Home
Unlabelled
kitendawili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Malawi na Tanzania kwenye ziwa Nyasa.
ReplyDeleteJames
rwanda na burundi vs tz
ReplyDelete-paka wa kwenye maji ziwa nyasa kati ya Tanzania na Malawi. Hauoneshi kuwa ziwa Nyasa linamilikiwa na nchi zote mbili.
ReplyDelete-pia mpaka wa kwenye maji kati ya Tanzania na Kenya kaskazini mwa Tanga mjini. Wete haioneshi kuwa iko Tanzania.
Tatizo lipo hapo kati ya Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa hakuna alama ya mpaka wa kimataifa.
ReplyDeleteMuhidin hizo picha zako tatu zimepandana halafu labda zimegandana pia!!! (Hongera sana kwa kazi nzuri!)
ReplyDeleteSasa juzi ile tulipoongea kwa simu nikiwa Dar, basi, jioni ile ile simu yangu ikayeyuka. Naona kuna vijana "wameinywa". Si neno ni rizki yao maana kijiji chetu kimekua kikubwa siku hizi na maisha yamekuwa magumu pia.
Kwa hiyo namba yangu ya simu imeshakuwa ya zamani tena, na yako sinayo kichwani. Tuwasiliane kwa namba hii chini.
0786 11 66 26 (Celtel)
maggid,
Liganga-Lilonga, Iringa.
Tatizo lipo hapo ziwa Nyasa mpaka wa kimataifa unaonyesha kuwa ziwa nyasa lipo malawi lote. hakuna sehemu ya ziwa nyasa tz.
ReplyDeleteWewe maggid sio Gabacholi wewe. Kama ni Gabacholi safi tu vijana wanarudisha mali mnazotuibia wahindi. Wahindi wezi sana, mhindi unafanya biashara ya mabilion lakini huna hata kibanda Tz kama sio kutuibia nini? Kwa nini humna investment za kudumu tz mnatubia mnahamishia uchumu wetu Kanada tu. Iko siku mtaondoka tu tutakapochukua nchi yetu wenye nchi. Biashara zenu za kiwizi wizi.
ReplyDeleteTatizo haliko kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi. Tanzania tuna strip nyembamba sana kama inavyoonekana kwenye ramani. Kwa sasa ndio haki yetu labda tudai upya. Kasoro anayoitaka Michuzi iko kwingine, ambako sijakung'amua bado.
ReplyDeletemimi nionavyo ni kwenye ziwa nyasa hakuna mpaka wa kimataifa kati ya Malawi na TZ, TZ haina sehemu yoyote katika ziwa hilo
ReplyDeleteNadhani mpaka wa Malawi na Tz hupita katikati ya ziwa Nyasa na si pembeni kama inavyoonekana.
ReplyDeleteMpaka wa Kutenganisha TZ na Malawi katika ziwa nyasa haupo. Pia ziwa victoria upande wa kenya limepunjwa. Sasa Bwn Michuzi jee utatubandikia kila picha tunayoomba wote tuliopatia? Binafsi naomba picha yakwako na mkeo pamoja na familia yako!
ReplyDeleteMuhidini,
ReplyDeleteNafikiri tatizo kubwa lipo kwenye huo Ziwa Nyasa - ambapo mpaka hauonyeshwi kabisa. Kama utachukulia dark blue ni mpaka - inakuwa shida hasa kwa kuwa itakuwa inaonyesha kuwa Tz haina sehemu yoyote katika ziwa Nyasa.
Utata huu ni wa muda mrefu sana (kama sikosei, tangu nipo darasa la tano (1975 -ok tayari wababe weshaanza kunizoza - kumbe haka kajamaa kikongwe - anyway:)tangu nipo darasa la tano nilikuwa nikisikia kuhusu hiki kizaa zaa. Nakumbuka na nyimbo za kumsuta Kamuzu Banda tuliimba!
KUhusu kwenye bahari ya Hindi - ni kwa vile tu haionyeshwi. Lakini huo mpaka wa kaskazini huwa haufuati mategemeo ya watu unapoingia sehemu za baharini -huwa kuna kitu kama "kiwiko" unapinda kaskazini na kuizunguka Wete - kwa eneeo kubwa tu.
Kuhusu Ziwa victoria - ni kweli mpaka unaotenganisha Kenya & Uganda haupo sahihi - Kenya imeminywa sana (Kenya na Uganda wana nusu nusu ya sehemu inaypbaki baada yakutoa Tz ambayo ipo sahihi BUT - that is really none of my Business!
TATIZO kubwa! Ramani hii ndiyo iliyopo kwenye "World Factbook" inayomilikiwa na CIA. Imekuwepo hapo siku nyingi, lakini nadhani hakuna anayejali kuwashitua jamaa - kuwa ramani hiyo ina kasoro. Kwa upande wangu hii ni kasoro muhimu hasa kwa kuwa - uki "google" Tz - guess ni mtandao gani unakuja kwanza - "World Factbook"
* Kwa sababu ya kukaa kimya - ramani hiyo hiyo (kasoro rangi) ndio imetumika kwenye mtandao wa "Infoplease" ambapo kuna - atlas, Encyclopedia n.k
*Kweli mzozo umetulia - lakini nani kashinda? Ningekuwa mMalawi - ningesubiri kupata wakati muafaka. Ramani hii itaendelea kugawanywa ma na kutumia, na in Just at the right time...., kutakuwa na a critical global mass ambayo itakuwa inafahamu mpaka huu tu! Then, nitazua mjadala mwingine - Wakati huo, itabidi Tz ifanye kazi ya ziada kujaribu kubadilisha uelewa (perception za dunia - Mambo yale yale ya "Njoo Kenya upande mlima wetu Kilimanjaro...!"
- Kalagh'abao - wajinga ndio waliwao"
Ned
Mpaka wa bahari ya indian ocean na mpaka wa lake nyasa.
ReplyDeleteand that's why people they call it free water or International territory
ReplyDeleteMpaka wa ziwa Nyasa hauna tatizo lolote. Ndivyo wazungu walivyogawa. Tanzania(then Tanganyika) tuliambulia a very parochial strip kama inavyoonekana kwenye ramani. Tatizo analolitaka michuzi liko kwingine sio nyasa.
ReplyDeleteMkumbuke pia jina halisi la ziwa hili ni ziwa malawi. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani linahodhiwa na malawi. Hata jina 'nyasa' ni jina pia la nchi hiyo. Wakati wa ukoloni nchi hiyo iliitwa 'nyasaland'
Walimu shuleni walikuwa wanatudanganya kwa kuchora mstari(mpaka katikati). Nao walikuwa wanadanganywa na vitabu vilivyoandikwa na maamuna wa jiografia. Sehemu ya ziwa nyasa Tanzania ni nyembamba kama inavyoonekana katika ramani. Lakini kwa uhalisia ukiwa pale ziwani ni sehemu kubwa tu huwezi kudhania ni ndogo hivi. Watu wanavua samaki (mbasa) na samaki wengine na shughuli zingine zote za ziwa. Nimesafiri kwa meli ziwa nyasa.
Kuhusu ugomvi wa mpaka kati ya tanzania na malawi tutofautishe kati ya ziwa na mto. Ugomvi uko kwenye mto Songwe ambao ni kama malaya hivi. Ni matokeo ya river miendering. Masika ya mwaka huu sehemu ya ardhi inakatwa kabisa inakuwa malawi, mwaka unaofuatia sehemu ilele inakuwa Tanzania. Ugomvi kati ya Marehemu Ngwazi Hastings Kamuzu Banda na Hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuwa katika mto Songwe, sio ziwa nyasa.
Labda sasa tudai upya kuwa tulidanganywa katika Berlin conference (Nov 1884/Febr 1885)na kupewa sehemu nyembamba hivi. Lakini kabla hatujadai, hiyo ndio haki yetu.
sio kuwa wanadanganya hiyo dispute ipo na haijapata kupata ufumbuzi. Ni kwamba malawi na Tanzania wako ktk mazingira ya kuelewana ila isingekuwa hivyo ungesikia mtafaruku juu ya mpaka ktk ziwa nyasa/malawi. Kwa maelezo zaidi nenda kasoma habari kwenye CIA fact book sehemu ya Tanzania International disputes
ReplyDeletemichuzi embu tuambie basi. tumechoka kusubiri
ReplyDeleteMICHUZI UMEENDA LIKIZO AU? NA KAMA NDIO HATUAGANI? KAMA SIO UKO WAPI LEO? NIMEKUMISO JAMANI.
ReplyDeletehivi nyie mnaosema hakuna mpka kati ya tanzania na malawi macho yenu yamekosa mchicha? Hebu angalieni vizuri mpaka ulipopita.
ReplyDeletesijapata ! lakini naomba picha ya salum londa, ni mjomba wangu ..yeye ni kiongozi serikalini !!
ReplyDeleteaccording to mpaka uliopo ina maana tz hatuna ziwa nyasa liko malawi na kidogo nsumbiji namtumbo kulie tuu.
ReplyDeleteMgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi una historia ndefu. Je ziwa nyasa liko Tanzania na Malawi au liko Malawi tu? Mnakumbuka nyimbo zile tulizokuwa tukimuuimba Kamuzu Banda. Kuna wakati Nyerere alitoa hotuba akatupa kisa kile cha Kamuzu Banda alivyomwendea Nyerere na ramani kuukuu akimthibitishia kuwa ziwa lile liko Malawi. nyerere akamfukuzia mbali!
ReplyDeletemstari wa bluu unaonyesha mpaka wa ziwa na si nchi hivyo basi kama tunasema ziwa
ReplyDeletenyasa lipo tz ina maana na malawi ni sehemu ya tz!!! na kama tunashikilia mpaka umewekwa kwa rangi nyeusi baina nchi na nchi basi ZIWA NYASA HALIPO TZ....na ina maana kwamba yale maji ya ziwa nyasa tunayaona hayo hapo na hatutakiwi hata kuyagusa ukiogelea tu humo malawi ina haki kukushitaki.
Nyerere ndio nilikuwa nampendea hapo UBABE!!!! bro sahizi hapa angebaki kuchekacheka tu mpaka wanachukua chao.
mpaka wa Malawi na Tz hupita katikati ya ziwa Nyasa na si pembeni kama inavyoonekana.
ReplyDeleteMARTHA,KTK UKOO WENU MPO WANGAPI?NA WANGAPI NI WANAMUZIKI?SASA ARUSHA KWAYA UMEMWACHIA NANI?
ReplyDeletesamahani kwa kuhitimisha mjadala nikiwa nimechelewa. ila napenda kusema wote waliosema kama dada martha hapo juu wamepatia. vile vile namshukuru ndesanjo kwa kutoa mwanga zaidi, japo kiduuuuchu.
ReplyDeleteni kweli tatizo la mpaka wa malawi na tanzania (sio kwenye ziwa nyasa tu, hata mto songwe ambao ukujaa hufanya wakazi wa mipakani aidha wa tanzania wajikute malawi, na wa malawi wajikute bongo.
hizi nchi mbili zimeunda tume ya pamoja juu ya swala hili na sasa mwenyekiti wake ni mama sijaona, katibu mkuu wizara ya ardhi, ili kujua namna ya kubishana bila kugombana.
vile vile kaa ukijiua kwamba wamalawi huliiza ziwa nyasa ziwa malawi kwani kwao neno `nyasa´ ni ziwa (nakubali kukosolewa kama si sahihi).
nikirudi bongo ntabandika stori yote kama ilivyo. naomba kutoa hoja...
Ulituahidi atakaepatia utampatia picha yoyote aliyoomba. Binafsi niliomba picha ya familia yako.
ReplyDeleteMichuzi line
ReplyDeletemstari wa ziwa nyasa unatakiwa kuamba na tanzania Ziwa la nyasa liko Malawi
Sidi
ni kweli nimeahidi kutoa zawadi ya picha. sasa nimpe nani nimnyime nani, maana karibu wote mmepatia na zawadi ni moja tu...
ReplyDeletemichuzi hili ni ombi la mwisho naomba picha ya salum londa ! kama unayo sawa kama hauna sawa !!
ReplyDelete