Mchu
Mchungaji akiongoza sala ya kuwaombea watoto wanne wa marehemu na wajukuu wanne alioacha Reggie. Mkewe aliishatangulia mbele ya haki miaka kadhaa ilopita
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Daily News na Habari Leo, Mkumbwa Ali, akizumzungumzia Reggie ambaye alimtaja kuwa alikuwa mhariri hadi alipostaafu, wakati wa kuumwa na hatimaye kufa
Mhariri mtendaji wa zamani Mh. Uli Mwambuluku akiongea yake juu ya Reggie
Rafiki wa karibu wa Reggie Dk Khoti Kamanga akiongea.
Mzee Barnabas Maro akimpa pongezi mdau aliyemuuguza Reggie hadi dakika ya mwisho
Sehemu ya waombolezaji
huzuni kila pembe
wanahabari na waombolezaji wengine
waombolezaji wa kila kada walikuwepo
hakika reggie alikuwa mtu wa watu
Rais Mstaafu Mh. Benjamin William Mkapa akiwa na nguli wenzi wa uandishi wakielekea kwenye maziko ya Reggie Mhango leo katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Kulia ni Mzee Samwilu Mwafisi, Mzee Ernest Ambali na mdau wa TBC. Mh Mkapa alikuwa Mhariri Mtendaji wa Daily News na Sunday News miaka ya 70 kabla ya kuwa mwandishi wa Rais enzi za Mwalimu
Home
Unlabelled
BURIANI REGGIE MHANGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huzuni kubwa Michuzi mzee wetu huyo namtakia mapunziko mema,
ReplyDeleteAsnte kwa picha na video Kaka Michuzi. I feel like I was there.
ReplyDeleteMay Reggie Rest in Eternal Peace.
Watu kwa uzushi, sie tunaoishi ulaya tulisikia mheshimiwa raisi mkapa eti hatembei kitu kama anatarajia kukatwa miguu sababu ya unene... si huyu hapa tunamwona sasa.
ReplyDeleteMICHUZI THANKS FOR THIS INFO umefanya vizuri kusawazisha huu UZUSHI
ni furaha kubwa kwangu (natumai na kwa familia yake pia) kwamba mzee mhango amezikika.
ReplyDeleteJamani ni kweli binti wa Mzee Mhango, Aika yule aliyekuwa akifanya kazi uhamiaji (mke wa Charles Kasambula) alifariki? Nimeona kwa mtoa maoni katika picha za awali. Kama ni kweli ni mwaka gani?
ReplyDeleteChares Rajabu anafanya nini siku hizi, Mze Makameni baloz wapi?
ReplyDeleteMdau wa Sun Feb 21, 02:56:00 AM, Haika hajafariki, anaishi, ni mzima, buheri wa afya pamoja na mumewe na familia yake.
ReplyDeleteAhsante mtoa maoni Sun Feb 21, 01:42:00 PM kwa habari njema.
ReplyDeletejamani huyu ni Mkapa yule aliekua rais wa Tanzania? mbona hapewi heshima yake anaonekana kama mtu wa kawaida tu, kasimama chini ya miti, ama kweli, mpanda ngazi hushuka, like me like him
ReplyDeleteMie nawapongeza wanahabari wote Tanzania, mna mshikamano na upendo na ushirika wa ajabu sana, kweli muendelee na moyo huo huo na Mwenyezi Mungu awaweze ili mzidi kudumu katika amani na upendo wa kweli, nimekuwa nikiangalia misiba mingi ambayo inawahusu wana habari nikagundua hili.Mungu amalaze pema mzee wetu.
ReplyDeleteAnony hapo juu, Bro Ben Mkapa ni mtu wa kujishusha linapokuja swala la kijamii. Hana haja ya walinzi 50 wa kuonekana na 80 wa kutoonekana na magari kama 15 hv ya kumsindikiza. Hayuko kwenye dhifa ya kitaifa, yuko kwenye maswala ya kijamii. Hapo watu wako kwenye huzuni uanze kuweka viti vya viongozi wakati wafiwa wa karibu wanalia huku wamesimama..!!
ReplyDeleteAika mhango kasambula hajafariki bado yupo anafanya kazi pale pale uhamiaji tanga!..mimi binamu yake
ReplyDelete