Ajali nyingine bwana hata hazielezeki. Jamaa chwaaa....! kaacha barabara kubwa ya main rodi, kavuka msingi wa bustani ya garden ya ofisi fulani hv huko maneo ya barabara ya Haileselasi rd, Masaki, kaingia kwenye banda la Mlinzi, ngwaaaaa!!Dereva bahati hakuuumia saaaana, na mlinzi aliekuwa akibadili nguo ndani ya kibdanda chake, aliacha zoezi hilo na kutoka nduki akidhani ni mabomu ya mbagala
Regards
Mdau
$Bonge$
Regards
Mdau
$Bonge$
adu 'mwendesha gari' alikuwa anajifunza udereva ndo akakosea na unajua tena ukishakosea kidogo na ukawa na mapaniki ya ajabu ajabu, ukiambiwa piga breki unakolezea accelerator?
ReplyDeleteIla uliyeweka hii habari umenichekesha kweli, eti akatoka nduki akidhani mabomu ya Mbagala.
Hahaha, Asante sana kwa taarifa, umenivunja mbavu sana huo uandishi na jinsi ya kuripoti...! hahahahhaha
ReplyDeleteBonge jifunze kuandika unaripoti kama vile ni story ya kuchekesha wakati hiyo ni ajali mwanadamu huwezi ikimbia, nadhani ulikuwa na kihoro cha kuhadithia ndo maana umesema bustani ya garden....sijapenda ulivyowasilisha nafsi ikusute kwa hili
ReplyDeletehahahahaaaa uwiii umeniacha hoi kwakweli
ReplyDeleteasante kuburudisha akili yangu mana apa nna stress za kufa mtu
heheheh habari hii inachekesha ingawaje ni ya kusikitisha!!cha ajabu zadi barabara ya hailleselase road!!
ReplyDeleteHaya sasa naona tuna mgeni mwingine hapa Anony wa 42:00 karibu sana kwenye blog yetu ya society ya jamii.Bustani za garden,barabara za road na mengineyo ndo libeneke lenyewe hilo hapa kijijini.Wakongwe wote wanajua hilo.pole sana.
ReplyDeleteTarehe Mon Jul 13, 05:42:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteHuyu ni mwandishi wa habari anaripoti ilivyokuwa na ni juu ya msomajo kutafsiri mwenyewe. Mbona hivyo kushambuliana kila wakati.
moja kwa moja mlinzi afukuzwe kazi kwa nini aache lindo?
ReplyDeleteDu Bonge hii nimeikubali ile wacha...maana sinambavu wala kongosho...
ReplyDeleteHahahahahahaah! KWI KWI KWI KWI aliyendika kanifurahisha sana. Tunashukuru mungu wametoka salama wote ndio muhimu. ila sijui kaweka chumvi au hahahahaha. MZ.
ReplyDeleteHivi bongo kuna sheria ya kuzuia walevi kuendesha gari au kuwafutia leseni? Things need to change in Africa ama sivyo tutamalizana barabarani. Kila siku ni ajali za kizembe zinatokea bila sababu. My Lord!
ReplyDeleteKwani hamjui baba yake huyo dereva ni kiongozi mkubwa na ¨hata sijui kwanini ninamuita dereva kwani hata leseni hana tena hapo inasemekana mwenye makosa ni huyo mlinzi aliyekimbia mwendeshaji hana hatia... bongo hiyoo..
ReplyDeleteJamaa alipiga honi weee,mlinzi kalala fofofo,akaona isiwe tabu ngoja niingie tu!
ReplyDelete