JK akiamua kujing’atua nani ashike hatamu?
Nimekuwa nikitafakari mwelekeo wa taifa
Nimekuwa nikitafakari mwelekeo wa taifa
ukizingatia kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi.
Mwanaharakati makini, Mzee M. M. Mwanakijiji ametoa sababu zake zisizopungua 51 kwa nini JK asigombee. Mheshimiwa Shibuda amesema atatumia haki yake ya demokrasia kugombea kushika hatamu baada ya miaka 5 ya JK kuisha pamoja na kwamba CCM wamejiwekea utamaduni na mazoea wa kupeana nafasi kwa miaka 10.
Hapohapo tunaambiwa kwamba tafiti zinaonesha kwamba asilimia 75% ya waliohojiwa wanataka Mheshimiwa aendelee, yaani wameridhika na utendaji wa JK.
Kimsingi watu mbalimbali wana
fikra tofauti na huo ndio ukomavu wa demokrasia.
Baba wa Taifa alichukua hatua ya hiari ya kujing’atua bila ya shinikizo lolote na kuwa mwasisi wa utamaduni huo nchini. Kama JK akiamua kufuata nyayo za Mwalimu ama Mzee Madiba kule Sauzi na kutangaza kwamba ameamua ‘kupumzika’ nani atafaa kushika hatamu na kwa nini ?
Baadhi ya majina mashuhuri ya kuzingatiwa
(ruksa kuongeza pendekezo lako).
E. Lowassa, B. Membe, J. Magufuli, J. Mashaka, S. A. Salim, R. Aziz, J. Shibuda, R. Mengi, L. Masha, Dr. H. Shayo, M. Pinda, Dr. US Blogger, A. Kilango,Dr. B. Buriani, M. Dewji, M. Mwandosya, I. Lipumba, Z. Kabwe, H. Mwakyembe, Vijisenti, J. Cheyo, R. Paulsen, C. Mtikila, J. Malecela, Dr. Kimei, Dr. S. Kawambwa, P. Nalitolela, Dr. Slaa. B.W.Mkapa, F. Sumaye, J. Warioba, Mch. Kakobe, J. Shibuda, P. Msekwa, A. Makinda, S. Sitta, Mch. G. Rwakatare, A.H. Mwinyi, Madaraka Nyerere, Kingunge, Seif Khatib, Dr. H. Mwinyi, M. Bomani,R, Kikwete, J.Makamba, Jerry Muro, M.M.Mwanakijiji etc. etc.
Comments welcome, criticism encouraged.
(US Blogger)
Usblogger11@gmail.com
MASHAKA !!
ReplyDeleteKikwete aking'atuka Nabii YOHANA MASHAKA ndiye Rais wetu............
ReplyDeleteBaraza la mwaziri JK aking'atuka
ReplyDeleteJohn Mashaka, President 2015
Mwamvita Makamba , Vice President 2015,
Dr. Hildeband Shayo, Prime minister 2015
John Mdau (UK), Finance minister
January Makamba, Foreign Affairs minister
Issa Muhidin michuzi, Waziri wa Habari
Steve Kanumba, Waziri wa Utamaduni
Wema Sepetu, Waziri wa Michezo,
Mwanakijiji, Waziri Mambo ya Ndani,
Dr. US-Blogger, Waziri wa Utalii
Kelvin Twissa, Waziri wa Totozzzzz
Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Maji
Baraka Chibiriti Wa Kibatari, Waziri wa Jinsia na Watoto,
Hapiness Magese, First Lady 2015 with a $76,000 ring
Profesa Joseoh Mbele waziri Elimu
Kamanda Suleiman Kova a.k.a ELEKTRONIKI , IGP
Pombe Magufuli, Waziri wa miundombinu
Profesa Mwakyembe, Katiba Sheria
Samwel SIXXX Spika National Aseembly
Nabii Mashaka Yohanna Rais, Pombe Magufuli Makamu wa Rais. Mwamvita makamba makamu wa Rais
ReplyDeletemimi nataka tu mashaka john awe lais ili niende ikuru kuwa mkuu wa kitengo cha upishi kwa sababu nimesomea upishi pale folodhani
ReplyDeletekwa hiyo mafisadi yote nitayawekea sumu kwenye chakura
PETER NALITOLEA NA US-BLOGGER WAKIWA RAIS MIMI NAAMIA SOMALIA. SIWEZI TENA KUKAA TANZANIA US-BLOGGER AKICHUKUA NCHI, HERI HATA NA YA ROSTAM AZIZ
ReplyDeletejohn mashaka all the way baby,,,,,
ReplyDeletedr. shayo makamu,,,,
zitto kabwe waziri wa mambo ya ndani
Sasa na wewe tena kama unapendekeza na MAFISADI na kuwaona wanafaa, ohhh basi tena naona hakuna vichwa Tanzania vya kuaminiwa!
ReplyDeleteus blogger kichaa kama kawaida. akishavuta mavitu vyake, anaingia humu kuropoka,,, kwenda zako
ReplyDeleteUS BLOGGER, INGAWA WEWE NI MBUZI, ILA KULA YANGU ITAENDA AKWA JOHN MASHAKA. HANA UFISADI NA NI KIJANA SAFI ANAYEJITUMA KULIKOMBOA NCHI. HANA MAKUU NA NI MCHAPA KAZI ANAYWAJALI MASIKINI MAALBINO WAZEE NA MAYATIMA, VILEVILE KICHWANI WAMO. HII NDO KICHWA KITACHOIPA BARAZA LETU LA MAWAZIRI KAZI YA KUFANYA, MAONI YANGU TU. MIMI PETER NALITOELA HICHO KINYANG'ANYIRO NITAMUACHIA MTU MMOJA KWA MASLAHI YANGU KWAMBA NAKUWA WAIRI WA MAMBO YA NDANI NA ELIMU ILI MUZUMBE CHUO KIKUU CHA UNIVESITY CHA MUZUMBE MOLOGOLO KIENDELEE IN THE DEVELOPMENT OF EDCATION OF TANZANIA
ReplyDeletelais wangu ni jonatan mashaka tu,,
ReplyDeleteRita pousin???????? ha ha haaa,mimi nataka FREEMAN MBOWE TU! au mtoto wa Mwinyi dr H. MWINYI kwisha kazi.
ReplyDeleteHapo ni LIPUMBA, au MAGUFULI au MKAPA, au MWANAKIJIJI. Ni kati ya hao tu. wana uwezo mkubwa kuliko hata aliyeko sasahivi
ReplyDeleteBILA JK, Mashaka ndani. Hapo Mwamvita Makamba nina uhakika atakuwa makamu wa Rais, na sie Mashosti wote wa U-turn tutaenda ikulu kujirusha, yaani zile za level 8 zitakweisha, mambo yatahamia Ikulu mwanangu. Kujirusha kwa sana, kwa hiwo wadau wote wa U-turn mnajua cha kufanya, kura kwa mashaka.
ReplyDeleteMwamvita Hoyeeeeeeeeeeeee
Michuzi hoyeeeeeeeeeeeee
U-turnnnnn juuuuuuuuuu
NI KWELI BW. KJ AJINGATUE AKAE BURE.
ReplyDeleteMBONA MMEMSAHAU --- BWANA MKUBWA,
MZEE WA KAZI ---- MZAWA WA KWELI::
BW. AUGUSTINE LYATONGA MREMA, ESQ.
You are not serious so I cant comment until you becomes serious especially with those names of mafisadi.
ReplyDeleteKenge
KATIBA INASEMA MTU MMOJA ANAWEZA KUGOMBEA MARA MBILI TU, SO HAMNA HOJA YA KUNG'ATUKA NI KWAMBA HII NI MARA YAKE YA MWISHO HATA AWE MZURI KAMA NANI THIS IS HIS LAST CHANCE, COME 2015 OFF HE GOES HATUANGALII MAKUNYANZI. KATIBA TUMEPEWA NA INASEMA HIVYO SASA MNATAKA NINI GUNIA LA CHAWA MJIKUNE!!!!
ReplyDeleteUS Blogger ashike hatamu.
ReplyDeleteNimecheka sana!
ReplyDeleteSasa huu ni utani au vipi Mkapa na Mwinyi hawaruhusiwi kuwa marais tena kwa mujibu wa katiba sasa sijui hujui au ulimbukeni.
ReplyDeleteUnachanganya sukari na mchanga then unataka watu wachambue? unalinganisha watu wasiolinganishika kwa std yoyote!!
ReplyDeleteHayo majina tumeshayazoea na wengine hapo wanabebwa kwa majina ya baba zao tu (watoto wa baba) tu lakini uongoji hawajui. We need fresh people.
ReplyDeleteHow about Kareem Abdulah, Sanjay Barhat, Mrs Kibwana na Ms Mbaga?
PINDA kwa sabb anaonekana ana uchungu na nchi hii. Lakini kwa vile amezungukwa na mafisadi, yatamshinda.Wakitaka kumsaidia waweke damu mpya ya viongozi serikalini, ili PINDA aongoze nchi
ReplyDeleteMashaka, Mwanakijiji, US Blogger, H. Shayo, P. Nalitolela, umaarufu wao ni nini na wana vigezo gani vya kuweza kuwa rais wa Tanzania? Kwanza huo uraia wa Tanzania wanao au walishautupa kapuni ndio maana waja na ishu ya dual citizen?
ReplyDeleteLabda wagombee urais kwenye Blogu ya Michuzi ndiko waliko maarufu, nje ya hapa hakuna anayewajua wala kutambua michango yao. Kwanza wengine ni waoga hata kutumia majina yao halisi, wanaogopa vivuli vyao wenyewe hivi watafaa kuwa marais kweli? Kwa mfano huyu US blogger unaenda kuomba kura kijijini unawaambia watu mie naitwa US Blogger au MM Mwanakijiji nipeni kura zenu niwaongoze? Nyie mtabai kuota hizo ndoto na kuongoza humu humu bloguni
Nampendekeza Prof. Beda Mutagahywa wa University Computing Centre
ReplyDeleteDr John Pombe Magufuli
ReplyDeleteBwana US blogger, CCM haina utaratibu wa kuwarudisha Marais/ mawaziri wakuu madarakani kwa kipindi kirefu. Halafu ukishangatuka, una kuwa stateman, haipendezi na inaleta kichefuchefu kurudia tena madarakani. Najua zama zile, akina Olusegen Obasanjo au Jerry Rawlings walirudi madarakani, lakini Afrika ya sasa inawakumbatia wastaarabu kama vile Mzee Mandela, joachim Chisano, waliachia madaraka vizuri na sasa wanakula kuku taratiiiiiibu huku wanatoa ushauri wa maana kwa bara la Afrika.
ReplyDeleteWish list yako inatia kichefuchefu.
Mashaka John
ReplyDeletePeter Nalitolela
ReplyDeleteBe serious man!!!!!!stupid
ReplyDeleteMimi sidhani kama ni busara kwa JK kupumzika, labda awe na tatizo la kiafya. Lakini anaonekana Healthier, enegetic na kadhalika. Kiukweli huwezi kutumikia watu kwa kipindi kifupi na kuondoka. Hasa pale unapokuwa na mipongo na mikakati mizuri na inayotekelezeka. Na ikumbekwe kuwa, mpaka sasa bado kuna baadhi ya strategies alizoanzisha Mzee Mkapa zinamaliziwa. sasa nani atamalizia za JK ambaye ameziengineer?
ReplyDeleteKuhusu possible candidate, ni wachache wenye uwezo kati ya hao waliopendekezwa. Tukumbuke Urais si kuuza sura. Ni wafuatao tu wanasifa:-
Dr. Salim, Mohamed S. Khatibu, F. Summaye, Mizengo Pinda, Asha Rose Migiro, Amina salum Ally na Membe. Wazee km Warioba,Malecela, Mkapa, Mwinyi na Msekwa wanafaa lakini huu ni wakati wenye mikiki. Hawataweza himili mikiki hii, wao nionavyo wabaki kuwa washauri.
Asante
Andrew Chenge, prof Beno Ndulu, Balali,Kova
ReplyDeletehuyu nae
ReplyDeleteMichuuzi. Nini hii? Anatupotezea muda. Nilifikiri siku zote kuwa blog hii ni kwa serious minded people. Hebu toa upuuzi huu!!
ReplyDeleteNothing will change...C.C.m wote ni baba ndugu moja...hakuna wa kugombea hapo..na aliyemtaja R.Mengi mhh hata kampuni yake imemshinda sasa ataongoza nji hii! c'mon people KIKWETE kachemsha na hata akibaki hali ni ile ile.na hata mkiwachagua wenigine hakuna hata mmoja labda (SALIM A SALIM pekee ndiye mwenye sifa za kuongoza.
ReplyDeleteMbongo mwenye uchungu
I am sorry, but this is useless!!
ReplyDeleteJK Hanauwezo wa kuendesha nchi zaidi ya kuirudisha nyuma nchi.
ReplyDeleteTuturidishieni Mkapa wetu tusonge mbele!
ReplyDeleteM.Dewji,P.Nalitolela,L.Masha,Z.kwabwe,J.Makamba,J.Muro.Hao wote umri hauwaruhusu kugombea nasafi hiyo ya urais.
ReplyDeleteSijui umri wa mashaka ila natilia shaka uwezo wake!!
Kila Mtanzania aliye na umri wa miaka 21 and above, akili timamu lakini sio timamu sana (maana tunawaona wa hivyo. Hao ndio wafaao
ReplyDeleteAAII, UMESAHAU,
ReplyDeleteMWENYE UCHUNGU NA INJI HII.
sina mbavu,,,what a clap?
ReplyDeletewomens????
ReplyDeleteNadhani US Blogger ametoa changamoto ya muhumu sana hivyo kuna haja ya kusugua vichwa na kutoa mapendekezo ya msingi kuliko maoni ya utani ambayo wengi wa wachangiaji wanayatoa. Nawaomba tuwe serious.
ReplyDeleteLAZIMA TUCHAGUE WACHAPA KAZI, RAIS PINDA MTOTO WA MKULIMA, WAZIRI MKUU JOHN POMBE MAGUFURI, MAKAMU WA RAIS C. MZINDAKAYA, HAPO KITACHIMBIKA.
ReplyDeleteList kamili hii hapa:
ReplyDeletePresident: EDO LOWASSA
Vice Pres : ANDREW CHENGE
PRIME MINISTER: ROSTI TAMU AZIZZI
Finance:SOFIA LION
UTAMADUNI NA MICHEZO :BABU SEA
WANAWAKE NA WATOTO :MAGUFULI
KUDHIBITI MAFISADI: HOSEA
N.K
Us Bloger -ur not serious,yaani umetaja watu ambao hawana mpango wa kugombea coz wanajua hawawezi pata kura pia wameshafanya usifadi wa wa kutosha,mfano,F.Sumaye,E.Lowassa,nani atawasapoti hawa?
ReplyDeletePia umetaja Mch.G.Lwakatare,Mch.Z.Kakobe are kidding?
Umewataja J Makamba,Jerry Muro,John Mashak,Shayo,Z.Kabwe,M.M.Mwanakijiji,R.Paulsen,L.Masha-sijaona hata mmoja mwenye sifa za urais,hawana miaka zaidi ya 50,wengine hawajakomaa kisiasa,wengine still wauza sura,wengine hawana elimu kabisa
R.Mengi,M.Dewji,R.Aziz-Hawa wanapenda kujulikana tu,hawana shida na urais,financially wapo fit,
wengine wazee sana,wanaweza kufa kwa stress za uongozi,eg Kingunge,J.Malecela,Vijicent,waache watafune walizovuna ktk uongozi wao
J,Magufuli,S.Sita,J,Kikwete,Dr Slaa,M,Pinda,B.Bembe,wengine ni A.Kilango,A.Makinda,I.Lipumba,wanaweza wakaingia kwenye kinyang'anyiro,
OOH SORRY NILIKUWA NAOTA ,KUMBE KIKWETE HANA MPINZANIA,KIDUMU CMM
Kissenga
Hii ilikuwa test na wengi wenu mmefeli, wa kuwa hamumheshimu kiongozi wa nchi na lengo lenu na hamuisupport serikali yetu hiyo dual citizenship yenu kwishnehi. MTAISHIA KUNAWA TU, HATULI SAHANI MOJA!!!
ReplyDeleteMkapa anafaa aliacha nchi inaiandaa kupaa sasa hivi imerudi parking. Ila atatakiwa kurekebisha mambo fulani ya kujiwekea 'vijisenti' yeye na mawaziri wake. Lakini sasa hivi cha moto tunakiona.
ReplyDeleteMaisha yamekuwa magumu sana kwa kweli, ingawa hapa mnafanya utani lakini mimi nasema ukweli Mkapa afadhali na hako kaudokozi ka maafisa wake na yeye mwenyewe. Lakini sio mbaya saaaana kihivyo, kwani baba nyumbani kwake kama ameacha watoto wanakula mboga saba mezani kwa mlo siyo mbaya na yeye kujiwekea vijisenti mfuko ili wakati warudi kutoka kazini apate bia moja mbili.
ReplyDeletemashaka apewe urais
ReplyDeleteUS blogger atakapokuwa anavuta maunga yake, nabii mashaka john aongoze nchi
ReplyDeleteni magufuli tu ndo rais
ReplyDeleteJamani watz nani katuroga !!, we are not serious at all , nategemea all of us in this discusson ni interllectuals sasa sielewi wanatoka wapi watu wenye mawazo butu hivi on this seriuos issues
ReplyDeleteKwanza who is John Mashaka to be proposed , mwamvita , jerry muro and many others in the list
If we are seriuos bwana Michuzi kiukweli
wafuatao are the only figures to be guessed 1. Dr John P Magufuli (huyu jamaa anaifaa tz hapa ilipo people are not serious wizi mwingi na mizaha ya ovyo ovyo)
2. S.A. salim (but we make sure all the existing politcal figures wanahjiita wawe prooned haraka)
3. Sitta Samwel (Mzee anafaa si mwoga na atatengeneza timu on his own anajiamini mdau)4.The rest wawe waandamizi kwa uchache kabisa najua under JPM watanyooka apewe ulinzi kama OBAMA Mtaona nchi inaenda
Naishia hapo michuzi na kama people wataendelea na hoja za hovyo block the thread
KWANI KUWA RAIS WA TANZANIA UNATAKIWA UWE NA VIGEZO GANI????
ReplyDeleteMIMI NINAVYOJUWA UKIJUWA KUONGEA KIINGILISH TU UNAPEWA URAIS
SASA KWANINI TUSIMPENDEKEZE ANKAL AWE RAIS WETU???????? KIINGILISH ANAKITWANGA VIZURI
ALAFU VIGEZO VYA KUWA MKUU WA JESHI AU MKUU WA PILISI SI MUHIMU UKIJUWA KUUWA TU AU SIO????
UJUWE KUUWA KUMTOA MWANADAMU ROHO KUMDHURUMU HAKI ZAKE BASI HIVO NDIO VIGEZO
NA KUWA MKUU WA CHAMA VIGEZO VYAKE NI KUWA HODARI KATIKA MAMBO YA KISHIRIKINA YANI UCHAWI
UKIJUWA UCHAWI VIZURI KUWATEKETEZA WENZIO KWA UCHAWI BASI UNAFAA KUWA MKUU WA CHAMA
BONGO MAMBO EASY ME MWENYEWE NIKIRUDI NAGOMBEA UBUNGE SABABU NAJUWA VIGEZO VYA KUWA MBUNGE
VIGEZO VYA UBUNGE NI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KILA KITONGOJI KISIMA 1, ALAFU KUCHANGIA MADAWATI YA SHULE JAPO MADAWATI 5 KILA SHULE
LA MWISHO NI KUNUNULIA JEZI ZA MPIRA TIMU ZA VITONGOJI HAPO UMEMAMLIZA VIGEZO VYA KUWA MBUNGE
BONGO NDIO NCHI ILIYOBAKI YA KUFANYA YOUR DREAM COME TRUE.......................................mdau ndani ya mahakama kuu ya dunia.
UPUUZI MTUPU................!Kukosa shughuli.
ReplyDeleteHivi huyu mashaka John ambaye anasemwa ndo awe rais, ameshaoa? Mimi namtaka hata akishaoa nitakuwa mke wa pili. Ikulu kutamu hata ukiwa mke wa kumi. Wivu nitavumilia tu
ReplyDeleteHE HE HE!!! MMEMSAHAU KANUMBA THE GREAT YEYE AWE WAZIRI WA UTAMADUNI NA MICHEZO.
ReplyDeletehizi comment ni kiburudisho tosha ni kucheka tuu msichulie siriazi kihivyo huyu us blogger kaamua kuchekesha watu lol!!
ReplyDeletendani ya hiyo cabinet awemo Magufuli, Mwandosya, Kilango, Mwakyembe, Pinda.
ReplyDeleteMAXIMO.
ReplyDeleteHiyo safu ya mawaziri umenikosa MIMI...Mmbeba Maboxxxxxxxxxxxx - Waziri wa NISHATI MPYA na RASILIMALI ZA WATANZANIA
ReplyDeleteHuyu Mashaka kafanya nini kwa nchi hii hadi afikiriwe uraisi. Acheni upumbafu. Kuna vijana wadogo ha UDSM. Ngoja muda usogee sogee muwaone. Lakini mimi namuunga mkono sana John Mnyika. toka CHADEMA njoo CCM utawale nchi
ReplyDeleteWAGOSI WA KAYA NDIO WAPEWE AU ANKAL MICHUZI. PAZI.
ReplyDeleteBi kidude!vice mtikila!
ReplyDeletetumwombe mugabe aje asaidie kuongoza na tz.na asiachie labda kifo ndio kimwachishe
ReplyDeleteMie siongelei ambayo hayatatokea!
ReplyDeleteMh.Kikwete hangátuki na ndiye rais wa 2010 kuendelea.
Jon masahaka anastahili kugombea uenyekiti wa mtaa nyumbani kwetu utegi katika uchaguzi ujao.
Mwanakijiji anastahili kurudi nyumbani na kugombea uwenyekiti wa baraza la wanahabari na sana sana kwenye siasa labda aanze na udiwani Kyela au Miswungwi.
Mch.Kakobe aombe kazi kuwa mwakilishi wa 'Fingure of God' Tanzanian chapter.
Mh. Z.Kambwe aache siasa kabisa awatafute washauri wanataaluma (sijui kama us bloger anaweza) kumshauri juu ya research proposal yake kwa ajili ya masomo yake ya Uzamili.
Ukiangalia baraza letu kubwa la mawaziri ni Dr. John Pombe Magufuri peke yake ambaye kazi yake inaonekana. Hata udokta wake sio feki.
ReplyDeleterais wa nji hii mweshimiwa mrema anafaa sana kuwa rais kwani ndiye mwenye uchungu na nji hii
ReplyDeleteHakutakuwa na uchaguzi mwaka 2015.Please note this, kisha weka kwenye diary, halafu tuongee zaidi mwaka 2012/3, Mungu akipenda.
ReplyDeleteJK amelea sana mafisad. Kwenye orodha ya wote waliotajwa majina yao,
ReplyDeleteMwakyembe na Magufuli wanafaa jkuongoza nchi.
JK tumemchoka ameendekeza sana ufisadi, na kuomba omba nje ya nchi. Sijaona maendelea yake hata chembe.
Mdau USA
MIMI NAPENDEKEZA MAGUFULI.......
ReplyDeleteDuu! Ya mzee wa Kiraracha umenikumbusha mbali. CCM wamemchosha mpaka anatamani kurudi. Siku hizi anahubiri sera zote za CCM huku akiwa mwenyekiti wa TLP, yale mawazo mapya aliyokuwa nayo enzi zile hana tena.
ReplyDeleteJ.Kikwete ndiye rais;
ReplyDeleteMh. wewe shughulike na yafuatayo:
1. Muungano wetu wacha ufe; tuwe na mkakati wa kuwa na muungano wa aina nyingine kama shirikisho au jumuiya tu. Hakuna lawama hapo!
2. Punguza kabisa idadi ya Wabunge & Mawaziri
3. Agiza Usalama wa Taifa, Takukuru, Polisi na Mahakama wenyewe kushughulikia wahujumu uchumi, wala rushwa, majambazi na wagombea watakao tumia rushwa. Hakuna huruma kwa watu hao.
4. Wape vijana na wazee (wapya) wasomi na wenye maono nafasi katika mawizara, Tume , Bodi na Taasisi za serikali hata kama ni katika wale walikuwa nje ya nchi. Tunahitaji mabadiliko ya attitude katika kufanya kazi na kutekeleza sera za maendeleo siyo tu kuziandika.
Hakuna huruma kwa asiye ajibika na wananchi wanachoka kusikia majina ya mawaziri & makatibu wakuu wa zamani sana.
Safi sana uendelee kuongeza nafasi kwa wanawake!
5. Kuanzia sasa anza kuchekecha ili baadaye uunde timu ya watu 5 waaminifu kabisa, wasomi, wazalendo, wenye hekima ya hali ya juu, wenye maono na wenye mitazamo mipana wasio na chembe za ukabila wala udini na si lazima kwamba wote watoke CCM; Hao ndio wawe washauri wako hata katika kukushauri juu ya kujaza nafasi mbalimbali. Mh. nakuahidi kuwa kwa kufanya hayo tutaanza ukurasa mpya na utashangaa jinsi tutakavyoanza kupiga hatua za maendeleo katika nyanja mbalimbali ingawa si kwamba itatokea usiku mmoja.
Na ikiwa hivyo unikumbuke nililolisema hapa leo katika blogu ya michuzi.
Tutaendelea kutoa ushauri kama utatakiwa.
Ni mimi kijana Gaye mjukuu wa Ngoho
Crazy Tanzanians(including myself). Tutaendelea kusifia wezi hadi kufa kwetu.Kama unabisha anzia na aliyetoa hii habari hadi wachangiaji wake walivyojituma kuandika upuuzi mtupu.
ReplyDeleteI prefer Dictators like Gadaffi to rule our country na si watu wa CCM ambao daima wapo kulinda maslahi ya chama hata kama yataigharimu nchi yetu. Na watanzania tunaridhika na kuishabikia CCM chama kilichopotea uelekeo na misingi ya kuanzishwa kwake. Ningeshauri wa re-brand hiki chama na kuondoa zile alama za jembe na nyundo na kuweka Noti na gari za kifahari kwani ndio alama z viongozi wetu ambao leo hii wanapigana ili kuongeza majimbo ya uchaguzi kisa ukumbi haujai!Nilitaraji wabunge wangepunguzwa kama Dar es Salaam kuwa lundo la wabunge ambao hawana hata mchano wowote kina Idd Azani, Keenja na Zungu nk mi sioni hata la maana wanalofanya sio bungeni wala mitaani hawaonekani. Kama Keenja ndio mzigo tu wala hana la maana analofanya na watanzania leo wanaweka madarakani watu kama hawa wakiamini kutakua na maendeleo Tanzania. Sahauni hili ikiwa tutaendelea kuweka mizigo tu bundeni na kisha mawaziri. Labda uwaziri uwe ni kazi ya kuajiriwa na sio kupeana kama ilivyo sasa.
jk anafaa kuwa mkuu wa kitu kama kampuni ya entertainment sio raisi
ReplyDeletebora ze komedi wawe mmoja wao raisi na wengine mawaziri au angalau mzee small awe raisi
ReplyDeleteTZ ni viongozi wanajua kupiga domo tuuu hkn vitendo. wabunge nao badala ya kukosoa na kurekebishana kwa manufaa ya walipa kodi na walala hoi, wanachojua ni kilinda allowance zao!! tunaitaji damu mpyaa, sio kupendekeza watu toka tunazaliwa mpk tuaelekea uzeeni wanangangania madaraka,kuanzia enzi Mwalimu mpk enzi ya JK wote muda wao umepita, waache vijana turekebishe nchi yetu, JK aliianza kwa gia kuubwaaa , sasa tuliiii keshalewa madaraka, tuwe na makini jamani, mfumo wote wa bunge, viongozi, na power tunazowapa, zirekebishwe ili wakosolewe inapohitajika. waliopendekezwa woteee awana sifa hata mmoja
ReplyDeleteSHIGONGO WAZIRI WA HABARI,
ReplyDeleteFRANK MACHOZI WAZIRI WA BURUDANI AKISAIDIANA NA JUMP AROUND,
MAMA BALOZI WAZIRI WA WANAWAKE NA WATOTO,to be cont....
juu ya nini hukuweka jina langu?? ntashusha bei ya umeme, maji bure, sherehe zote za ndoa bili kwangu, daladala zote mia mia, hospitali huduma bure ukiwa na kadi ya chama changu, ntasimamia chanjo ya malaria kwa wajawazito na watoto chini ya miaka 15 nk nk. NANI ANABISHA???
ReplyDeleteNi DR. JOHN POMBE MAGUFULI TUU.
ReplyDeleteRAIS NI JOHN MASHAKA. AU MPAKA DILI ILITOKEE, TENA DILI LA NGUVU, VINGINEVYO WAFUASI WA NABII WAKUBALI VIJISENTI
ReplyDeleteBora tuikabidhi nchi kwny ufalme wa mungu.
ReplyDeleteRaisi: nabii J mwingira
makamu wake: sheikh mkuu juma shaaban
waziri mkuu: mama Getrude Rwakatare
waziri wa fedha: sheikh yahaya
waziri waulinzi najeshi lakujenga taifa: mzee wa upako A. Lusekelo
waziri wa nishati na madini: Z Kakobe
waziri wakatiba na sheria: sheikh mtopea
waziri wa habari na michezo: mchungaji mtikira
hapo kutakuwa hamna fisadi mkono waheri naupako hii nchi yakupewa watu wa mungu tu si vinginevyo
Khaaa!!! kweli nimekubali JK hana mpinzani nchi hii pamoja na kashi kashi zote za ufisadi hakuna hata mmoja anayefikiliwa kiukweli kuongoza labda mbowe na zitto kwa tabu ya ukakasi wa kutaja majina ya kifisadi.
ReplyDelete