Matango toka shambani hapo
Nauza shamba langu lenye ekari 18. Liko maeneo ya Vianzi, Mkuranga. Takriban km 30 toka makao makuu ya Bp kurasini. Lina bwawa la samaki (lahitaji ukarabati), Msingi wa nyumba ya wafanyakazi, mto wenye maji ya kutosha kumwagilia mwaka mzima.
*Kuna bwawa la samaki (20mt X 30mt) linalohitaji ukarabati kwa ajili ya ufugaji wa Sato.
*Msingi wa nyumba ya wafanyakazi.
*Kuna mto kwa ajili ya umwagiliaji maji mwaka mzima.
*Mazao yanayofaa, migomba, passion, matikiti, matango, nyanya, hoho, pilipili mbuzi, biringanya,nk.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba
*Kuna bwawa la samaki (20mt X 30mt) linalohitaji ukarabati kwa ajili ya ufugaji wa Sato.
*Msingi wa nyumba ya wafanyakazi.
*Kuna mto kwa ajili ya umwagiliaji maji mwaka mzima.
*Mazao yanayofaa, migomba, passion, matikiti, matango, nyanya, hoho, pilipili mbuzi, biringanya,nk.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba
mbona hujatwambia unataka dola laki ngapi?
ReplyDeletehilo shamba linaonekana linalipa mdau sema bei,hapo ni kama nimefika hapo mkuranga na kuliona
ReplyDeleteWeka at least unahitaji shilling ngapi kwanza kabla hatujanyanyua simu. halafu ni heka 15 au 18? Biashara matangazo lakini bongo tumeshindwa kutangaza.....
ReplyDeleteUnaliuza kwa shilingi ngani? Na kwanini unataka kuliuza?
ReplyDeletemaswali yote apo juu kwa annons ndo nayauliza ata mimi...
ReplyDelete1.bei
2.sababu ya kuliuza
3.ekari ngapi 15/18?
4.bwawa la samaki me silioni apo naona manyasi na kama kidimbwi/bonde tu
5.mto unaitweje apo karibu na shamba lako unaposema unapita,na je mafuriko ya el-nino yaweje?
ni ayo tu,jieleze
we muuza shamba hebu uza kama mtu ulieenda shule sio unauza kisanii kama miaka ya 1980s weka bei kamili na kama kuna maelewano sema maana kuficha bei means hujui au huna uhakika na unachokiuza na weka all legal details down
ReplyDeletetahnx
Ni kweli kabisa bei ni muhimu kujua kabla hatujaongea,naunga mkono wote waliotangulia
ReplyDelete