mdau kichere w. kichere na mai waifu wake wakikata ndafu katika ukumbi wa mgulani jkt usiku huu baada ya kumeremeta katika kanisa katoliki la mtakatifu maxmilian mary kolbe la mwenge. wote ni wafanyabiashara ya mahindi na ndizi kule rorya na tukuyu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Michuzi shekhe inakuwaje hapo tena? nimeangalia hadi nikamuita my waifu mke wangu aje kunisaidia kuangalia lakini sijaona ndafu hapo naye akasema anaona kitu kama ugali kikiwa na shepu ya libugando (bugando kwa watani zangu wasukuma ni kitu chochote chenye ghorofa)

    ReplyDelete
  2. jamani ongereni sana maarusi, kwani bado tunaamini na hatuta acha kuamini kwamba Alicho kiunganisha mungu mwanadamu kamwe asikitenganishe!!!!!!!!

    ila msisau kwamba ndoa ni alama inayoonyesha hapo juu kabisa ya hiyo keki yenu nzuri sana!!!!
    Ongereni sana!!

    Mdau wa canada!

    ReplyDelete
  3. Hivi hiyo ni keki au ndafu am sorry but mi naona kama keki

    ReplyDelete
  4. MICHUZI HIYO NI NDAFU AU KEKI...???..ANYWAYZ BEST OF LUCK KWA MAHARUSI..

    ReplyDelete
  5. Wewe anony. uliyejitambulisha mdau wa Canada hatusemi "ongereni"? Hicho ni kiswahili cha ki-Canada labda!!!. Tunasema "hongereni" Tafadhari jifunze kiswahili sanafu na sio kuharibu lugha za watu.
    Mdau

    ReplyDelete
  6. mdau hapo juu hakuna "kiswahili sanafu" kuna "kiswahili sanifu.nyani kucheka kundule.
    Mdau wa Buja.

    ReplyDelete
  7. hapo juu mdau wa 11:23am, tunasema TAFADHALI na sio TAFADHARI... r u from Bukoba??? Watch out b 4 u COMMENT...

    ReplyDelete
  8. Napenda sana kukosolewa!
    Jamani wandoa hongereni!!!!
    Ila jamani tusiwaonee wivu,tunachotakiwa ni kuwapongeza kwani wametimiza maandiko ya kitabu cha mungu na pongezi zangu kwa wafamilia hii ni ya Kiroho!!!!!!
    Hongereni sana na mungu awabariki mpate familia bora!!

    Mdau canadaa!!

    ReplyDelete
  9. siwajui but siyo mbaya kumsifia mtu akifanya kitu kizuri...kwakweli mmependeza sana na cake yenu ni unique! Mungu awabariki siku zite.

    ReplyDelete
  10. Okay, guys this is not about you or how good your Swahili is. It is about the bride and the groom.

    Hongereni maharusi.

    ReplyDelete
  11. "Ongereni" , "Tafadhari" na "Sanafu", mimi sioni tofauti yake, wewe mwenyewe lugha inakupiga chenga halafu unathubutu kukosoa watu!
    ama wewe kweli mcheka kundule!

    ReplyDelete
  12. hongereni sana maharusi.lakin hakuna ndizi za kuuza wala mahindi huku Rorya.hapo inakuwaje?mnatupiga chogi hapo!!!

    ReplyDelete
  13. mmmhhhh, wafanyabiashara ya mahindi na Ndizi?, haya bana

    ReplyDelete
  14. We Anony wa saa 11:23 unajifanya kukosoa wenzako wakati we mwenyewe full kuchapia, huwa hatusemi KISWAHILI SANAFU ni KISWAHILI SANIFU, haloooooooooooooooooooooooo!

    Kibajaj

    ReplyDelete
  15. kwani hamjaelewa na iyo michapio?
    wafanyabiashara?sasa mtashare mtaji na kubadili mwelekeo kibiashara au ndo ndoa za siku izi "chako chetu,changu ni changu"
    kaaaaaaaaazi kweli
    mmependeza

    ReplyDelete
  16. ni wafanyabishara wa mahindi hao????uongo mtupu!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Elimu kweli ni kitu muhimu sana, ni afadhali kutunga uongo unaofanana na ukweli, huko kujifanya ni wafanyabiashara ndio wameharibu kabisaaa

    ReplyDelete
  18. MICHUZI ACHA KUBANA MISAMIATI KAMA NYANI HAONI KUNDULE HUONA LA MWENZIE TU . HUO NI MSAMIATI WEKA COM YANGU YA JANA ASHA KUM SI MATUSI BWA SHEM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...