Reggie Mhango jr. akibeba msalaba wakati mwili wa baba yake reggie mhango sr ulipowasili nyumbani leo alasiri tayari kwa kuombewa na hatimaye kupelekwa mazikoni. Reggie sr alikuwa ni mwanahabari nguli aliyefanya kazi Daily News, Herald ya Zimbabwe, Daily Mail ya Malawi na pia Guardian ya Tanzania kabla ya kustaafu miaka kadhaa ilopita. Aliaga dunia Alhamis kwa kiharusi (stroke) katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar
Mwili wa Reggie unawasili nyumbani kwake Magomeni Mikumi
Charles Rajabu, aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Daily News na Sunday News, akitoa heshima zake za mwisho akifuatiwa na Balozi Makame Rashid
Franklin Mziray (kulia) na Profesa Alec Chemponda wakitoa heshima zao za mwisho kwa Reggie

Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa akimpa pole ndugu wa marehemu
Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa akisalimiana na Profesa Alec Chemponda kwenye mazishi ya Reggie
Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga akisalimiana na manahabari veterani Mangengesa Mdimi wakati wa mazishi ya Reggie leo
MchuMchungaji akiongoza sala ya kuwaombea watoto wanne wa marehemu na wajukuu wanne alioacha Reggie. Mkewe aliishatangulia mbele ya haki miaka kadhaa ilopita
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Daily News na Habari Leo, Mkumbwa Ali, akizumzungumzia Reggie ambaye alimtaja kuwa alikuwa mhariri hadi alipostaafu, wakati wa kuumwa na hatimaye kufa
Mhariri mtendaji wa zamani Mh. Uli Mwambuluku akiongea yake juu ya Reggie
Rafiki wa karibu wa Reggie Dk Khoti Kamanga akiongea.
Mzee Barnabas Maro akimpa pongezi mdau aliyemuuguza Reggie hadi dakika ya mwisho
Sehemu ya waombolezaji
huzuni kila pembe
wanahabari na waombolezaji wengine
waombolezaji wa kila kada walikuwepo
hakika reggie alikuwa mtu wa watu
Rais Mstaafu Mh. Benjamin William Mkapa akiwa na nguli wenzi wa uandishi wakielekea kwenye maziko ya Reggie Mhango leo katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Kulia ni Mzee Samwilu Mwafisi, Mzee Ernest Ambali na mdau wa TBC. Mh Mkapa alikuwa Mhariri Mtendaji wa Daily News na Sunday News miaka ya 70 kabla ya kuwa mwandishi wa Rais enzi za Mwalimu
Rais Mstaafu Mh. Benjamin William Mkapa na baadhi ya waandishi habari wenzie
Mabalozi Ami Mpungwe na Makame wakiwa na Mh. H. Kitine na Meya wa zamani wa jiji la Dar, Mh. Kleist Sykes
Rais Mstaafu Benjmin Mkapa akiondoka makaburini baada ya mazishi
baadhi ya wanahabari waliowahi kufanya kazi na Reggie Mhango






















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Huzuni kubwa Michuzi mzee wetu huyo namtakia mapunziko mema,

    ReplyDelete
  2. Asnte kwa picha na video Kaka Michuzi. I feel like I was there.

    May Reggie Rest in Eternal Peace.

    ReplyDelete
  3. Watu kwa uzushi, sie tunaoishi ulaya tulisikia mheshimiwa raisi mkapa eti hatembei kitu kama anatarajia kukatwa miguu sababu ya unene... si huyu hapa tunamwona sasa.

    MICHUZI THANKS FOR THIS INFO umefanya vizuri kusawazisha huu UZUSHI

    ReplyDelete
  4. ni furaha kubwa kwangu (natumai na kwa familia yake pia) kwamba mzee mhango amezikika.

    ReplyDelete
  5. Jamani ni kweli binti wa Mzee Mhango, Aika yule aliyekuwa akifanya kazi uhamiaji (mke wa Charles Kasambula) alifariki? Nimeona kwa mtoa maoni katika picha za awali. Kama ni kweli ni mwaka gani?

    ReplyDelete
  6. Chares Rajabu anafanya nini siku hizi, Mze Makameni baloz wapi?

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Sun Feb 21, 02:56:00 AM, Haika hajafariki, anaishi, ni mzima, buheri wa afya pamoja na mumewe na familia yake.

    ReplyDelete
  8. Ahsante mtoa maoni Sun Feb 21, 01:42:00 PM kwa habari njema.

    ReplyDelete
  9. jamani huyu ni Mkapa yule aliekua rais wa Tanzania? mbona hapewi heshima yake anaonekana kama mtu wa kawaida tu, kasimama chini ya miti, ama kweli, mpanda ngazi hushuka, like me like him

    ReplyDelete
  10. Mie nawapongeza wanahabari wote Tanzania, mna mshikamano na upendo na ushirika wa ajabu sana, kweli muendelee na moyo huo huo na Mwenyezi Mungu awaweze ili mzidi kudumu katika amani na upendo wa kweli, nimekuwa nikiangalia misiba mingi ambayo inawahusu wana habari nikagundua hili.Mungu amalaze pema mzee wetu.

    ReplyDelete
  11. Anony hapo juu, Bro Ben Mkapa ni mtu wa kujishusha linapokuja swala la kijamii. Hana haja ya walinzi 50 wa kuonekana na 80 wa kutoonekana na magari kama 15 hv ya kumsindikiza. Hayuko kwenye dhifa ya kitaifa, yuko kwenye maswala ya kijamii. Hapo watu wako kwenye huzuni uanze kuweka viti vya viongozi wakati wafiwa wa karibu wanalia huku wamesimama..!!

    ReplyDelete
  12. Aika mhango kasambula hajafariki bado yupo anafanya kazi pale pale uhamiaji tanga!..mimi binamu yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...