afisa uhusiano ubalozi wa marekani jeffery salaiz akiongoea na wahariri wa vyombo vya habari leo kuhusiana na libeneke la ujio wa rais george bush wa marekani anayetarajiwa kutua bongo februari 16 na kupiga mbonji siku kadhaa dar na a-taun. of kozi jamaa kamwaga mkwara mbuzi kwamba hii ni bahati ya mtende kwa mtu kama bush kupiga mbonji siku kibao bongo, bila shaka na zile shilingi takriban bilioni 700 na ushee za changamoto ya milenia nchi yake ilizotoa anataka ajue zitavyotumika kwani hakuna nchi afrika iliyowahi kuvuta mkwanja hevi kama huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ni kweli kama alivyosema ni bahati ya Mtende.Viongozi wengine wenye pesa hata Kuliko Bush huleta misaada ya ajabu ajabu tu kama vile Tende za kula mwezi wa Ramadhani wakati watanzania tuna matatizo makubwa kuliko kuletewa tende! Huyu analeta PESA siyo tende.Hii ni bahati ya mtende.

    ReplyDelete
  2. Anon hapo juu swala sio pesa! Tanzania tuna pesa nyingi sana. Swala ni je hizo pesa zitamnufaisha nani? au zitaishia kwenye account za wajanja (kama ilivyo kawaida) baadala ya kununua madawa na kujengea shule....

    ReplyDelete
  3. Bahati Bush kuja kwetu, mie sioni bahati yeyote. Kama fedha tunazo nyingi tu ambazo zinatafunwa huku kwenye migodi ya madini na kule BoT na kwingineko kwingi ambapo wanahabari hawajapafikia.
    Ingekuwa ni Shilingi yetu imepanda thamani, mie ningeona ni bahati kuliko Bush kuja na kumbonji hapa Tz.
    Lakini Enewey, mwache aje tuone hiyo bahati anayotupigia nayo mkwala huyu afisa ubalozi.

    ReplyDelete
  4. amechoshwa na siasa anakuja kupumzika mwenzenu. mpokeeni lakini, si unajua sisi watanzania ni wakarimu.

    ReplyDelete
  5. nasikia DELTA FORCE (crack commandos and elite bodyguard unit)wameshaingia tanzania,be very afraid hii mitu,ni afadhali ukutane na moto wa jahanam,so lethal that the govt of USA denies the existence of this unit,president musharaf of pakistan owes his continued existence in this world to this crack unit

    ReplyDelete
  6. Nyie acheni upumbavu mbona mnakuwa mmelala hivyo hebu amkeni huyo jamaa anakuja hapo kuja kuangalia kama kuna uwezekano wa kusecure mikataba ya mafuta na other natural resources nyie mnaona bahati ya mtende kumbe bahati hiyo wanaifaidi wachache tuamke watanzania ohhh nyie ndo yaliwa hivyoooo!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. HIYO GESI ILIYO GUNDULIWA NA KUFANYWA (SIRI) NDIO JAMAA ATAZUIA AU

    ReplyDelete
  8. mi sina zaidi la kusema zaidi ya analake jambo huyo,Misaada mingine yaweza hatarisha nchi jamaniiiii.kuna mithali inasema bure inauwa.

    ReplyDelete
  9. Gesi, mafuta, madini, na ukichukulia china anavyokamata africa marekani inabidi itafute washkaji wa kumpelekea nishati kwake. Mie nakubalia na annony hapo tuangalie hizi safari za viongozi wengine jamani wa kutoka nchi za nje sio tu mgeni njoo mwenyeji apone.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...