viongozi wa Kilimanjaro FC wakisherehekea ubingwa wa kombe la mbuzi mwaka huu baada ya kuifunga FC Bongo bao 4-3 kwa shiiiiida leo huko Stockholm
picha ya pamoja ya Kilimanjaro Fc (bluu) na FC Bongo (Yanga) kabla ya gemu. Mwenye kibandiko ni mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya Kilimanjaro FC. Chini Kocha wa FC Bongo Ezza Scolari akiwa ametingwa na mashabiki wakitaka kujua kwa nini kachezesha kikosi cha pili mechi muhimu kama hiyo, akiwaacha jamaa wa sweden wakitambaHabari ambazo si za uhakika sana zinasema leo Kilimanjaro FC ya wabongo wa Sweden imeilaza kwa taaaaaaabu FC Bongo ya wabongo wa Finland bao 4-3 katika mechi yao ya kombe la mbuzi huko Stockholm.


Mlezi na kocha wa FC Bongo EZZA SCOLARI inasemekana anampango wakuhamia Sweden baada ya kipigo hicho cha aina yake.


Watanzania wa Finland wameonesha mpira wa hali ya juu na tumefurahia kiwango chao ni cha kimataifa,lakini Watanzania wa Stockholm wamethibitisha kuwa wao ni mabingwa na scandinavia.Pokeeni salaam zetu Watanzania wa Norge na Denmark tunawakaribisha.

Khalifa ZAM
Nordkapsgatan 15,1tr
164 36 Kista
SWEDEN
Tel.nr. +46 8 6320116
Mobil. + 46 737234412
www.kilimanjaroclub.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Haa haaaa michu acha majungu!kufunga ni kufungwa tu hakuna tabu wala nn!!!!!!!4-3 haloooooooooo kwa raha zetu,na pilau tumewapa!

    ReplyDelete
  2. FC BONGO FC BONGO KUJITAPA KOTE HUKO KUMBE YALIKUWA MANENO MATUPUUUUU. NAONA VIJANA WA KILIMANJARO WAMEWAROWESHA KWA BAO NNE NA SASA MANENO YAMEWAISHA. NAWAPA PONGEZI KILIMANJARO MNATISHA SANA AU SUNGURA KAMPANDA TEMBO?
    MDAU DENMARK

    ReplyDelete
  3. Zaack nakuona mchumba wa zamani unawakilisha na kakio. Hongereni.

    ReplyDelete
  4. Na Nyie Kilimanjaro FC Mtaishia Kujisifia Tu Hamna Lolote mmekalia Kualika Wenzenu Mkialikwa Nyie Wataenda Viongozi Tu Kwani Wacheza Wote Hamtoki Nje Ya Sweden.FC BONGO Meonyesha Uzalendo Tunawakaribisha Holland...Mdau VIMTO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...