ofisa toka kampuni ya ukaguzi ya Deloitte Touche akitoa ufafanuzi wa jinsi watavyosimamia upigaji kula na hatimaye uteuzi wa wanamuziki bora wa mwaka jana wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards mchana huu katika ukumbi wa New World Cinema jijini Dar
Afisa mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa Angelo Luhala akielezea namna baraza hilo litavyoratibu na kusimamia zoezi la kupata wanamuziki bora wa mwaka jana
meneja wa kilaji cha Kilimanjaro George Kavishe akihutubia na kufafanua vipengele vitayotumika katika uteuzi wa wanamuziki bora wa mwaka jana. Kulia ni Mkurugenzi wa OnePlus Communications Fina Mango ambao walikuwa waratibu wa hafla hii leo
mkurugenzi wa BASATA Mh. Gonche Materego (kaunda suti nyeusi) akiwa na meneja wa Kilimanjaro George Kavishe (shoto) na maafisa wa baraza hilo wakifuatilia kinachoendelea
Prezidaa wa FM Academia Nyoshi el Saadat akiuliza maswali ambayo yote alipatiwa majibu. Moja kubwa lilikuwa kwa nini wanamuziki wa Kongo wanaofanya kazi nchini hubaguliwa, akajibiwa udhaifu huo umeonekana na umeshafanyiwa kazi na haitotokea tena, na akiambiwa kwamba maadam bendi na wanamuziki hao wanahudumia watanzania safari hii hakuna ubaguzi
Gerald Hando wa PowerBreakfast ya Clouds FM akiuliza swali
Mwandishi Saleh Ali akiuliza maswali. Pamoja na mambo mengine alitaka kuwepo na usimamizi wenye weledi katika kuhakikisha hakuna njia ya mkato katika upigaji kura kupata wanamuziki bora ambapo magazeti, simu za mkononi na mitandao vitatumika
mwenyekiti wa kamati ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards George Mhina 'Vanga' (wa pili shoto) na wadau wengine. Abubakar Sadik (shoto) Joseph Senga, Angetille Osia na mdau wanafuatia
Nyoshi el Saadat na bosi wa Manywele entertainment
wahudhuriaji wa toka sehemu mbalimbali walikuwapo ikiwa ni pamoja na TID na Emelda Mwamanga wa Bang! (kulia)
toka kulia ni mwandishi Mahmoud Zuberi, AY, Profesa J na Lady JD
Mgeni rasmi Katibu Mtendaji wa BASATA Gonche Materego akiwa na meneja wa Kilimanjaro George Kavishe (shoto) na baadhi ya wanamuziki nyota waliohudhuria. Toka shoto ni AY, Nyoshi el Saadat, Mzee Yusuf, Profesa J, TID na Lady JD
Ratiba ya Zoezi hili kwa mwaka huu ni kama ifuatavyo.
February 18: Uzinduzi rasmi (tayari leo)
March 9: Semina kwa wasanii
March 20 na 21: Semina ya mchakato wa kuchambua kura
March 30: Waliopendekezwa (nominees) kugombea kategori mbalimbali kutajwa
April 1: Kura zinaanza kupigwa na wananchi
April 9: Semina ya wasanii waliopendekezwa (nominees)
May 14: Kilele cha shughuli, washindi kutajwa na kutuzwa















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. DO KABUKTA KA MSANII NOMA INGEKUA ON STAGE SAWA

    ReplyDelete
  2. sasa sijui? mchango wa wanamziki wa Tanzania wanaofanyia kazi zao nje,lakini nyimbo zao zinapigwa na redio za nyumbani tutawapa kipau mbele gani? maana nao wanaiwakilisha bongo na pia kutoa ujumbe kwa jamii kupitia kazi zao za mziki.

    ReplyDelete
  3. kamanda wa ffu na supu yako ya mawe,sijui utaambulia nini?wenzio watapewa zawadi ya Kili na wewe utapewa mawe uzidishe katika supu

    ReplyDelete
  4. hata mimi nimeona hako kabukta hakakukaa sawa na hiyo shughuli..jamani bongo artists hamna stylist???

    ReplyDelete
  5. NAOMBA KUKUREKEBISHA ANKAL JOHN MUHINA AKA VAGA SIO VANGA TAFADHALI USICHAFUA JINA LA MZEE WETU...LOL
    MDAU UK

    ReplyDelete
  6. ha ha haaa uuwii lady gaga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...