Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).
Baadhi ya wananchi wakijitokeza kuangalia maonesho ya wiki ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutimiza miaka 45 wakipata maelezo kuhusu silaha za kivita kutoka kwa wataalam wa Jeshi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange


Wananchi wakijitokeza katika mabanda ya huduma za tiba kwenye maonyesho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kutimiza miaka 45
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya JWTZ kutimiza miaka 45 wakipata huduma za tiba na ushauri leo katika mabanda ya Maonyesho katika viwanja vya kikosi cha 603 cha Jeshi la wananchi Air wing,Ukonga jijini Dar es salaam.




Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi (kushoto kwa afande Mwamunyange) wakipata maelezo mara baada ya ufunguzi wa maonesho na maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar
Askari wa kikosi cha anga katika maonesho hayo
Wanafunzi wakiangalia baadhi ya silaha katika maonesho hayo
Askari wenye silaha za kutungua ndege katika maonesho
Wananchi wakiangalia vifaa vya kijeshi kwenye maonesho hayo
Picha zote na Aron Msigwa wa Maelezo









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. JESHI GANI HILI LISILOWEZA KULINDA WATANZANIA WANAOIBIWA NG'OMBE NA WAKENYA?

    UPUUZI MTUPU, SASA HILI JESHI LIKO KWA FAIDA YA NANI IWAPO HALIWEZI KULINDA MIPAKA YETU?

    WATANZANIA UPOLE WETU UNATUUMIZA, HAKUNA SABABY YA MANYANG'AU KUIBA NG'OMBE WA WATU WETU MASKINI.

    KAMA HILI JESHI HALIWEZI KUWATETEA, BASI HAKUNA HATA HAJA YA KUFANYA SHEREHE.

    ReplyDelete
  2. michuzi mimi naomba kuuliza hivi kiutendaji nani mkubwa kati ya Masilingi na Mwinyi? mimi naona Mwinyi ndo alistahili kua mgeni rasmi yeye akiwa kama waziri wa wizara husika. ni hayo tu mhesimiwa mkuu wa wilaya.

    ReplyDelete
  3. SASA WALE ASKARI WA KIKOSI CHA KUTUNGUA NDEGE, NAWAONA WAMEBEBA YALE MA-ROCKET INAMAANA WATABEBA HIVYO BEGANI SIKU NZIMA AU NDIO BEGA 1 LIKUMA ANAHAMISHIA JINGINE NA AKICHOKA KABISA WANAPEANA ZAMU YA KULINYANYUA MPAKA MDA WA MAONESHO UISHE.... teh teh teh tehehehe....kweli hii ni TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO...

    ReplyDelete
  4. Nalipongeza jeshi letu kwa kutimiza miaka 45 ya kuanzishwa kwake. majukumu mengi limetekeleza na hasa zile vita vya kusini mwa afrika.katika kuikomboa msumbiji,zimbabwe, namibia, angora na nyinginezo. pia kuhakikisha utawala mbovu wa makaburu kule afrika ya kusini unakoma.
    Ila nalisihi jeshi kuacha kuingilia mambo ya ndani, kama majuzi katika kituo kimoja cha televisheni tumeoneshwa wanajeshi wakishiliki kupambana na wananchi wakati wa uandikishaji wa daftari la kudumu kule zanzibar. nafikili hiyo si kazi ya jeshi hata kidogo nikuingilia mambo yasiyo wahusu.
    Pia tabia ya kupiga wananchi hovyo bila sababu nayo muikomeshe kabisa.

    ReplyDelete
  5. kiswahili bwana....!! sio maonesho ni maonyesho, wakishiliki wakishiriki, nafikili nafikiri, hovyo ovyo, angora angola mie naona ni poa siku nyingine ikawa mada ya neno moja linalokosewa sana wadau tukalichangiakutoa usahihi wake kwa vile hii ni blog ya jamii tunataka kiswahili safi kama kiinglish is not richabo na lugha ya taifa pia???
    mtanzania, north america

    ReplyDelete
  6. mdau wa kigomaAugust 27, 2009

    huyo anony anaesema sio maonesho ni maonyesho kajifunza wapi kiswahili? nakumbuka nikiwa form two , mwalimua wangu wa KISWAHILI alinifundisha kwamba, KUONYESHA kunatokana na neno KUONYA.Ukilinyumbua ndio utapata neno KUONYESHA,MAONYESHO,NK. ila MAONESHO yanatokana na kuona(ONA), ukilinyumbua ndio utapata ONESHA,MAONESHO, NK. HIVYO BASI MAONESHO NI NENO SAHIHI KABISA.

    ReplyDelete
  7. Mdau wewe ndio hujui kiswahili ni maonesho na sio MAONYESHO! Ukinyumbulisha neno maonyesho utakutana na neno kuonya! na ukinyumbulisha neno kuonesha utapata neno kuona! Upo hapo mdau?

    ReplyDelete
  8. Anon wa Aug 27,12:07:00 PM, kwa kukataa neno MAONESHO kuwa siyo sahihi naona nawe unachemsha. Hicho ndicho kiswahili fasaha.

    Pengine kosa ambalo naliona na ambalo wengi wetu tunalifanya ni kumtaja Generali Mwamnyange kama Mkuu wa Majeshi.Hii siyo sahihi. Ukweli yeye ni Mkuu wa Majeshi ya ULINZI.(CHIEF OF DEFENCE FORCES).Polisi na Magereza nayo ni majeshi. Sasa mtu akisema Mkuu wa Majeshi ina maana yeye ni Mkuu wa Polisi na Magereza pia. Nawakilisha.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  9. Kaka michuzi, nalipongeza jeshi letu kwa kutimiza umri wa miaka 45 likiwa na kiongozi msomi na wasomi kadhaa ndani ya jeshi hilo.Kwa maoni aliyoyatoa mdau wa hapo juu inatujulisha wazi ni kijana mdogo aliyezaliwa bila shaka baada ya awamu ya pili. Na ndio gharama ya vijana ambao hawakufundwa katika jeshi la kujenga taifa, na ndio maana anakuwa na maoni" wazi yasiyo na tija". Kazi ya jeshi sii kukomboa mifugo inayoibiwa na wahalifu wachache wa nchi jirani. Kufanya hivyo ni sawa na baba mzimaaa kuingilia ugomvi wa watoto wadogo marafiki walio chini ya umri wa miaka 5.Matokeo yake dakika chache wanaendelea kuwa marafiki. Ni wapi utauficha uso wako?? Zipo shughuli wanazoweza kuzifanya ambazo mdau wala hatopata taarifa kwamba zimefanyika. yeye aendelee kuishi na kuvuta hewa kwa amani huku akiamini kwamba uwezo wake wa kifikiria hauna ukomo. Hongeta TPDF

    ReplyDelete
  10. It is easy to become a soldier when there is no War

    ReplyDelete
  11. mbavu zangu hahahahaaaa annons 4.44pm,10.06am,3.02am

    jamani watu mna visa?

    ila kusema ukweli dah jamaa mkuu wa majeshi MWAMUNYANGE...unanimaliza kabisaaa yani nimekufa nimeoza kwako,ivi inaruhusiwa siku japo nisogee nikupe mkono?au nikuwawooo?

    basi tu sina la kusema,serious tena ukipiga ilo jezi ndo nalowaaaa

    ReplyDelete
  12. safi sana Afande Bahati kwa kuwakilisha TATC-Nyumbu,hongera JWTZ kwa miaka 45.

    ReplyDelete
  13. Kuna Mdau Kanigusa Kuwaambia Waache Kutogonga Hawa Wajesh Uswazi Namuunga Mkono Sana Na Pia Wasituvue Vtshirt Vyetu Vya Mtumba Kisa Vinamabaka mabaka

    ReplyDelete
  14. Wadau nauliza hivi hao askari wanaovaa kofia nyekundu ni wa vikosi gani? Maana ukiona blue basi ni anga, kijani ni wa miguu na nyeupe ni wa maji. Sasa hao nyekundu ni wa kikosi gani? Anayejua basi hatufahamishe. Salaam

    ReplyDelete
  15. Anon wa Thu Aug 27, 10:28:00 PM, kama sijakosea wanaovaa kofia nyekundu ni makomandoo wa JWTZ

    ReplyDelete
  16. Bongo kweli tambarare, mtu anafanyiwa procedure ya kung'olewa meno mbele ya kadamnasi yoote hiyo? Hapo ni anasaidiwa kung'olewa jino ama anazidishiwa magonjwa kwa kuongezewa ma-bacteria kwenye icho kidonda kinachochimbuliwa kwenye magego? Oh My god!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...