mtunzi mahiri wa faraji h.h. katalambula alivyo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2007

    Huyu Jamaa pamoja na E.Musiba ni vichwa katika stori za kipelelezi. Ila mwenzake naona kaacha siku hizi utunzi. Kwa wale wanaotumia Reli ya Kati kuna stesheni moja inaitwa 'Igalula', ndipo huyu jamaa alipozaliwa na kusomea shule ya msingi. Namuombea maisha marefu na afya njema zaidi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2007

    sio igalula bro, ni "kaliua" kama sijakosea

    ReplyDelete
  3. mbona nasikia Elvis Musiba nyingi ya hadisi zake katafsiri kutoka novo wa kizungu? na kufanya sligght changes tu. Kwa maana ingine ameprajiaraizi novo za watu wangine!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2007

    Hivi jamani mnaikumbuka hadithi ya Lawalawa Tabora? Sijui aliiandika Mzee Katalambula, sina uhakika.Bonge la stori ilikuwa, Lawalawa aligonganisha barua moja kwa mume moja kwa mpenzi, akakosea bahasha , ya mume ikaenda kwa mpenzi na ya mpenzi ikaenda kwa mume!
    Mnakumbuka hilo sheshe? Itakuwa bonge ya movie wakii akti.
    Hongera sana Mzee Katalambula!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2007

    Kwa kweli Katalambula ni gwiji wa riwaya. Watu wa darja lake ni kama Aristablus Elvis Musiba na Ben Mtobwa. Huyu ni gwiji hasa wa riwaya pendwa. Waandishi chipukizi kama Shigongo wanapaswa kuiga mfano wa magwiji waliotangulia katika fani kwa kutunga tungo zinazogusa maisha ya jamii waliyomo.

    ReplyDelete
  6. Kiki, naomba kutofautiana nawe kidoogo. Katalambula huwezi kumuweka daraja moja na E.Musiba na Mtobwa kwa vile hawa wawili theme za riwaya zao nyingi zilikuwa ni Action na zilikuwa na muelekeo wa kukopiwa kutoka Novel za kizungu.
    Mzee Katalambula unaweza kumuweka daraja moja na akina Euphrace Kezilahabi aliyetunga Roza Mistika na Dunia Uwanja wa Fujo ama mzee Said Muhamed Abdullah kama sikosei aliyetunga Kisima cha Giningi, Siri ya Sifuri na Vinginevyo...!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2007

    Anon wa 6:36 pm huyo ni wa igalula mi natoka nae kijiji kimoja na no jirani yetu pale iga'la

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2007

    Nampa hongera huyu jamaa ni mahiri sana mungu ampe maisha marefu. Kuna waandishi wazuri Tanzania sijui wamepotelea wapi mfano huyu aliyekuwa anaitwa SAM KITOGO. Nakumbuka vitabu vyake km NITAKUFA NAE, CHA MOTO UTAKIONA, na kadhalika. Wengine ni kama kina Eddie Genzel wa Morogoro..jamaa ni mahiri sana hawa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2007

    Kaka Chesi nakubaliana nawe. Katalambula daraja lake ni kin aKezilahabi, Ruhumbika na Shafi Adam Shafi kwakuwa riwaya zake zinaangukia katika kundi la riwaya dhati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...