Mama Maria Nyerere ametembelea Ubalozi wa Tanzania London leo, Ijumaa tarehe 18 Septemba 2009 akiwa safarini kutoka New York alikokabidhiwa nishani ya Umoja wa Mataifa ya Ushujaa wa Kutetea Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice) kwa niaba ya Mwalimu Julius K. Nyerere.

Akiwa Ubalozini hapo, Mama Maria alipata fursa ya kuzungumza na maafisa wa Ubalozi huku akiwaonyesha nishani hiyo na cheti kikubwa (pichani juu) alivyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Aidha Mama Maria aliweka saini kwenye kitabu cha wageni na kupiga picha za kumbukumbu na maafisa.

Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akionyesha Nishani ya Umoja wa Taifa aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Mwalimu Julius K. Nyerere, alipotembelea Ofice za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Kutoka kulia mwa picha ni Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi Sinare Maajar na Kushoto mwa Picha ni Mkuu wa Utawala Ubalozini hapo, Dada Caroline Chipeta.
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania- Uingereza, Mama Mwanaidi Sinare Maajar, Mama Maria Nyerere na Mheshimiwa Makamu wa Balozi, Bwana Chabaka F. Kilumanga.
Mheshimiwa Balozi akiwa na Mama Maria Nyerere
wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa wengine wa Ubalozini hapo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. MAMA MARIA NYERERE NIMEFURAHI SANA KUKUONA HAPO UK.
    naomba uwaambie hao maofisa wafanye kazi kwa moyo mmoja walifanyie taifa sio wajifanyie wao tu wajitume kama mwalimu nyerere alivyojituma.
    SI UNAJUWA KALE KATABIA KA UFISADI WATANZANIA WENGI HIVI SASA WAMEKAPENDA. ni hayo tu michuzi kama ulifunga usinibanie

    ReplyDelete
  2. KUNGURU!!!!MAMA MARIA ANAMIAKA MINGAPI?KWANI ANAONEKANA YUPO BOMBA NA NGUVU ZAKE,KUNA ANAEJUWA UMRI WAKE?

    ReplyDelete
  3. I wish ungetembelea ubalozi wetu wa hapa DC uwapechangamoto. Labda wangefanya kazi kwa kuwajibika badala ya kumweka mtu kwenye hold nusu saa, na mwishowe uambiwe ahhh....yupo kwenye mkutano jaribu tena baadaye.

    ReplyDelete
  4. So in every country that we represent we have about 10 workers.

    ReplyDelete
  5. Jamaa marafiki, tumechoka na mtu moja hapa ubalozi afisa wa uwamiaji(uk) kwa jina ni mr, AMBUKILE anatunyanyasa sana watanzania tunaomba aondolewe pls please.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...