Michuzi Mkuu!
Ajali nyingine bwana hata hazielezeki. Jamaa chwaaa....! kaacha barabara kubwa ya main rodi, kavuka msingi wa bustani ya garden ya ofisi fulani hv huko maneo ya barabara ya Haileselasi rd, Masaki, kaingia kwenye banda la Mlinzi, ngwaaaaa!!Dereva bahati hakuuumia saaaana, na mlinzi aliekuwa akibadili nguo ndani ya kibdanda chake, aliacha zoezi hilo na kutoka nduki akidhani ni mabomu ya mbagala


Regards

Mdau
$Bonge$

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2009

    adu 'mwendesha gari' alikuwa anajifunza udereva ndo akakosea na unajua tena ukishakosea kidogo na ukawa na mapaniki ya ajabu ajabu, ukiambiwa piga breki unakolezea accelerator?
    Ila uliyeweka hii habari umenichekesha kweli, eti akatoka nduki akidhani mabomu ya Mbagala.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2009

    Hahaha, Asante sana kwa taarifa, umenivunja mbavu sana huo uandishi na jinsi ya kuripoti...! hahahahhaha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2009

    Bonge jifunze kuandika unaripoti kama vile ni story ya kuchekesha wakati hiyo ni ajali mwanadamu huwezi ikimbia, nadhani ulikuwa na kihoro cha kuhadithia ndo maana umesema bustani ya garden....sijapenda ulivyowasilisha nafsi ikusute kwa hili

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2009

    hahahahaaaa uwiii umeniacha hoi kwakweli

    asante kuburudisha akili yangu mana apa nna stress za kufa mtu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2009

    heheheh habari hii inachekesha ingawaje ni ya kusikitisha!!cha ajabu zadi barabara ya hailleselase road!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2009

    Haya sasa naona tuna mgeni mwingine hapa Anony wa 42:00 karibu sana kwenye blog yetu ya society ya jamii.Bustani za garden,barabara za road na mengineyo ndo libeneke lenyewe hilo hapa kijijini.Wakongwe wote wanajua hilo.pole sana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2009

    Tarehe Mon Jul 13, 05:42:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Huyu ni mwandishi wa habari anaripoti ilivyokuwa na ni juu ya msomajo kutafsiri mwenyewe. Mbona hivyo kushambuliana kila wakati.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 13, 2009

    moja kwa moja mlinzi afukuzwe kazi kwa nini aache lindo?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 13, 2009

    Du Bonge hii nimeikubali ile wacha...maana sinambavu wala kongosho...

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2009

    Hahahahahahaah! KWI KWI KWI KWI aliyendika kanifurahisha sana. Tunashukuru mungu wametoka salama wote ndio muhimu. ila sijui kaweka chumvi au hahahahaha. MZ.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2009

    Hivi bongo kuna sheria ya kuzuia walevi kuendesha gari au kuwafutia leseni? Things need to change in Africa ama sivyo tutamalizana barabarani. Kila siku ni ajali za kizembe zinatokea bila sababu. My Lord!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2009

    Kwani hamjui baba yake huyo dereva ni kiongozi mkubwa na ¨hata sijui kwanini ninamuita dereva kwani hata leseni hana tena hapo inasemekana mwenye makosa ni huyo mlinzi aliyekimbia mwendeshaji hana hatia... bongo hiyoo..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2009

    Jamaa alipiga honi weee,mlinzi kalala fofofo,akaona isiwe tabu ngoja niingie tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...