Waziri wa Maji na Umwagiliaji azindua mkutano wa Utekelezaji wa programu ya maji vijijijini
Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya amesema lengo la kitaifa kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ni asilimia 65 ifikapo mwaka 2010.
Amesema hilo ni lengo la Milenia ,lengo namba saba ambalo ni lengo la kidunia kwamba ifikapo mwaka 2015 idadi iwe imepungua kwa nusu.
Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof.Mark J.Mwandosya amesema hayo katika Mkutano wa siku mbili wa mwaka wa utekelezaji wa programu ya maji vijijini unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Desemba 14 na 15, 2009 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha AICC jijini Arusha.
Pia ameongeza kuwa tafsiri ya kitaifa ya lengo la milenia ni asilimia 74 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwaka 2015, na kwamba lengo kuu ni kwamba ifikapo mwaka 2020 kila mtanzania awe anaweza kupata maji safi katika umbali usiozidi mita 400 na iwe ni haki kwa Mtanzania kupata angalau lita 25 za maji kwa siku.
Amesema hadi kufikia mwaka 2008 asilimia 58.3 ya wananchi waishio vijijini waliweza kufikiwa na huduma ya maji na kuongeza kuwa juhudi za serikali katika kuyafikia malengo hayo zinafanyika katika utekelezaji wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji.
Home
Unlabelled
profesa mwandosya afungua mkutano wa maji vijijini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


kaka michuzi tafadhali tupe habari kuhusu maziwa feki ya watoto yaliyokamatwa na tfda jamani mbona hawa wachina watuua
ReplyDeletehongera prof mwandosya uko juu..
ReplyDeletehuyu waziri ilibidi awepo kule copen lakini nani anawakilisha mambo ya mabadiliko ya hewa nchi?
ReplyDeleteau maji hayahusiki na climate change?
kweli bado tupo kizani si ajabu ukakuta waziri wa miundo mbinu na jeshi ndhio kaenda copenhagen
porojo tu miaka nenda rudi tuna shughulikia maji vijijini
ReplyDeletetanzania ndo nchi yenye vyanzo vingi vya maji na vya kudumu kuliko nchi yoyote ile duniani
kama lake victoria,nyansa,tanganyika na mito lukuki.
angalieni ramani mjionee.
lakini maji ni tatizo, je tungeishi jangwani ingekuwaje?
Mwandosya for president or Vice President? what is your next move? I don't understand what is going on for this PR stunt!?
ReplyDeleteLets wait and see.
mwakani huu mkutano ufanyike kwenye kijiji tena kile chenye shida ya maji
ReplyDeleteannon bennet umesema sawa...
ReplyDeleteper diems izo
Nani mwakilishi wa wananchi kwenye mkutano huu?
ReplyDelete