balozi wetu wa kudumu huko umoja wa mataifa mh. balozi dk. augustine mahiga, akiongea na waandishi wa habari jijini dar leo kuhusu ujio wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa mh. ki-moon ban kesho kwa ziara ya siku mbili. kulia ni mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa bongo, oscar fernandez taranco, na kushoto ni ofisa alieambatana na balozi mahiga.
ili kuona video ya mkutano huo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sikujua Tanzania tuna "balozi wa kudumu."

    ReplyDelete
  2. "Tarehe February 25, 2009 8:02 PM, Mtoa Maoni: Banzi
    Sikujua Tanzania tuna "balozi wa kudumu." "

    Sasa unajua

    ReplyDelete
  3. "Tarehe February 25, 2009 8:02 PM, Mtoa Maoni: Banzi

    Sikujua Tanzania tuna "balozi wa kudumu." "

    Sasa Unajua

    ReplyDelete
  4. Balozi wa kudumu tunae - ila mimi nilipoona Ki-Moon nikafikiri mwanamuziki - rapa...

    ReplyDelete
  5. bongo kulikoni mbona tunahost wageni wengi hivyo? si tutaishiwa? wangechukua basi hata muda kuja....juzi tuna mgeni toka china, mara japani, sasa UN...tutachacha sana before we know what's up with them .....

    ReplyDelete
  6. Wewe Banzi na wenzio mwashangaa nini kuweko kwa balozi wa kudumu. Hicho ni cheo ambacho mwakilishi yeyote wa Rais kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa huitwa Permanent Representative yaani Balozi wa kudumu. Haimaanishi kuwa Dr Mahiga kama binafsi yake ni wa kudumu. Hapana ila ile nafasi anayoishikilia ndivyo inavyoitwa. Kwa hiyo anaweza akaondolewa na akapelekwa Banzi na akawa balozi wa kudumu. Mmeelewa sasa?

    ReplyDelete
  7. Wewe Banzi na wenzio mwashangaa nini kuweko kwa balozi wa kudumu. Hicho ni cheo ambacho mwakilishi yeyote wa Rais kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa huitwa Permanent Representative yaani Balozi wa kudumu. Haimaanishi kuwa Dr Mahiga kama binafsi yake ni wa kudumu. Hapana ila ile nafasi anayoishikilia ndivyo inavyoitwa. Kwa hiyo anaweza akaondolewa na akapelekwa Banzi na akawa balozi wa kudumu. Mmeelewa sasa?

    ReplyDelete
  8. balozi wa kuduma,,,mahiga,,
    bela kamwene mnoge,makaasi,wanoge wana uko ku-ulaya,ale bela!ndili ipaa bongo..

    ivi ina mana ndo forever yan mtu mwingine hatakiwi kuchaguliwa badala yake???siasa za wapi izo?
    nani anamlipa mshahara UN au TZ?

    ReplyDelete
  9. Wewe Anonymous wa Feb 26, 9:59 AM

    Sasa kama Mahiga mwenyewe sio balozi wa maisha ila "kudumu" ni uwepo wa ule ubalozi basi cheo chochote kile duniani tunaweza kukiita cha kudumu, maadam kipo kila siku bila ya kujali nani anakikalia.

    Hata Kikwete tunaweza kumuita Rais wa kudumu! Eeeeh, maana cheo chake si kipo bwana, atoke asitoke, cheo chake kipo, au? Kikwete nae ni Rais wa Tanzani wa kudumu?

    Kama sio, na Mahiga nae hatuwezi kumuita balozi wa kudumu eti kwa vile kile kiti cha ubalozi ndio cha kudumu.

    Kama nakosea nitajie cheo ambacho sio cha kudumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...