Picha ya pamoja ya waandaaji na wadhamini wa redds miss ilala 2009.
Taarifa ni kwamba Globu ya Jamii ni moja ya wadhamini wa shindano hili linalosubiriwa kwa hamu, ambapo kati ya warembo 17 walio kambini mmoja atachaguliwa na jopo la wapiga picha waandamizi wakisaidiwa na wadau kuwa Miss Photogenic ama miss mwenye mvuto wa picha.
Zawadi nono inaandaliwa na Globu ya Jamii kwa Miss Photogenic wa Redds Miss Ilala 2009 ambapo tovuti maalumu imeandaliwa ili kuwezesha wadau wasaidie kumchagua miss mwenye mvuto wa picha.
Taarifa kamili na namna ya kusidia kumchagua MichuziBlog Miss Photogenic zitatolewa kesho. Hivyo wadau kaeni tayari tayari.
-------------------------------------------------------------------------------
Redds Miss Ilala 2009 yapanga mikakati kutwa Taji la Miss TZ, kuzuru Ngorongoro kesho

Wakati huo huo, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Redds Miss Ilala 2009 Jackson Kalikumtima amesema wana mikakati mbalimbali iliyopangwa ili kuhakikisha kanda hiyo inatoa Vodaco Miss Tanzania 2009.

Shindano la Redds Miss Ilala linatarajiwa kufanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijjini Dar. Kabla ya kufanyika kwa shindano hilo warembo watakuwa na ziara ya kutembelea mbuga za Ngorongoro mkoani arusha kuazia kesho Julai 22 mpaka 26 na watakaporudi watashiriki kwenye onyesho la vipaji litakalofanyika Lamada Hotel Julai 28.

Warembo wanaoshiriki kwenye shindano hilo ni Fatma Bongi, Everline Gamasa, Julieth Lugembe, Magreth Motau, Lilian Nyamizi Mihayo, Irene Karugaba, Neema Doreen Kasunga, Winnfrida Mmari na Husna Ahmed.

Wengine ni Doris Luis, Groly Mwandani, Pendo Lema, Anne Mkandawile, Khadija Mhecha, Sylivia Shally, Gladness Shao na Zena Mbasha pamoja na mwalimu wao Regina Joseph na matron Nelly Kamwelu aliyekuwa Miss Ilala namba mbili mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    http://missilala.com/gallery.php

    Nataka ku vote for Gladys Shao lakini wame weka picha yake nakusema yeye ni Doris. Na sikujua kwamba tulikuwa na ma miss mwaka 1988. Jamani wa fix web site ili watu tu vote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...