naenda kulala nikiacha hiki kitendawili. kuna alama za mipaka ya kimataifa haiko sahihi kwenye ramani hii. ni ipi hiyo? zawadi: picha yoyote utayoomba. samahani zimegandana tatu, lakini zote hazina tofauti, ni aina moja...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2006

    Malawi na Tanzania kwenye ziwa Nyasa.
    James

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2006

    rwanda na burundi vs tz

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2006

    -paka wa kwenye maji ziwa nyasa kati ya Tanzania na Malawi. Hauoneshi kuwa ziwa Nyasa linamilikiwa na nchi zote mbili.

    -pia mpaka wa kwenye maji kati ya Tanzania na Kenya kaskazini mwa Tanga mjini. Wete haioneshi kuwa iko Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2006

    Tatizo lipo hapo kati ya Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa hakuna alama ya mpaka wa kimataifa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2006

    Muhidin hizo picha zako tatu zimepandana halafu labda zimegandana pia!!! (Hongera sana kwa kazi nzuri!)

    Sasa juzi ile tulipoongea kwa simu nikiwa Dar, basi, jioni ile ile simu yangu ikayeyuka. Naona kuna vijana "wameinywa". Si neno ni rizki yao maana kijiji chetu kimekua kikubwa siku hizi na maisha yamekuwa magumu pia.
    Kwa hiyo namba yangu ya simu imeshakuwa ya zamani tena, na yako sinayo kichwani. Tuwasiliane kwa namba hii chini.
    0786 11 66 26 (Celtel)
    maggid,
    Liganga-Lilonga, Iringa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2006

    Tatizo lipo hapo ziwa Nyasa mpaka wa kimataifa unaonyesha kuwa ziwa nyasa lipo malawi lote. hakuna sehemu ya ziwa nyasa tz.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2006

    Wewe maggid sio Gabacholi wewe. Kama ni Gabacholi safi tu vijana wanarudisha mali mnazotuibia wahindi. Wahindi wezi sana, mhindi unafanya biashara ya mabilion lakini huna hata kibanda Tz kama sio kutuibia nini? Kwa nini humna investment za kudumu tz mnatubia mnahamishia uchumu wetu Kanada tu. Iko siku mtaondoka tu tutakapochukua nchi yetu wenye nchi. Biashara zenu za kiwizi wizi.

    ReplyDelete
  8. Tatizo haliko kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi. Tanzania tuna strip nyembamba sana kama inavyoonekana kwenye ramani. Kwa sasa ndio haki yetu labda tudai upya. Kasoro anayoitaka Michuzi iko kwingine, ambako sijakung'amua bado.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 09, 2006

    mimi nionavyo ni kwenye ziwa nyasa hakuna mpaka wa kimataifa kati ya Malawi na TZ, TZ haina sehemu yoyote katika ziwa hilo

    ReplyDelete
  10. Nadhani mpaka wa Malawi na Tz hupita katikati ya ziwa Nyasa na si pembeni kama inavyoonekana.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 09, 2006

    Mpaka wa Kutenganisha TZ na Malawi katika ziwa nyasa haupo. Pia ziwa victoria upande wa kenya limepunjwa. Sasa Bwn Michuzi jee utatubandikia kila picha tunayoomba wote tuliopatia? Binafsi naomba picha yakwako na mkeo pamoja na familia yako!

    ReplyDelete
  12. Muhidini,
    Nafikiri tatizo kubwa lipo kwenye huo Ziwa Nyasa - ambapo mpaka hauonyeshwi kabisa. Kama utachukulia dark blue ni mpaka - inakuwa shida hasa kwa kuwa itakuwa inaonyesha kuwa Tz haina sehemu yoyote katika ziwa Nyasa.
    Utata huu ni wa muda mrefu sana (kama sikosei, tangu nipo darasa la tano (1975 -ok tayari wababe weshaanza kunizoza - kumbe haka kajamaa kikongwe - anyway:)tangu nipo darasa la tano nilikuwa nikisikia kuhusu hiki kizaa zaa. Nakumbuka na nyimbo za kumsuta Kamuzu Banda tuliimba!
    KUhusu kwenye bahari ya Hindi - ni kwa vile tu haionyeshwi. Lakini huo mpaka wa kaskazini huwa haufuati mategemeo ya watu unapoingia sehemu za baharini -huwa kuna kitu kama "kiwiko" unapinda kaskazini na kuizunguka Wete - kwa eneeo kubwa tu.
    Kuhusu Ziwa victoria - ni kweli mpaka unaotenganisha Kenya & Uganda haupo sahihi - Kenya imeminywa sana (Kenya na Uganda wana nusu nusu ya sehemu inaypbaki baada yakutoa Tz ambayo ipo sahihi BUT - that is really none of my Business!
    TATIZO kubwa! Ramani hii ndiyo iliyopo kwenye "World Factbook" inayomilikiwa na CIA. Imekuwepo hapo siku nyingi, lakini nadhani hakuna anayejali kuwashitua jamaa - kuwa ramani hiyo ina kasoro. Kwa upande wangu hii ni kasoro muhimu hasa kwa kuwa - uki "google" Tz - guess ni mtandao gani unakuja kwanza - "World Factbook"
    * Kwa sababu ya kukaa kimya - ramani hiyo hiyo (kasoro rangi) ndio imetumika kwenye mtandao wa "Infoplease" ambapo kuna - atlas, Encyclopedia n.k
    *Kweli mzozo umetulia - lakini nani kashinda? Ningekuwa mMalawi - ningesubiri kupata wakati muafaka. Ramani hii itaendelea kugawanywa ma na kutumia, na in Just at the right time...., kutakuwa na a critical global mass ambayo itakuwa inafahamu mpaka huu tu! Then, nitazua mjadala mwingine - Wakati huo, itabidi Tz ifanye kazi ya ziada kujaribu kubadilisha uelewa (perception za dunia - Mambo yale yale ya "Njoo Kenya upande mlima wetu Kilimanjaro...!"
    - Kalagh'abao - wajinga ndio waliwao"
    Ned

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 09, 2006

    Mpaka wa bahari ya indian ocean na mpaka wa lake nyasa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 09, 2006

    and that's why people they call it free water or International territory

    ReplyDelete
  15. Mpaka wa ziwa Nyasa hauna tatizo lolote. Ndivyo wazungu walivyogawa. Tanzania(then Tanganyika) tuliambulia a very parochial strip kama inavyoonekana kwenye ramani. Tatizo analolitaka michuzi liko kwingine sio nyasa.

    Mkumbuke pia jina halisi la ziwa hili ni ziwa malawi. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani linahodhiwa na malawi. Hata jina 'nyasa' ni jina pia la nchi hiyo. Wakati wa ukoloni nchi hiyo iliitwa 'nyasaland'

    Walimu shuleni walikuwa wanatudanganya kwa kuchora mstari(mpaka katikati). Nao walikuwa wanadanganywa na vitabu vilivyoandikwa na maamuna wa jiografia. Sehemu ya ziwa nyasa Tanzania ni nyembamba kama inavyoonekana katika ramani. Lakini kwa uhalisia ukiwa pale ziwani ni sehemu kubwa tu huwezi kudhania ni ndogo hivi. Watu wanavua samaki (mbasa) na samaki wengine na shughuli zingine zote za ziwa. Nimesafiri kwa meli ziwa nyasa.

    Kuhusu ugomvi wa mpaka kati ya tanzania na malawi tutofautishe kati ya ziwa na mto. Ugomvi uko kwenye mto Songwe ambao ni kama malaya hivi. Ni matokeo ya river miendering. Masika ya mwaka huu sehemu ya ardhi inakatwa kabisa inakuwa malawi, mwaka unaofuatia sehemu ilele inakuwa Tanzania. Ugomvi kati ya Marehemu Ngwazi Hastings Kamuzu Banda na Hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuwa katika mto Songwe, sio ziwa nyasa.

    Labda sasa tudai upya kuwa tulidanganywa katika Berlin conference (Nov 1884/Febr 1885)na kupewa sehemu nyembamba hivi. Lakini kabla hatujadai, hiyo ndio haki yetu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 10, 2006

    sio kuwa wanadanganya hiyo dispute ipo na haijapata kupata ufumbuzi. Ni kwamba malawi na Tanzania wako ktk mazingira ya kuelewana ila isingekuwa hivyo ungesikia mtafaruku juu ya mpaka ktk ziwa nyasa/malawi. Kwa maelezo zaidi nenda kasoma habari kwenye CIA fact book sehemu ya Tanzania International disputes

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 10, 2006

    michuzi embu tuambie basi. tumechoka kusubiri

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 10, 2006

    MICHUZI UMEENDA LIKIZO AU? NA KAMA NDIO HATUAGANI? KAMA SIO UKO WAPI LEO? NIMEKUMISO JAMANI.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 10, 2006

    hivi nyie mnaosema hakuna mpka kati ya tanzania na malawi macho yenu yamekosa mchicha? Hebu angalieni vizuri mpaka ulipopita.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 10, 2006

    sijapata ! lakini naomba picha ya salum londa, ni mjomba wangu ..yeye ni kiongozi serikalini !!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 10, 2006

    according to mpaka uliopo ina maana tz hatuna ziwa nyasa liko malawi na kidogo nsumbiji namtumbo kulie tuu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 10, 2006

    Mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi una historia ndefu. Je ziwa nyasa liko Tanzania na Malawi au liko Malawi tu? Mnakumbuka nyimbo zile tulizokuwa tukimuuimba Kamuzu Banda. Kuna wakati Nyerere alitoa hotuba akatupa kisa kile cha Kamuzu Banda alivyomwendea Nyerere na ramani kuukuu akimthibitishia kuwa ziwa lile liko Malawi. nyerere akamfukuzia mbali!

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 10, 2006

    mstari wa bluu unaonyesha mpaka wa ziwa na si nchi hivyo basi kama tunasema ziwa
    nyasa lipo tz ina maana na malawi ni sehemu ya tz!!! na kama tunashikilia mpaka umewekwa kwa rangi nyeusi baina nchi na nchi basi ZIWA NYASA HALIPO TZ....na ina maana kwamba yale maji ya ziwa nyasa tunayaona hayo hapo na hatutakiwi hata kuyagusa ukiogelea tu humo malawi ina haki kukushitaki.

    Nyerere ndio nilikuwa nampendea hapo UBABE!!!! bro sahizi hapa angebaki kuchekacheka tu mpaka wanachukua chao.

    ReplyDelete
  24. mpaka wa Malawi na Tz hupita katikati ya ziwa Nyasa na si pembeni kama inavyoonekana.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 10, 2006

    MARTHA,KTK UKOO WENU MPO WANGAPI?NA WANGAPI NI WANAMUZIKI?SASA ARUSHA KWAYA UMEMWACHIA NANI?

    ReplyDelete
  26. samahani kwa kuhitimisha mjadala nikiwa nimechelewa. ila napenda kusema wote waliosema kama dada martha hapo juu wamepatia. vile vile namshukuru ndesanjo kwa kutoa mwanga zaidi, japo kiduuuuchu.

    ni kweli tatizo la mpaka wa malawi na tanzania (sio kwenye ziwa nyasa tu, hata mto songwe ambao ukujaa hufanya wakazi wa mipakani aidha wa tanzania wajikute malawi, na wa malawi wajikute bongo.

    hizi nchi mbili zimeunda tume ya pamoja juu ya swala hili na sasa mwenyekiti wake ni mama sijaona, katibu mkuu wizara ya ardhi, ili kujua namna ya kubishana bila kugombana.

    vile vile kaa ukijiua kwamba wamalawi huliiza ziwa nyasa ziwa malawi kwani kwao neno `nyasa´ ni ziwa (nakubali kukosolewa kama si sahihi).

    nikirudi bongo ntabandika stori yote kama ilivyo. naomba kutoa hoja...

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 15, 2006

    Ulituahidi atakaepatia utampatia picha yoyote aliyoomba. Binafsi niliomba picha ya familia yako.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 15, 2006

    Michuzi line
    mstari wa ziwa nyasa unatakiwa kuamba na tanzania Ziwa la nyasa liko Malawi
    Sidi

    ReplyDelete
  29. ni kweli nimeahidi kutoa zawadi ya picha. sasa nimpe nani nimnyime nani, maana karibu wote mmepatia na zawadi ni moja tu...

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 21, 2006

    michuzi hili ni ombi la mwisho naomba picha ya salum londa ! kama unayo sawa kama hauna sawa !!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...