SWALI: Nini kipya kipya kuhusu K-Lynn?

KYLIN: Kipya kuhusu K-Lynn ni kwamba kwa sasa nasoma kwa njia ya posta kupitia chuo kimoja kilichopo Uingereza ili niwe mbunifu wa mapambo ya ndani, pili nimekuwa niko studio kwa mwaka mzima nikitengeneza nyimbo mpya ambazo natumai nitaziachia kabla ya mwisho wa mwaka huu, pia nimeanzisha kampuni yangu ya masuala ya mapambo ya ndani ambayo inashughulika kila kitu kinachohusiana na kupendezesha ndani, ambapo nashirikiana na wataalam wengine wa fani hiyo hivyo nina mambo mengi mapya.

SWALI: Jamii inakutazamaa vipi, kutokana na umaarufu wako?

KYLIN: Umaarufu ni sawa siwezi kulalamika, nashukuru naishi katika nchi ambayo celebrity anaachiwa uhuru binafsi tofauti na nchi kama vile Marekani ambako kila kitu kuhusu maisha ya celebrity kinaandikwa kwenye magazeti ya udaku. Hivyo naweza kusema niko poa. Napenda kukutana na mashabiki wangu ambao wanapenda kazi zangu na wanakuwa motisha kwangu.
Kwa hayo na mengi mengineyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. MICHUZI KWA NINI USIKAMATE HIKI KIFAA TUNAJUA HUNA MKE NA YEYE HANA MUME?

    ReplyDelete
  2. Very Beautiful

    ReplyDelete
  3. Michuzi hana mke
    Hicho ni kitendawili
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. Nina swali nauliza hivi dada zako wako wapi wakina Jessie na Shimmi? Niliwaona wakiwa wadogo sana we ulikuwa hujazaliwa.

    ReplyDelete
  5. michuzi ana mke tena dogodogo, toto la kichaga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...