Matango toka shambani hapo
Nauza shamba langu lenye ekari 18. Liko maeneo ya Vianzi, Mkuranga. Takriban km 30 toka makao makuu ya Bp kurasini. Lina bwawa la samaki (lahitaji ukarabati), Msingi wa nyumba ya wafanyakazi, mto wenye maji ya kutosha kumwagilia mwaka mzima.

*Kuna bwawa la samaki (20mt X 30mt) linalohitaji ukarabati kwa ajili ya ufugaji wa Sato.

*Msingi wa nyumba ya wafanyakazi.

*Kuna mto kwa ajili ya umwagiliaji maji mwaka mzima.

*Mazao yanayofaa, migomba, passion, matikiti, matango, nyanya, hoho, pilipili mbuzi, biringanya,nk.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba
0767775152
Juu na chini ni sehemu ya hizo ekari 15 la shamba

Nyanya chungu zinamea kwa wingi shambani hapo
Sehemu yenye mazao shambani hapo
Bwawa la samaki






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. mbona hujatwambia unataka dola laki ngapi?

    ReplyDelete
  2. hilo shamba linaonekana linalipa mdau sema bei,hapo ni kama nimefika hapo mkuranga na kuliona

    ReplyDelete
  3. Weka at least unahitaji shilling ngapi kwanza kabla hatujanyanyua simu. halafu ni heka 15 au 18? Biashara matangazo lakini bongo tumeshindwa kutangaza.....

    ReplyDelete
  4. Unaliuza kwa shilingi ngani? Na kwanini unataka kuliuza?

    ReplyDelete
  5. maswali yote apo juu kwa annons ndo nayauliza ata mimi...
    1.bei
    2.sababu ya kuliuza
    3.ekari ngapi 15/18?
    4.bwawa la samaki me silioni apo naona manyasi na kama kidimbwi/bonde tu
    5.mto unaitweje apo karibu na shamba lako unaposema unapita,na je mafuriko ya el-nino yaweje?

    ni ayo tu,jieleze

    ReplyDelete
  6. we muuza shamba hebu uza kama mtu ulieenda shule sio unauza kisanii kama miaka ya 1980s weka bei kamili na kama kuna maelewano sema maana kuficha bei means hujui au huna uhakika na unachokiuza na weka all legal details down
    tahnx

    ReplyDelete
  7. Ni kweli kabisa bei ni muhimu kujua kabla hatujaongea,naunga mkono wote waliotangulia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...