza kunguni hawa haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...