MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA SHADYA KARUME AKISALIMIANA NA WANAFUNZI WA SKULI YA MSINGI YA UZINI WAKATI KALIPOWEKA JIWE LA MSINGI LA SKULI YA MAANDALIZI YA TUNDUNI WILAYA YA KATI KUSINI UNGUJA LEO
MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA ZAYEDESA MAMA SHADYA KARUME AKIONDOSHA KIPAZIA KUASHIRIA KUIZINDUWA RASMNI SKULI YA MAANDALIZI YA CHEKECHEA TUNDUNI UZINI JANA

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MAMA SHADYA KARUME AKLIPANDA MNAZI BAADA YA KUIFUNGUWA SKULI YA MAANDALIZI WA WATOTO KATIKA KIJIJI CHA TUNDUNI UZINI WILAYA YA KATI JANA. PICHA NA OTHMAN MAULID WA ZANZIBAR LEO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Majina ya zenji ni burudani tosha yani.

    ReplyDelete
  2. Tunduni! tena Uzini! mmh! yangu masikio na macho!

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani umefika wakati sasa kwa viongozi wetu kuwa realistic, kwani wao ndiyo vioo vya jamii.

    Tungejaribu kuonyesha mifano ambayo ni halisi.

    Mfano kiongozi anapanda mti, tunafahamu kabisa kwamba ukienda shamba hutandiki mkeka au kitenge chini ili usichafuke. Mzingira ya shamba, ili uweze kufanya kazi vema, lazima uchafuke. Viongozi wa ngazi za juu wangekuwa mifano ya kweli ya hali halisi ya mazingira ya mtanzania.

    Tungefurahi siku moja kumuona JK akitupilia mbali jamvi alilotayarishiwa kwa ajili ya kupanda miti, kwani mazingira halisi ya kupanda miti hayahusiani na kutandika jamvi, kitenge au kanga ardhini.

    Inapendeza zaidi kumwona kiongozi akifanya kazi, au kutoa mfano katika mazingira halisi.

    ReplyDelete
  4. kapanda mnazi tunduni uzini wilaya ya kati

    ReplyDelete
  5. hicho kiswahili mi hoi,eti akiondosha pazia,du rahisi kweli kufeli mtihani.

    ReplyDelete
  6. majina ya zenji bwana kama wazenji wenyewe

    ReplyDelete
  7. come on wadanganyika hapo sio tunduni ni tunduuni (inatamkwa tundu-uni)

    ReplyDelete
  8. sawa ni Tuunduni,je mchambawima na Makunduchi ni vipi tupe elimu...

    ReplyDelete
  9. Majina ya z.bar kwa kweli kila siku napata jipya na kali zaidi! tunduuni alafu uzini,
    kuhusu kuweka mikeka sio poa, hata jana Obama alipopanda mti kuadhimisha earth day hakuwa na mikeka (ingawa alipiga gloves )
    teh teh

    ReplyDelete
  10. Kaweka jiwe Tunduni, akapanda mnazi Tunduni, Uzini wilaya ya kati.

    ReplyDelete
  11. Sie wa Mchambawima hatuna lakusema. Tutamsubiri akija Tunduni

    ReplyDelete
  12. Uzini??Tunduni??
    hahahahaaaaa sina mbavu dah!!aya ndo majina ya kiswahili aswaaa safi sana wazenji-Tanzania

    kisiwandui,ubago,bwajuu,nk nk

    ReplyDelete
  13. Ni kwa vile nyani hajioni tu.

    Hebu angalia hii: Zenji Makunduchi, Bongo Kunduchi. Zenji Mchambawima, Bongo Matombo. Zenji Jang'ombe, Bongo Chang'ombe. Hapo kuna kuchekana kweli?

    ReplyDelete
  14. Bwahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    Chang'ombe kinini?

    ReplyDelete
  15. Ukishakua awali Tunduni!!!!

    ReplyDelete
  16. tumekusikieni wabongo, mwaka 2010 wazenji tutabadilisha majina ya mitaa yetu na tutaita, newyork badala ya tunduuni, na capetown bdl ya uzini, yorkshire bdl ya makunduchi, eastham bdl y mchambawima, lkn sharti letu 1, msije mkatuambia hatuutaki uswahili

    ReplyDelete
  17. kaka michuzi naomba kuuliza mama shadia amepanda mnazi au ameotesha mnazi?

    ReplyDelete
  18. hapa zenji hapana majina ya kuchekesha kama pemba huko utakuta :chaka la kati,mpika tango,maziwa ya ngo'mbe,jadida,utaani,mchanga mdogo n.k.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...