Home
Unlabelled
katalambula
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huyu Jamaa pamoja na E.Musiba ni vichwa katika stori za kipelelezi. Ila mwenzake naona kaacha siku hizi utunzi. Kwa wale wanaotumia Reli ya Kati kuna stesheni moja inaitwa 'Igalula', ndipo huyu jamaa alipozaliwa na kusomea shule ya msingi. Namuombea maisha marefu na afya njema zaidi.
ReplyDeletesio igalula bro, ni "kaliua" kama sijakosea
ReplyDeletembona nasikia Elvis Musiba nyingi ya hadisi zake katafsiri kutoka novo wa kizungu? na kufanya sligght changes tu. Kwa maana ingine ameprajiaraizi novo za watu wangine!
ReplyDeleteHivi jamani mnaikumbuka hadithi ya Lawalawa Tabora? Sijui aliiandika Mzee Katalambula, sina uhakika.Bonge la stori ilikuwa, Lawalawa aligonganisha barua moja kwa mume moja kwa mpenzi, akakosea bahasha , ya mume ikaenda kwa mpenzi na ya mpenzi ikaenda kwa mume!
ReplyDeleteMnakumbuka hilo sheshe? Itakuwa bonge ya movie wakii akti.
Hongera sana Mzee Katalambula!
Kwa kweli Katalambula ni gwiji wa riwaya. Watu wa darja lake ni kama Aristablus Elvis Musiba na Ben Mtobwa. Huyu ni gwiji hasa wa riwaya pendwa. Waandishi chipukizi kama Shigongo wanapaswa kuiga mfano wa magwiji waliotangulia katika fani kwa kutunga tungo zinazogusa maisha ya jamii waliyomo.
ReplyDeleteKiki, naomba kutofautiana nawe kidoogo. Katalambula huwezi kumuweka daraja moja na E.Musiba na Mtobwa kwa vile hawa wawili theme za riwaya zao nyingi zilikuwa ni Action na zilikuwa na muelekeo wa kukopiwa kutoka Novel za kizungu.
ReplyDeleteMzee Katalambula unaweza kumuweka daraja moja na akina Euphrace Kezilahabi aliyetunga Roza Mistika na Dunia Uwanja wa Fujo ama mzee Said Muhamed Abdullah kama sikosei aliyetunga Kisima cha Giningi, Siri ya Sifuri na Vinginevyo...!
Anon wa 6:36 pm huyo ni wa igalula mi natoka nae kijiji kimoja na no jirani yetu pale iga'la
ReplyDeleteNampa hongera huyu jamaa ni mahiri sana mungu ampe maisha marefu. Kuna waandishi wazuri Tanzania sijui wamepotelea wapi mfano huyu aliyekuwa anaitwa SAM KITOGO. Nakumbuka vitabu vyake km NITAKUFA NAE, CHA MOTO UTAKIONA, na kadhalika. Wengine ni kama kina Eddie Genzel wa Morogoro..jamaa ni mahiri sana hawa.
ReplyDeleteKaka Chesi nakubaliana nawe. Katalambula daraja lake ni kin aKezilahabi, Ruhumbika na Shafi Adam Shafi kwakuwa riwaya zake zinaangukia katika kundi la riwaya dhati.
ReplyDelete