MAREHEMU DAUDI MWAKAWAGO

HABARI ZIMETUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.
MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.
BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.
BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU.
ALIWAHI PIA KUTEULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, MH. KOFFI ANNAN, KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.
MOLA AIWEKE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU
AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Duh! Mzee wetu ametutoka!!! Amelitumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu mkubwa....Poleni wafiwa

    ReplyDelete
  2. Poleni sana ndugu na jamaa na watanzania wote, huyo mzee alikuwa moja ya wasaidizi wa mwalimu, mwenye data zaidi atukumbushe

    mdau

    ReplyDelete
  3. Patrick TsereFebruary 25, 2010

    Tunawapa pole wafiwa. Huyu mzee alikuwa very resourceful and a man of unquestionable integrity. I remember nikiwa mwanafunzi IDM Mzumbe 1974 alikuja pale kama Waziri wa Habari kuzungumzia juu ya Press Freedom. They shared the podium with the late Walter Rodney. Tuliokuwa wasikilizaji tuliridhika na mchango wake na jinsi alivyokuwa akijibu maswali tena mengi yakitoka kwa walimu wetu ambao nao walikuwa intellectuals wa hali ya juu kama akina Jacskon Makwetta akina George Hadjivayanis. Halafu nikiwa Afisa Mipango Wilaya ya Iringa Vijijini mwaka 1975 na yeye alikuja kugombea ubunge wa Iringa mjini, nikawa nafuatilia sana zile kampeni. Siku zile Chama cha TANU. Mgombea mwingine wa TANU alikua Hakimu mmoja akiitwa Sheikh Mbarazi. Siyo siri wananchi walikuwa wanaweza kupambanua vizuri tu kuwa Daudi Ngelautwa Mwakawago was a better candidate.

    Aidha wakati ule kama sikosei alikuwa pia Publicity Secretary wa TANU. Hiyo ilikuwa kabla CCM haijazaliwa.

    Hatuwezi kulalamika wakati Mola anaamua kumchukua kiumbe chake. Kwa sababu kifo siyo balaa wala siyo laana, bali ni majaliwa yake Mola na kifo ni faradhi. Inna Lilahi wa Inna ilahi Rajiuun.

    ReplyDelete
  4. poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli ni msiba mkubwa.I have known the late Mwakawago for a long time. He was a leader to emulate, an oustanding civil servant. Tumepoteza mtu ambaye alituwakilisha vyema katika anga za kidiplomasia duniani kote. Raha ya Milele umpe Ee Bwana....na mwanga wa milele umwangazie.

    ReplyDelete
  6. Duh inasikitisha kuona wazee wetu wanaondoka tuliokuwa tunawategemea kwa mchango katika Taifa letu. Kazi ya mungu haina makosa. Poleni sana wafiwa mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mzee wetu.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wafiwa. Tupo pamoja nanyi kwa tukimuombea Hayati Mzee Mwakawago, katika kipindi hiki kigumu mlichonacho.

    Lakini nadhani nyingine ya historia ya Mzee Mwakawago haikutajwa hapa juu kuwa aliwahi kufanya kazi Radio Tanzania RTD katika nyadhifa mbali-mbali.

    ReplyDelete
  8. Alikuwa makini, mzalendo, mchapakazi na mwadilifu. Tunamuomba Muumba amuweke mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  9. Namkumbuka kwani nilimfahamu tangu enzi za akina Nyerere miaka ya 1980's nikisoma primary.Sikuwahi kumuona ila nikisikia jina lake napata hisia za viongozi wa enzi za Mwalimu ambao waliishi sera za wakati huo kikweli.
    Najua alikuwa balozi Marekani kwa muda mrefu.
    Mungu amuweke mahali pema peponi. Nashukuru mh. Tsere ameeleza hasa jinsi alivyokuwa.Ongeza zaidi kwa faida ya vijana wa leo ambao hawana habari ya viongozi waliotukuka wa nchi h ii.

    ReplyDelete
  10. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN. Nilimhoji mara kadhaa na kutafuta habari kwake nikiwa mwandishi wa habari Daily News. Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  11. Anon Feb 25, 02:27pm, mtu ana umri wa miaka 71 amestaafu baada ya kulitumikia taifa kwa uadilifu, halafu bado unawategemea katika mchango kwa Taifa letu mpaka lini?
    Hata wazazi kuna point inafika inabidi ukajitegemee you gotta move out ili wazee wafaidi life yao once more!
    Unapostaafu especially ukishafikisha 70 angalau uwe na time for yourself playing golf na labda your spouse. Watoto wako ndio time yao ya kuchacharika wewe unatulia tuli.
    Natumaini Mzee wetu alipata muda kama huo, pole sana kwa wafiwa, na tunamuombea Mungu ampumzishe pema peponi - Amen

    ReplyDelete
  12. Ni masikitiko makubwa sana tumepotelewa na mzee muadilifu. Hawa ndio wale wazee ambao walitoa kafara maisha yao kwaajili ya taifa la Tanzania.Hawakupatikana hata na doa lolote litakalomzuia asipewe nafasi ya kitaifa kuhudumia Taifa. Wazee kama hawa, laiti wangekuwa na uroho wa madaraka, kwakweli ndiyo hasa ambao tungewahitaji wangekuwa viongozi wa leo katika kipindi kibaya cha uroho wa pesa kama hiki.
    Tanzania tunahitaji watu kama hao. Wamekufa masikini wa mali, lakini wamekufa wakiwa matajiri wa Roho na uaminifu.Ndiyo historia aliyoiacha huyu mzee. Ndugu wa Tanzania, Nchi yetu ili iendelee kusonga mbele inabidi mioyo yetu ibadilike iwe kama ya hawa wazee wetu hawa.Watu waliojitolea maisha yao kuishi kama watu wa kawaida tu bila kujilimbikizia mali. Mzee kawawa, mzee mwakawago na mzee Nyerere mwenyewe, ni wa Tanzania ambao historia yao inabidi isimuliwe kwenye vitabu waisome dunia nzima.
    Mzee mwakawago aliwahi kuwa Mkuu wa CHUO kikuu cha siasa cha kivukoni ezi hizo. mimi ninayeandika hii taarifa yaani rambi rambi zangu kwa wafiwa na wananchi wote, Baba yangu amesomeshwa na Mwakawago katika chuo hicho.Baba yangu ana degree ya siasa chuokikuu cha KIVUKONI Daresalaam, na baadaye Urusi. Alikuwa ananiambia Mwakawago wakati huo alikuwa kijana mdogo sana alipokuwa Mkuu wa chuo yaani baba akiwa kama mwanafunzi na Mwakawago ni Mkuu wa chuo walikuwa karibu rika moja japo wamepishana miaka mitano yaani ni age mate moja. Baba mdogo miaka mitano kwa Mwakawago. Aliwahi kuwa Katibu MTENDAJI wa TANU wa Taifa pia, alikuja Iringa mimi nikiwa kamanda wa gwaride la chipukizi alikagua gwaride Mkoa wa Iringa. Nimesahau siku hiyo ilikuwa ni ya nini sijuwi, bali ilikwa siku kubwa.Japo haikuzidi ile ya mwalimu Nyerere alipofanya Sherehe kubwa IRINGA ambayo haijawahi tokea mpaka leo tena.
    Wafiwa, poleni sana ndugu zanguni tumefiwa mzee wetu wa taifa na family pia.
    eeh jamani Tanzania kweli tunaondokewa na watu jamani.

    ReplyDelete
  13. Innalillahi Wainnailaihi Rajiuun,poleni sana wafiwa kazi ya Mungu haina makosa sote tutarejea kwake Allah kwa siku na wasaa aliotupangia mwenyewe Maulana,Lulu,Imani,poleni sana wadogo zetu Mwenyezi Mungu atawatia nguvu,uvumulivu na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu.Sisi tulimpenda mzazi wetu lakini Mungu amempenda zaidi,apumzike kwa amani Mzee wetu.

    ReplyDelete
  14. Terribly Saddened. He will be sorely missed by all of us who worked with and knew him. It is so disheartening to lose kind people like Amb. Mwakawago, who represented our country with Love and Dignity. His heart was open for everybody and welcomed everyone os us (NEW YORK) to our house without discrimination. What can we do as human beings but to pray. We all extend our heart felt condolonces to the family.

    ReplyDelete
  15. R.I.P Mzee Mwakawago.. Tagie, Kie, Imani na watoto wote wa marehem na familia kwa ujumla, poleni sana..

    ReplyDelete
  16. Mwenyezi Mungu ampumzishe Mzee Mwakawago mahala pema (InshaAllah). Poleni familia yake Mama na watoto wote Imani, Lulu, na wengine wote Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo. Amin!!

    ReplyDelete
  17. He was like a father figure to me, mcheshi,mchekeshaji na mwenye upendo wa hali ya juu, R.I.P Babu,Bibi Mwakawago,Imani,Kie,Lulu n Tage kazi ya Mungu haina makosa may the Gods strength be upon u guys. We love you so much.

    ReplyDelete
  18. Moya ailaze mahala pema peponi roho ya Mzee Mwakawago. Tulikaa naye vizuri sana pale New York. Mungu awape nguvu mke,watoto na familia yote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...