HABARI NJEMA KWA WA TANZANIA WOTE 

CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI MAREKANI KINAPENDA KUWAFAHAMISHA WATANZANIA WOTE KWAMBA KIMEKAMILISHA MIPANGO YAKE YA KUONYESHA SINEMA ZINAZOHUSU TANZANIA KATIKA KUMBI MBALI MBALI ZA MAREKANI. SINEMA YA KWANZA ITAONYESHWA KATIKA UKUMBI WA AMC ULIOPO KATIKATI YA JIJI LA KANSAS CITY, MISSOURI. KWA MALEZO ZAIDI KUHUSU SIKU NA MDA SOMA HABARI HAPO CHINI 
 

Jumba la Sinemal itakalotumika kuonyeshewa sinema hiyo: 

AMC Theatres

1400 Main Street.

Kansas City, MO 64105 
 

Chama Cha Mapinduzi nchini Marekani kinapenda kuwajulisha watanzania wote kuwa kimekamilisha mipango yake ya kuonyesha sinema zenye lengo la kuitangaza tanzania katika kumbi mbali mabali nchini Marekani. Sinema ya kwanza itaonyeshwa katika kumbi la AMC lililopo katikati ya jiji la Kansas City, Missouri siku ya Alhamisi ya tarehe 23/ 04/2009 kuanzia saa 1:45 usiku.

Kabra ya sinema hiyo video ifuatayo http://www.tanzaniatouristboard.com/pages/ttb_video.php itaonyeshwa. Uongozi wa ccm nchini Marekani unatoa pongezi kwa wote walioshiriki katika kufanikisha mpango huu.

Address kamili ya ukumbi huo wa AMC ni:

AMC Theatres

1400 Main Street.

Kansas City, MO 64105

Pia tunapenda kuwafamisha kuwa CCM nchini marekani imefanikisha Tanzania kujiunga na shirika la Ethnic Enrichment Commissiner linalotumika kuzitangaza nchi mbali mbali wanachama katika nyanja za kiuchumi, utamaduni, na mambo yote yanayousiana na nchi mwanachama. Kwa taharifa zaidi kuhusiana na hili shirika tembelea tovuti yao na ukibonyeza pale panaposema Countries utakuta bendera ya Tanzania tayari imeshatundikwa na ukibonyeza kwenye bendera ya nchi yetu basi utakutana na mambo yote yanayohusu tanzania. Tovuti yao ni www.eeckc.org

Kwa taharifa na maelezo zaidi wasiliana na wafuatao hapa chini

Michael Ndejembi--Mwenyekiti CCM makao makuu nchini Marekani 713 384 4567

Miraji Malewa--Katibu mkuu CCM makao makuu nchini Marekani 832 741 4452

Deogratias Rutabana--Mwenyekiti CCM shina la Kansas City, Missouri - Marekani 816 812 5495

Mungu Ibariki Tanzania.

Taarifa hii imeletwa na uongozi wa CCM nchini Marekani

www.ccmmarekani.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. CCM kumbe wako mpaka huku. Dah. mi sikujua. Kadi mnazo? Ninataka kujiunga CCM sasa kwani wanamageuzi bado wanaendealea kugeuka na kugeuzana! Nitumieni kadi ya CCM miye!

    ReplyDelete
  2. habari nzuri , tumefurahi kusikia hivyo , tunamatumaini na mengi mazuri yatakuja

    ReplyDelete
  3. Namimi naomba card,Inaweza ikanitoa nikirudi Bongo LINE ya kupata UFISADI.

    ReplyDelete
  4. CCM OOYEE!!!!
    KWAKWELI CCM MAREKANI MNASTAHILI PONGEZA KWA JITIHADA ZENU, NYINYI NI WASAFIRI BADO MPO NJIANI, NA NI MATUMAINI YANGU MTAFIKA PALE MNAPOKWENDA.
    "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
    "SALAMU KUTOKA UNITED KINGDOM (UK)"

    ReplyDelete
  5. Mimi nimegundua kuwa hawa jamaa wa ccm nchi za nje mitizimo yao ni mizuri. Nimependezwa sana na hili tangazo na nawaombea wazidi kuitangaza nchi yetu.


    Michuzi na wewe kazi yako ni nzuri sana.

    ReplyDelete
  6. Hivi nyinyi wenzetu mliopo nje ya nchi,amna chama kingine mnachoshabikia zaidi ya ccm? maana kila mkitoa maoni yenu ama mnapokutana katika mambo yenu ni ccm tu ndio inayozungumzwa, mnakatazwa kujiunga ama kushabikia vyama vingine? mbona mnatupa hofu.

    ReplyDelete
  7. Watanzania wenzetu mliopo nje ya nchi wote mkifanya mambo kama haya Tanzania yetu itafika mbali sana.

    Namna hii CCM mtatawala daima. Viongozi na wanachama nawapongeza sana kwa mambo mnayofanya sio tu kufanya sherehe kulewa pombe. Nawaomba msikate tamaa maana hata wenzetu wa nchi zingine ndio wanavyofanya wawapo ugenini.

    Mtandao wetu wa jamii kila siku unazidi kutuabarisha. Kazi njema!!!!!Mkuuuuu

    ReplyDelete
  8. vyama vingine bado wako ktk mageuzi jaman,hawana uhakika wa uanachama mguu pande,,,tobo,,,

    ila mmh!!ccm nje za nchi

    ReplyDelete
  9. Hatuna chama cha mapinduzi hapa Amerika ila kuna wapuuzi kadhaa wanaojipendekeza,marekani tunajumuia za watanzania.Huyo mwenyekiti alichaguliwa wapi na nani marekani tuna majimbo zaidi ya 50 Kansas City haiwezi kutuwakilisha watanzania wote Mwenyekiti nakuona kama hujaliangalia hilo kwa upana.
    nawasilisha.
    Mtanzania/Mzalendo.

    ReplyDelete
  10. binafsi nawapongeza sana hawa jamaa
    kwani kazi wanazozifanya ni kwa maendeleo ya tanzania tofauti baadhi ya watu wanavyodhani. nilitaka kumshauri huyu mwenyekiti bwana michael ndejembi kwamba ongea pia na viongozi kule nyumbani ili tuwe na siku yetu hapa marekani, kama vile uhuru day

    ReplyDelete
  11. nadhani we mzalendo ndio mpuuzi kama hata uwepo wa ccm hapa marekani huujui unawezaje kujua viongozi wake wamepetikana vipi, tatizo wajinga wajinga kama wewe mko wengi sana. acha uwendawazimu wako kama huna cha kuandika kaangalie porno.

    ReplyDelete
  12. jamii ya kitanzania inatakiwa kuwa na tabia ya kutambua mchango wa watu kama hawa badala ya kuanza kuwakashfu kama baadhi yetu tunavyofanya. sio tatizo kwa kina ndejembi kusimama na kuwaletea nafasi nzuri kama hii ambayo naamini hata ubalozi wetu haujawahi kufanya, si hivyo tu ni vigumu sana kwa sisi watanzania kuwa na mawazo kama haya ya kuisaidia nchi yetu kama tunapokuwa nje ya nchi. Nadhani ni vizuri kuwapongeza CCM Marekani kwa kazi nzuri ili pia kuwapa moyo wengine wenye mawazo kama haya.

    mwana harakati

    ReplyDelete
  13. CCM hii ya Marekani haiongozwi na wapuuzi wala mafisadi ila ni watu wenye kujua nini wanafanya na kwa faida ya nani, wanaelewa watumie njia gani kufanikisha malengo yao. kama kunajumuia za kutanzania zinafanya nini zaidi ya majungu wakikutana. tujifunze kuheshimu, kutambua na kuzienzi kazi zetu.

    ReplyDelete
  14. Safi sana ccm US hii ni zaidi ya kila kitu. jamani niko marekani kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa sijaona mtu mwenye mawazo mazuri na endelevu kama dogo ndejembi. kuwa na wazo then ukaliweka kuwa kitu halisi kama hivi si kitu kidogo jamani na hasa ukizingatia kuwa mawazo yetu huwa ni wapi nikabebe mabox nilipwe dola nyingi nikamchukue demu wa fulani, sasa ktk kipindi kama hiki watu kibao hawana kazi si rahisi ukawa na mawazo mazuri kama haya. bwana ndejembi we endelea mimi niko pamoja nawe hata ma wife wangu anakusifu sana kwa mambo yako mazuri.

    ReplyDelete
  15. CCM ndio yenyewe na hasa ikiwa na watu kama kina michael mambo huwa mswano sana, sisi tutakuwepo kujionea sinema hiyo mapema kabisa.

    ReplyDelete
  16. watu wengine bwana eti ccm iko hata marekani, we ulitaka iwe mpaka wapi? ikisikia usenge ndio huu kama huipendi kaa pembeni endelea kutongoza wake za watu tuachie ccm yetu tujifanyie mambo usituchanganye mjinga wewe.

    ReplyDelete
  17. e bwana michuzi niulizie kwa hao viongozi wa ccm ni lini wataonyesha huku DC msije mkatusahau.

    ReplyDelete
  18. Mungu wabariki watu wote wenyemitizamo ya kulisaidia taifa letu. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kama wenzetu wanavyofanya nawapongeza siangalii wana tumia nini.

    Kwa wale wenye rohoo za kwanini kwa taifa letu basi mungu waangamizie mbali.

    ReplyDelete
  19. Hawa watu washenzi watupu, kama mmeshindwa kufanya kazi za heshima maofisini hapa US , si mrudi tu TZ mkaendelee na chama. Nyie wawili bado mnafanya kazi za home health kwa vichaa , halafu na shue zenu mmeshindwa kutafuta kazi za ofsi mnataka kila mtu ajiunge na CCM , nyinyi kiwa kama wakubwa wao.
    watu wako busy na kazi bwana hapa Kansas city za proffesional bwana , nyie kazaneni na utumbo wenu wa chama.Najua mtafaidi kugombea ubunge kwa mtindo huo lakini msitake umaarufu kupitia migongo ya wengine hapa.

    ReplyDelete
  20. kweli mambo ni mazuri sana,unajua watu wengine wanapenda majina yao yasikike ila jinsi ya kujitoa hawajui wafanye nini ili atambulike wanaishia majungu na chuki mtu ukibuni kitu chake anaona siyo kitu ila cha kwake ndiyo kitu bwana wewe kama hauna bahati kaa chini utulie fanya kazi yako siyo unajifanya msomi kumbe bure kabisa unapo anza kuzungumzia uelekeo jiangalie wewe mwenyewe upo wApi siyo kulopoka tu na kujiingiza katika mambo ya watu ili upate usawa ukiona hakuna kitu kelele wewe unadhani wao walianza vipi unajitokeza mbele ya watu kumbe wanakudharau tu kazi kukaa kuwadanganya watu tz nina nyumba usa kuna mtz ana nyumba hapa wazaa wenyewe wanahesabika iwe wewe wa kuja jenga nyumbani
    HONGERA NDEJAMBI

    ReplyDelete
  21. Kazi nzuri vijana!!!!!. Nawapongeza kwa juhudi zenu. Naomba endelea kuitangaza nchi yetu. Nchi yetu inaitaji watu wenye moyo huu, naomba mtu hasiwakatishe tamaa hata kido, tutafika.

    Nimependa sana hili tangazo lenu vijana wa CCM mungu awazidishie.

    ReplyDelete
  22. Kweli hii imenigusa. Ninashangaa sana watanzania wanaokwenda nchi za nje na kuiona tanzania kama si nyumbani kwao kama huyu mwenzetu hapo juu anayedai yeye amesoma na anafanya kazi nzuri. Mimi naamini mtu aliyesoma anakuwa na mawazo ya kusaidia ndugu zake kama hawa wenzetu wa CCM wanavyojitolea kulitangaza taifa letu.

    Sizani maoni yote yanatolewa na watanzania wenye akili timamu. Naamini wengine sio ndugu zetu bali ni wale wanaosikia uchungu wasikiapo Tanzania inaendelea

    Mungu ibariki nchi yetu

    ReplyDelete
  23. Iwe ccm,chadema au chama chochote cha siasa/kidinikama mlengho wake ni kusaidi nchi yetu mimi nitajiunga.

    Mawazo yenu ni mazuri ndugu zetu. Sina uakika kama mnapata picha za kisa zaidi. Nitapenda kushirikiana nanyi katika kulitangaza taifa letu

    ReplyDelete
  24. Pia msisaau kuwaeleza wamarekani kuwa nchi yetu inavivutio vingi ikiwa ni pamoja na utulivu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...