Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi SACCOS ya Nyalikungu,mjini Maswa,mkoani Shinyanga jana mchana.Pembeni kulia ni Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Sospeter Jaffari.Wakati wa hafla hiyo Mama kikwete alitoa jumla ya Shilingi milioni tatu na nusu kwa SACCOS ZaNyalikungu.Maswa Teachers SACCOS na Malampaka SACCOS.


Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maandamano ya kulaani vitendo vya mimba dhidi ya wanafunzi yaliyofanyika katika uwanja wa michjezo wa Nguzonane wilayani Maswa,Mkoani Shinyanga jana mchana

Baadhi ya wanafunzi wakazi wa mji wa Maswa wakiwa na bago yenye ujumbe dhidi ya Gonjwa la ukimwi na mimba kwa wanafunzi muda mfupi baada ya kushiriki maandamano kulaani vitendo vya baadhi ya watu wazima kuwapa ujauzito wananfunzi na kuwaambukiza virusi vya ukimwi yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Nguzonane mjini Maswa jana mchana.Baadaye Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliwahutubia wakazi hao akikemea vikali tatizo la mimba mashuleni na kuzorota kwa elimu wilayani humo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    sasa kama hao watoto ni wanafunzi wakipinga wanafunzi kupewa mimba na vijeba, kwa nini wamevalishwa hayo mashati ya kijani.
    Nchi hii bado ina watu wanaoamini zaidi katika dhana ya vyama kuliko utaifa, wanadhani ukivaa kijani ndio uTanzania wako unakuwa bora. Achane kuchafua fikra za vijana wasijerithi UFISADI unaowanyima fursa za kuishi na kusoma katika shule bora kwa kuwa haki hizo zimeporwa na manyang'au.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    U-chama hautaleta maendeleo. Rais akichaguliwa anakuwa rais wa Watz wote, sio wanachama wa chama chake tu. Hata huu mfumo wa rais kuwa mwenyekiti wa chama haufai. Hiki ni kitu ambacho tunapaswa kuiga kwa "wenzetu". Rais awe rais, kiongozi wa chama awe kiongozi wa chama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...