Na David Azaria Geita

ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya zoezi la upigaji wa kura kufanyika katika jimbo la Busanda wilayani Geita mkoani mwanza,Helikopta ya CHADEMA imewasili kwenye jimbo hilo kwa ajili ya kuendeleza kampeni za chama hicho na kuuteka mamia ya wananchi wa jimbo.

Helikopta hiyo iliwasili katika mji mdogo wa Katoro ambapo ndipo yalipo makao makuu ya jimbo la Busanda majira ya saa 8;05 mchana,na kutua kwenye kiwanja cha nyumba ya kulala wageni ya Twiga iliyopo mita 50 kutoka katika kituo kidogo cha polisi cha Katoro,ambapo ndipo walipofikia viongozi kadhaa wa chama hicho pamoja na wapiga Debe wao.

Kuwasili wa helikopta hiyo kuliuzizma mji wa Katoro na kuwafanya mamia ya wananchi kukimbia kuelekea katika viwanja hivyo kwa ajili ya kushuhudia kuwasili kwa helikopta hiyo,na mara baada ya kuwasili na viongozi wa chama hicho kuanza kushuka wakiongozwa na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe,mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika kwenye eneo hilo walianza kushangilia kwa kunyoosha vidole viwili juu.

Kabla ya kutua katika eneo hilo Helikopta hiyo ilizunguka mji wa Katoro mara moja na baada ya viongozi hao kusalimiana na wananchi,baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliondoka na helikopta hiyo kwa ajili ya kuanza kampeni huku zikiwa zimesalia siku nne tu kabla ya zoezi la upigaji wa kura kufanyika.

Habari kutoka ndani ya CHADEMA zimesema kwamba wakati Jumanne kilitarajia kufanya mikutano mitatu,kuanzia leo chama hicho kitakuwa kikifanya mikutano sita hadi siku ya mwisho ya kamepni ambayo ni Mei 23 mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2009

    Sasa tunasubiri helikopta ya CCM! Kaazi kwelikweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2009

    yaani CUF na CHADEMA wangekubaliana kuweka mgombea mmoja mbana ligi ingekuwa imeisha zamaani!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2009

    acha ushabiki watu wanakimbilia chadema sio pipa hapo geita kuna mapipa ya mkabulu ya kwenda na kurudi kwa madiba kila siku.

    chadema ushindi upo mikononi halaf nasikia kesi za mafisadi zimefutwa,michu unabana....

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2009

    Tanzania tunaelekea wapi...watu wanaona helikopta basi imekua dili...hivi hata hawa waandishi wa habari wanaweka kichwa kikubwa cha habari kuhusu helikopta, badala ya kuongelea sera na mabadiliko gani hivi vyama vitayaleta iwapo wakiteuliwa wao wanaongelea helikopta. Jamani sisi bado kabisaaaaa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2009

    RA anawalipia helikopta hao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2009

    michuzi nafuu urudi bongo. Yaani siku nzima picha moja utafikiri mtandao siyo richabo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2009

    Ngojeni na sie atuletee ya Obama,ambayo wabeba mabokisi hamtaki kutugaia

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2009

    Helicopter ni CEREMONIAL, what matters most ni kama wananchi wamejiandikisha kwa wingi na watakipigia kura chama gani. Jamani tusihadaliwe na mass inayohudhuria ktk mkutano, kuna uwezekano kwamba 50% ya watu walihudhuria hawakujiandikisha na hivyo hawatapiga Kura.
    Mkereketwa wa Ckama Cha xxxxxxx

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...