Mama Maria Nyerere ametembelea Ubalozi wa Tanzania London leo, Ijumaa tarehe 18 Septemba 2009 akiwa safarini kutoka New York alikokabidhiwa nishani ya Umoja wa Mataifa ya Ushujaa wa Kutetea Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice) kwa niaba ya Mwalimu Julius K. Nyerere.Akiwa Ubalozini hapo, Mama Maria alipata fursa ya kuzungumza na maafisa wa Ubalozi huku akiwaonyesha nishani hiyo na cheti kikubwa (pichani juu) alivyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Aidha Mama Maria aliweka saini kwenye kitabu cha wageni na kupiga picha za kumbukumbu na maafisa.
Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akionyesha Nishani ya Umoja wa Taifa aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Mwalimu Julius K. Nyerere, alipotembelea Ofice za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Kutoka kulia mwa picha ni Mheshimiwa Balozi, Mama Mwanaidi Sinare Maajar na Kushoto mwa Picha ni Mkuu wa Utawala Ubalozini hapo, Dada Caroline Chipeta.
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania- Uingereza, Mama Mwanaidi Sinare Maajar, Mama Maria Nyerere na Mheshimiwa Makamu wa Balozi, Bwana Chabaka F. Kilumanga. wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa wengine wa Ubalozini hapo.



MAMA MARIA NYERERE NIMEFURAHI SANA KUKUONA HAPO UK.
ReplyDeletenaomba uwaambie hao maofisa wafanye kazi kwa moyo mmoja walifanyie taifa sio wajifanyie wao tu wajitume kama mwalimu nyerere alivyojituma.
SI UNAJUWA KALE KATABIA KA UFISADI WATANZANIA WENGI HIVI SASA WAMEKAPENDA. ni hayo tu michuzi kama ulifunga usinibanie
KUNGURU!!!!MAMA MARIA ANAMIAKA MINGAPI?KWANI ANAONEKANA YUPO BOMBA NA NGUVU ZAKE,KUNA ANAEJUWA UMRI WAKE?
ReplyDeleteI wish ungetembelea ubalozi wetu wa hapa DC uwapechangamoto. Labda wangefanya kazi kwa kuwajibika badala ya kumweka mtu kwenye hold nusu saa, na mwishowe uambiwe ahhh....yupo kwenye mkutano jaribu tena baadaye.
ReplyDeleteSo in every country that we represent we have about 10 workers.
ReplyDeleteJamaa marafiki, tumechoka na mtu moja hapa ubalozi afisa wa uwamiaji(uk) kwa jina ni mr, AMBUKILE anatunyanyasa sana watanzania tunaomba aondolewe pls please.
ReplyDelete