Kwa dhati kabisa kwa niaba ya Familia ya Mpogole, ndugu na jamaa wote tunatoa shukrani zetu kwenu nyote mlioshiriki kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha kusafirisha mwili wa Marehemu ndugu yetu Castory Mpogole.
Msaada wenu kwetu umekuwa wa umuhimu usio na kifani. Hivyo basi hatuna budi kuwashukuru kwa fadhila kubwa mliotutendea.
Aidha tunawashukuru sana kuweza kuchangia gharama zote za kusafirisha mwili wa marehemu hadi nyumbani Tanzania. Huu ni msaada usio kifani kwetu tunasema tena
ASANTENI SANA.
Marehemu Castory Mpogole alizikwa tarehe 20/08/2008 katika makaburi ya familia kwenye kijiji cha Nzivi, tarafa ya Nyololo, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Kwa yote hayo mliyoyafanya ili kufanikisha utaratibu mzima wa mazishi ya marehemu ndugu yetu, sisi kama ndugu tunakuombeeni Baraka nyingi zenye fanaka na mafanikio mema katika shughuli zenu za kila siku.
Sisi tulimpenda Castory lakini Mungu alimpenda zaidi.
CHRISTOPHER J. MASASI
KAKA WA MAREHEMU
NA KWA NIABA YA WAFIWA



R.I.P Castory
ReplyDeletePoleni sana, mimi nilisoma tosamaganga miaka ya 1980, huyu alikuwa na undungu wowote na aliyekuwa headmaster wetu wakati huu, hayati Mzee Mpogole? baada ya hapo bw. christoper masasi unaweza nisaidi kama unayo contact ya bwana mmoja alisoma pale tosamaganga anaitwa Chesco Mfikwa, mi naitwa Mazengo Kasilati, email: mazengo@yahoo.com
ReplyDeletejamani ndugu yangu
ReplyDeletehazina ya pekee hii kwa sie wanyalu imetutoka.
Bwana ametoa,,,ametwaa jina lake lihimidiwe
wa-kuboma