HABARI ZIMETUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.
MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.
BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.
BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU.
ALIWAHI PIA KUTEULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, MH. KOFFI ANNAN, KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU
AMIN
Duh! Mzee wetu ametutoka!!! Amelitumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa....Poleni wafiwa
ReplyDeletePoleni sana ndugu na jamaa na watanzania wote, huyo mzee alikuwa moja ya wasaidizi wa mwalimu, mwenye data zaidi atukumbushe
ReplyDeletemdau
Tunawapa pole wafiwa. Huyu mzee alikuwa very resourceful and a man of unquestionable integrity. I remember nikiwa mwanafunzi IDM Mzumbe 1974 alikuja pale kama Waziri wa Habari kuzungumzia juu ya Press Freedom. They shared the podium with the late Walter Rodney. Tuliokuwa wasikilizaji tuliridhika na mchango wake na jinsi alivyokuwa akijibu maswali tena mengi yakitoka kwa walimu wetu ambao nao walikuwa intellectuals wa hali ya juu kama akina Jacskon Makwetta akina George Hadjivayanis. Halafu nikiwa Afisa Mipango Wilaya ya Iringa Vijijini mwaka 1975 na yeye alikuja kugombea ubunge wa Iringa mjini, nikawa nafuatilia sana zile kampeni. Siku zile Chama cha TANU. Mgombea mwingine wa TANU alikua Hakimu mmoja akiitwa Sheikh Mbarazi. Siyo siri wananchi walikuwa wanaweza kupambanua vizuri tu kuwa Daudi Ngelautwa Mwakawago was a better candidate.
ReplyDeleteAidha wakati ule kama sikosei alikuwa pia Publicity Secretary wa TANU. Hiyo ilikuwa kabla CCM haijazaliwa.
Hatuwezi kulalamika wakati Mola anaamua kumchukua kiumbe chake. Kwa sababu kifo siyo balaa wala siyo laana, bali ni majaliwa yake Mola na kifo ni faradhi. Inna Lilahi wa Inna ilahi Rajiuun.
poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteKwa kweli ni msiba mkubwa.I have known the late Mwakawago for a long time. He was a leader to emulate, an oustanding civil servant. Tumepoteza mtu ambaye alituwakilisha vyema katika anga za kidiplomasia duniani kote. Raha ya Milele umpe Ee Bwana....na mwanga wa milele umwangazie.
ReplyDeleteDuh inasikitisha kuona wazee wetu wanaondoka tuliokuwa tunawategemea kwa mchango katika Taifa letu. Kazi ya mungu haina makosa. Poleni sana wafiwa mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mzee wetu.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa. Tupo pamoja nanyi kwa tukimuombea Hayati Mzee Mwakawago, katika kipindi hiki kigumu mlichonacho.
ReplyDeleteLakini nadhani nyingine ya historia ya Mzee Mwakawago haikutajwa hapa juu kuwa aliwahi kufanya kazi Radio Tanzania RTD katika nyadhifa mbali-mbali.
Alikuwa makini, mzalendo, mchapakazi na mwadilifu. Tunamuomba Muumba amuweke mahali pema peponi.
ReplyDeleteNamkumbuka kwani nilimfahamu tangu enzi za akina Nyerere miaka ya 1980's nikisoma primary.Sikuwahi kumuona ila nikisikia jina lake napata hisia za viongozi wa enzi za Mwalimu ambao waliishi sera za wakati huo kikweli.
ReplyDeleteNajua alikuwa balozi Marekani kwa muda mrefu.
Mungu amuweke mahali pema peponi. Nashukuru mh. Tsere ameeleza hasa jinsi alivyokuwa.Ongeza zaidi kwa faida ya vijana wa leo ambao hawana habari ya viongozi waliotukuka wa nchi h ii.
Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN. Nilimhoji mara kadhaa na kutafuta habari kwake nikiwa mwandishi wa habari Daily News. Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteAnon Feb 25, 02:27pm, mtu ana umri wa miaka 71 amestaafu baada ya kulitumikia taifa kwa uadilifu, halafu bado unawategemea katika mchango kwa Taifa letu mpaka lini?
ReplyDeleteHata wazazi kuna point inafika inabidi ukajitegemee you gotta move out ili wazee wafaidi life yao once more!
Unapostaafu especially ukishafikisha 70 angalau uwe na time for yourself playing golf na labda your spouse. Watoto wako ndio time yao ya kuchacharika wewe unatulia tuli.
Natumaini Mzee wetu alipata muda kama huo, pole sana kwa wafiwa, na tunamuombea Mungu ampumzishe pema peponi - Amen
Ni masikitiko makubwa sana tumepotelewa na mzee muadilifu. Hawa ndio wale wazee ambao walitoa kafara maisha yao kwaajili ya taifa la Tanzania.Hawakupatikana hata na doa lolote litakalomzuia asipewe nafasi ya kitaifa kuhudumia Taifa. Wazee kama hawa, laiti wangekuwa na uroho wa madaraka, kwakweli ndiyo hasa ambao tungewahitaji wangekuwa viongozi wa leo katika kipindi kibaya cha uroho wa pesa kama hiki.
ReplyDeleteTanzania tunahitaji watu kama hao. Wamekufa masikini wa mali, lakini wamekufa wakiwa matajiri wa Roho na uaminifu.Ndiyo historia aliyoiacha huyu mzee. Ndugu wa Tanzania, Nchi yetu ili iendelee kusonga mbele inabidi mioyo yetu ibadilike iwe kama ya hawa wazee wetu hawa.Watu waliojitolea maisha yao kuishi kama watu wa kawaida tu bila kujilimbikizia mali. Mzee kawawa, mzee mwakawago na mzee Nyerere mwenyewe, ni wa Tanzania ambao historia yao inabidi isimuliwe kwenye vitabu waisome dunia nzima.
Mzee mwakawago aliwahi kuwa Mkuu wa CHUO kikuu cha siasa cha kivukoni ezi hizo. mimi ninayeandika hii taarifa yaani rambi rambi zangu kwa wafiwa na wananchi wote, Baba yangu amesomeshwa na Mwakawago katika chuo hicho.Baba yangu ana degree ya siasa chuokikuu cha KIVUKONI Daresalaam, na baadaye Urusi. Alikuwa ananiambia Mwakawago wakati huo alikuwa kijana mdogo sana alipokuwa Mkuu wa chuo yaani baba akiwa kama mwanafunzi na Mwakawago ni Mkuu wa chuo walikuwa karibu rika moja japo wamepishana miaka mitano yaani ni age mate moja. Baba mdogo miaka mitano kwa Mwakawago. Aliwahi kuwa Katibu MTENDAJI wa TANU wa Taifa pia, alikuja Iringa mimi nikiwa kamanda wa gwaride la chipukizi alikagua gwaride Mkoa wa Iringa. Nimesahau siku hiyo ilikuwa ni ya nini sijuwi, bali ilikwa siku kubwa.Japo haikuzidi ile ya mwalimu Nyerere alipofanya Sherehe kubwa IRINGA ambayo haijawahi tokea mpaka leo tena.
Wafiwa, poleni sana ndugu zanguni tumefiwa mzee wetu wa taifa na family pia.
eeh jamani Tanzania kweli tunaondokewa na watu jamani.
Innalillahi Wainnailaihi Rajiuun,poleni sana wafiwa kazi ya Mungu haina makosa sote tutarejea kwake Allah kwa siku na wasaa aliotupangia mwenyewe Maulana,Lulu,Imani,poleni sana wadogo zetu Mwenyezi Mungu atawatia nguvu,uvumulivu na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu.Sisi tulimpenda mzazi wetu lakini Mungu amempenda zaidi,apumzike kwa amani Mzee wetu.
ReplyDeleteTerribly Saddened. He will be sorely missed by all of us who worked with and knew him. It is so disheartening to lose kind people like Amb. Mwakawago, who represented our country with Love and Dignity. His heart was open for everybody and welcomed everyone os us (NEW YORK) to our house without discrimination. What can we do as human beings but to pray. We all extend our heart felt condolonces to the family.
ReplyDeleteR.I.P Mzee Mwakawago.. Tagie, Kie, Imani na watoto wote wa marehem na familia kwa ujumla, poleni sana..
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ampumzishe Mzee Mwakawago mahala pema (InshaAllah). Poleni familia yake Mama na watoto wote Imani, Lulu, na wengine wote Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo. Amin!!
ReplyDeleteHe was like a father figure to me, mcheshi,mchekeshaji na mwenye upendo wa hali ya juu, R.I.P Babu,Bibi Mwakawago,Imani,Kie,Lulu n Tage kazi ya Mungu haina makosa may the Gods strength be upon u guys. We love you so much.
ReplyDeleteMoya ailaze mahala pema peponi roho ya Mzee Mwakawago. Tulikaa naye vizuri sana pale New York. Mungu awape nguvu mke,watoto na familia yote.
ReplyDelete