JK akiaga
JK akiamua kujing’atua nani ashike hatamu?
Nimekuwa nikitafakari mwelekeo wa taifa
ukizingatia kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi.

Mwanaharakati makini, Mzee M. M. Mwanakijiji ametoa sababu zake zisizopungua 51 kwa nini JK asigombee. Mheshimiwa Shibuda amesema atatumia haki yake ya demokrasia kugombea kushika hatamu baada ya miaka 5 ya JK kuisha pamoja na kwamba CCM wamejiwekea utamaduni na mazoea wa kupeana nafasi kwa miaka 10.
Hapohapo tunaambiwa kwamba tafiti zinaonesha kwamba asilimia 75% ya waliohojiwa wanataka Mheshimiwa aendelee, yaani wameridhika na utendaji wa JK.
Kimsingi watu mbalimbali wana
fikra tofauti na huo ndio ukomavu wa demokrasia.
Baba wa Taifa alichukua hatua ya hiari ya kujing’atua bila ya shinikizo lolote na kuwa mwasisi wa utamaduni huo nchini. Kama JK akiamua kufuata nyayo za Mwalimu ama Mzee Madiba kule Sauzi na kutangaza kwamba ameamua ‘kupumzika’ nani atafaa kushika hatamu na kwa nini ?

Baadhi ya majina mashuhuri ya kuzingatiwa
(ruksa kuongeza pendekezo lako).

E. Lowassa, B. Membe, J. Magufuli, J. Mashaka, S. A. Salim, R. Aziz, J. Shibuda, R. Mengi, L. Masha, Dr. H. Shayo, M. Pinda, Dr. US Blogger, A. Kilango,Dr. B. Buriani, M. Dewji, M. Mwandosya, I. Lipumba, Z. Kabwe, H. Mwakyembe, Vijisenti, J. Cheyo, R. Paulsen, C. Mtikila, J. Malecela, Dr. Kimei, Dr. S. Kawambwa, P. Nalitolela, Dr. Slaa. B.W.Mkapa, F. Sumaye, J. Warioba, Mch. Kakobe, J. Shibuda, P. Msekwa, A. Makinda, S. Sitta, Mch. G. Rwakatare, A.H. Mwinyi, Madaraka Nyerere, Kingunge, Seif Khatib, Dr. H. Mwinyi, M. Bomani,R, Kikwete, J.Makamba, Jerry Muro, M.M.Mwanakijiji etc. etc.

Comments welcome, criticism encouraged.
(US Blogger)
Usblogger11@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 84 mpaka sasa

  1. MASHAKA !!

    ReplyDelete
  2. Kikwete aking'atuka Nabii YOHANA MASHAKA ndiye Rais wetu............

    ReplyDelete
  3. Baraza la mwaziri JK aking'atuka

    John Mashaka, President 2015
    Mwamvita Makamba , Vice President 2015,
    Dr. Hildeband Shayo, Prime minister 2015
    John Mdau (UK), Finance minister
    January Makamba, Foreign Affairs minister
    Issa Muhidin michuzi, Waziri wa Habari
    Steve Kanumba, Waziri wa Utamaduni
    Wema Sepetu, Waziri wa Michezo,
    Mwanakijiji, Waziri Mambo ya Ndani,
    Dr. US-Blogger, Waziri wa Utalii
    Kelvin Twissa, Waziri wa Totozzzzz
    Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Maji
    Baraka Chibiriti Wa Kibatari, Waziri wa Jinsia na Watoto,
    Hapiness Magese, First Lady 2015 with a $76,000 ring
    Profesa Joseoh Mbele waziri Elimu
    Kamanda Suleiman Kova a.k.a ELEKTRONIKI , IGP
    Pombe Magufuli, Waziri wa miundombinu
    Profesa Mwakyembe, Katiba Sheria
    Samwel SIXXX Spika National Aseembly

    ReplyDelete
  4. Nabii Mashaka Yohanna Rais, Pombe Magufuli Makamu wa Rais. Mwamvita makamba makamu wa Rais

    ReplyDelete
  5. mimi nataka tu mashaka john awe lais ili niende ikuru kuwa mkuu wa kitengo cha upishi kwa sababu nimesomea upishi pale folodhani
    kwa hiyo mafisadi yote nitayawekea sumu kwenye chakura

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLEA NA US-BLOGGER WAKIWA RAIS MIMI NAAMIA SOMALIA. SIWEZI TENA KUKAA TANZANIA US-BLOGGER AKICHUKUA NCHI, HERI HATA NA YA ROSTAM AZIZ

    ReplyDelete
  7. john mashaka all the way baby,,,,,
    dr. shayo makamu,,,,
    zitto kabwe waziri wa mambo ya ndani

    ReplyDelete
  8. Sasa na wewe tena kama unapendekeza na MAFISADI na kuwaona wanafaa, ohhh basi tena naona hakuna vichwa Tanzania vya kuaminiwa!

    ReplyDelete
  9. us blogger kichaa kama kawaida. akishavuta mavitu vyake, anaingia humu kuropoka,,, kwenda zako

    ReplyDelete
  10. US BLOGGER, INGAWA WEWE NI MBUZI, ILA KULA YANGU ITAENDA AKWA JOHN MASHAKA. HANA UFISADI NA NI KIJANA SAFI ANAYEJITUMA KULIKOMBOA NCHI. HANA MAKUU NA NI MCHAPA KAZI ANAYWAJALI MASIKINI MAALBINO WAZEE NA MAYATIMA, VILEVILE KICHWANI WAMO. HII NDO KICHWA KITACHOIPA BARAZA LETU LA MAWAZIRI KAZI YA KUFANYA, MAONI YANGU TU. MIMI PETER NALITOELA HICHO KINYANG'ANYIRO NITAMUACHIA MTU MMOJA KWA MASLAHI YANGU KWAMBA NAKUWA WAIRI WA MAMBO YA NDANI NA ELIMU ILI MUZUMBE CHUO KIKUU CHA UNIVESITY CHA MUZUMBE MOLOGOLO KIENDELEE IN THE DEVELOPMENT OF EDCATION OF TANZANIA

    ReplyDelete
  11. lais wangu ni jonatan mashaka tu,,

    ReplyDelete
  12. Rita pousin???????? ha ha haaa,mimi nataka FREEMAN MBOWE TU! au mtoto wa Mwinyi dr H. MWINYI kwisha kazi.

    ReplyDelete
  13. Hapo ni LIPUMBA, au MAGUFULI au MKAPA, au MWANAKIJIJI. Ni kati ya hao tu. wana uwezo mkubwa kuliko hata aliyeko sasahivi

    ReplyDelete
  14. BILA JK, Mashaka ndani. Hapo Mwamvita Makamba nina uhakika atakuwa makamu wa Rais, na sie Mashosti wote wa U-turn tutaenda ikulu kujirusha, yaani zile za level 8 zitakweisha, mambo yatahamia Ikulu mwanangu. Kujirusha kwa sana, kwa hiwo wadau wote wa U-turn mnajua cha kufanya, kura kwa mashaka.
    Mwamvita Hoyeeeeeeeeeeeee
    Michuzi hoyeeeeeeeeeeeee
    U-turnnnnn juuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  15. NI KWELI BW. KJ AJINGATUE AKAE BURE.
    MBONA MMEMSAHAU --- BWANA MKUBWA,
    MZEE WA KAZI ---- MZAWA WA KWELI::

    BW. AUGUSTINE LYATONGA MREMA, ESQ.

    ReplyDelete
  16. You are not serious so I cant comment until you becomes serious especially with those names of mafisadi.

    Kenge

    ReplyDelete
  17. KATIBA INASEMA MTU MMOJA ANAWEZA KUGOMBEA MARA MBILI TU, SO HAMNA HOJA YA KUNG'ATUKA NI KWAMBA HII NI MARA YAKE YA MWISHO HATA AWE MZURI KAMA NANI THIS IS HIS LAST CHANCE, COME 2015 OFF HE GOES HATUANGALII MAKUNYANZI. KATIBA TUMEPEWA NA INASEMA HIVYO SASA MNATAKA NINI GUNIA LA CHAWA MJIKUNE!!!!

    ReplyDelete
  18. US Blogger ashike hatamu.

    ReplyDelete
  19. Nimecheka sana!

    ReplyDelete
  20. Sasa huu ni utani au vipi Mkapa na Mwinyi hawaruhusiwi kuwa marais tena kwa mujibu wa katiba sasa sijui hujui au ulimbukeni.

    ReplyDelete
  21. Unachanganya sukari na mchanga then unataka watu wachambue? unalinganisha watu wasiolinganishika kwa std yoyote!!

    ReplyDelete
  22. Hayo majina tumeshayazoea na wengine hapo wanabebwa kwa majina ya baba zao tu (watoto wa baba) tu lakini uongoji hawajui. We need fresh people.

    How about Kareem Abdulah, Sanjay Barhat, Mrs Kibwana na Ms Mbaga?

    ReplyDelete
  23. PINDA kwa sabb anaonekana ana uchungu na nchi hii. Lakini kwa vile amezungukwa na mafisadi, yatamshinda.Wakitaka kumsaidia waweke damu mpya ya viongozi serikalini, ili PINDA aongoze nchi

    ReplyDelete
  24. Mashaka, Mwanakijiji, US Blogger, H. Shayo, P. Nalitolela, umaarufu wao ni nini na wana vigezo gani vya kuweza kuwa rais wa Tanzania? Kwanza huo uraia wa Tanzania wanao au walishautupa kapuni ndio maana waja na ishu ya dual citizen?

    Labda wagombee urais kwenye Blogu ya Michuzi ndiko waliko maarufu, nje ya hapa hakuna anayewajua wala kutambua michango yao. Kwanza wengine ni waoga hata kutumia majina yao halisi, wanaogopa vivuli vyao wenyewe hivi watafaa kuwa marais kweli? Kwa mfano huyu US blogger unaenda kuomba kura kijijini unawaambia watu mie naitwa US Blogger au MM Mwanakijiji nipeni kura zenu niwaongoze? Nyie mtabai kuota hizo ndoto na kuongoza humu humu bloguni

    ReplyDelete
  25. Nampendekeza Prof. Beda Mutagahywa wa University Computing Centre

    ReplyDelete
  26. Dr John Pombe Magufuli

    ReplyDelete
  27. florian rweyemamuFebruary 26, 2010

    Bwana US blogger, CCM haina utaratibu wa kuwarudisha Marais/ mawaziri wakuu madarakani kwa kipindi kirefu. Halafu ukishangatuka, una kuwa stateman, haipendezi na inaleta kichefuchefu kurudia tena madarakani. Najua zama zile, akina Olusegen Obasanjo au Jerry Rawlings walirudi madarakani, lakini Afrika ya sasa inawakumbatia wastaarabu kama vile Mzee Mandela, joachim Chisano, waliachia madaraka vizuri na sasa wanakula kuku taratiiiiiibu huku wanatoa ushauri wa maana kwa bara la Afrika.

    Wish list yako inatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  28. Mashaka John

    ReplyDelete
  29. Peter Nalitolela

    ReplyDelete
  30. Be serious man!!!!!!stupid

    ReplyDelete
  31. Mimi sidhani kama ni busara kwa JK kupumzika, labda awe na tatizo la kiafya. Lakini anaonekana Healthier, enegetic na kadhalika. Kiukweli huwezi kutumikia watu kwa kipindi kifupi na kuondoka. Hasa pale unapokuwa na mipongo na mikakati mizuri na inayotekelezeka. Na ikumbekwe kuwa, mpaka sasa bado kuna baadhi ya strategies alizoanzisha Mzee Mkapa zinamaliziwa. sasa nani atamalizia za JK ambaye ameziengineer?
    Kuhusu possible candidate, ni wachache wenye uwezo kati ya hao waliopendekezwa. Tukumbuke Urais si kuuza sura. Ni wafuatao tu wanasifa:-
    Dr. Salim, Mohamed S. Khatibu, F. Summaye, Mizengo Pinda, Asha Rose Migiro, Amina salum Ally na Membe. Wazee km Warioba,Malecela, Mkapa, Mwinyi na Msekwa wanafaa lakini huu ni wakati wenye mikiki. Hawataweza himili mikiki hii, wao nionavyo wabaki kuwa washauri.
    Asante

    ReplyDelete
  32. Andrew Chenge, prof Beno Ndulu, Balali,Kova

    ReplyDelete
  33. Michuuzi. Nini hii? Anatupotezea muda. Nilifikiri siku zote kuwa blog hii ni kwa serious minded people. Hebu toa upuuzi huu!!

    ReplyDelete
  34. Nothing will change...C.C.m wote ni baba ndugu moja...hakuna wa kugombea hapo..na aliyemtaja R.Mengi mhh hata kampuni yake imemshinda sasa ataongoza nji hii! c'mon people KIKWETE kachemsha na hata akibaki hali ni ile ile.na hata mkiwachagua wenigine hakuna hata mmoja labda (SALIM A SALIM pekee ndiye mwenye sifa za kuongoza.

    Mbongo mwenye uchungu

    ReplyDelete
  35. I am sorry, but this is useless!!

    ReplyDelete
  36. JK Hanauwezo wa kuendesha nchi zaidi ya kuirudisha nyuma nchi.

    ReplyDelete
  37. Tuturidishieni Mkapa wetu tusonge mbele!

    ReplyDelete
  38. M.Dewji,P.Nalitolela,L.Masha,Z.kwabwe,J.Makamba,J.Muro.Hao wote umri hauwaruhusu kugombea nasafi hiyo ya urais.
    Sijui umri wa mashaka ila natilia shaka uwezo wake!!

    ReplyDelete
  39. Kila Mtanzania aliye na umri wa miaka 21 and above, akili timamu lakini sio timamu sana (maana tunawaona wa hivyo. Hao ndio wafaao

    ReplyDelete
  40. AAII, UMESAHAU,

    MWENYE UCHUNGU NA INJI HII.

    ReplyDelete
  41. sina mbavu,,,what a clap?

    ReplyDelete
  42. womens????

    ReplyDelete
  43. Nadhani US Blogger ametoa changamoto ya muhumu sana hivyo kuna haja ya kusugua vichwa na kutoa mapendekezo ya msingi kuliko maoni ya utani ambayo wengi wa wachangiaji wanayatoa. Nawaomba tuwe serious.

    ReplyDelete
  44. LAZIMA TUCHAGUE WACHAPA KAZI, RAIS PINDA MTOTO WA MKULIMA, WAZIRI MKUU JOHN POMBE MAGUFURI, MAKAMU WA RAIS C. MZINDAKAYA, HAPO KITACHIMBIKA.

    ReplyDelete
  45. List kamili hii hapa:

    President: EDO LOWASSA
    Vice Pres : ANDREW CHENGE
    PRIME MINISTER: ROSTI TAMU AZIZZI
    Finance:SOFIA LION
    UTAMADUNI NA MICHEZO :BABU SEA
    WANAWAKE NA WATOTO :MAGUFULI
    KUDHIBITI MAFISADI: HOSEA
    N.K

    ReplyDelete
  46. Us Bloger -ur not serious,yaani umetaja watu ambao hawana mpango wa kugombea coz wanajua hawawezi pata kura pia wameshafanya usifadi wa wa kutosha,mfano,F.Sumaye,E.Lowassa,nani atawasapoti hawa?
    Pia umetaja Mch.G.Lwakatare,Mch.Z.Kakobe are kidding?

    Umewataja J Makamba,Jerry Muro,John Mashak,Shayo,Z.Kabwe,M.M.Mwanakijiji,R.Paulsen,L.Masha-sijaona hata mmoja mwenye sifa za urais,hawana miaka zaidi ya 50,wengine hawajakomaa kisiasa,wengine still wauza sura,wengine hawana elimu kabisa

    R.Mengi,M.Dewji,R.Aziz-Hawa wanapenda kujulikana tu,hawana shida na urais,financially wapo fit,
    wengine wazee sana,wanaweza kufa kwa stress za uongozi,eg Kingunge,J.Malecela,Vijicent,waache watafune walizovuna ktk uongozi wao

    J,Magufuli,S.Sita,J,Kikwete,Dr Slaa,M,Pinda,B.Bembe,wengine ni A.Kilango,A.Makinda,I.Lipumba,wanaweza wakaingia kwenye kinyang'anyiro,

    OOH SORRY NILIKUWA NAOTA ,KUMBE KIKWETE HANA MPINZANIA,KIDUMU CMM
    Kissenga

    ReplyDelete
  47. Hii ilikuwa test na wengi wenu mmefeli, wa kuwa hamumheshimu kiongozi wa nchi na lengo lenu na hamuisupport serikali yetu hiyo dual citizenship yenu kwishnehi. MTAISHIA KUNAWA TU, HATULI SAHANI MOJA!!!

    ReplyDelete
  48. Mkapa anafaa aliacha nchi inaiandaa kupaa sasa hivi imerudi parking. Ila atatakiwa kurekebisha mambo fulani ya kujiwekea 'vijisenti' yeye na mawaziri wake. Lakini sasa hivi cha moto tunakiona.

    ReplyDelete
  49. Maisha yamekuwa magumu sana kwa kweli, ingawa hapa mnafanya utani lakini mimi nasema ukweli Mkapa afadhali na hako kaudokozi ka maafisa wake na yeye mwenyewe. Lakini sio mbaya saaaana kihivyo, kwani baba nyumbani kwake kama ameacha watoto wanakula mboga saba mezani kwa mlo siyo mbaya na yeye kujiwekea vijisenti mfuko ili wakati warudi kutoka kazini apate bia moja mbili.

    ReplyDelete
  50. mashaka apewe urais

    ReplyDelete
  51. US blogger atakapokuwa anavuta maunga yake, nabii mashaka john aongoze nchi

    ReplyDelete
  52. ni magufuli tu ndo rais

    ReplyDelete
  53. Jamani watz nani katuroga !!, we are not serious at all , nategemea all of us in this discusson ni interllectuals sasa sielewi wanatoka wapi watu wenye mawazo butu hivi on this seriuos issues
    Kwanza who is John Mashaka to be proposed , mwamvita , jerry muro and many others in the list

    If we are seriuos bwana Michuzi kiukweli
    wafuatao are the only figures to be guessed 1. Dr John P Magufuli (huyu jamaa anaifaa tz hapa ilipo people are not serious wizi mwingi na mizaha ya ovyo ovyo)
    2. S.A. salim (but we make sure all the existing politcal figures wanahjiita wawe prooned haraka)
    3. Sitta Samwel (Mzee anafaa si mwoga na atatengeneza timu on his own anajiamini mdau)4.The rest wawe waandamizi kwa uchache kabisa najua under JPM watanyooka apewe ulinzi kama OBAMA Mtaona nchi inaenda
    Naishia hapo michuzi na kama people wataendelea na hoja za hovyo block the thread

    ReplyDelete
  54. KWANI KUWA RAIS WA TANZANIA UNATAKIWA UWE NA VIGEZO GANI????

    MIMI NINAVYOJUWA UKIJUWA KUONGEA KIINGILISH TU UNAPEWA URAIS

    SASA KWANINI TUSIMPENDEKEZE ANKAL AWE RAIS WETU???????? KIINGILISH ANAKITWANGA VIZURI

    ALAFU VIGEZO VYA KUWA MKUU WA JESHI AU MKUU WA PILISI SI MUHIMU UKIJUWA KUUWA TU AU SIO????

    UJUWE KUUWA KUMTOA MWANADAMU ROHO KUMDHURUMU HAKI ZAKE BASI HIVO NDIO VIGEZO

    NA KUWA MKUU WA CHAMA VIGEZO VYAKE NI KUWA HODARI KATIKA MAMBO YA KISHIRIKINA YANI UCHAWI

    UKIJUWA UCHAWI VIZURI KUWATEKETEZA WENZIO KWA UCHAWI BASI UNAFAA KUWA MKUU WA CHAMA

    BONGO MAMBO EASY ME MWENYEWE NIKIRUDI NAGOMBEA UBUNGE SABABU NAJUWA VIGEZO VYA KUWA MBUNGE

    VIGEZO VYA UBUNGE NI KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KILA KITONGOJI KISIMA 1, ALAFU KUCHANGIA MADAWATI YA SHULE JAPO MADAWATI 5 KILA SHULE

    LA MWISHO NI KUNUNULIA JEZI ZA MPIRA TIMU ZA VITONGOJI HAPO UMEMAMLIZA VIGEZO VYA KUWA MBUNGE

    BONGO NDIO NCHI ILIYOBAKI YA KUFANYA YOUR DREAM COME TRUE.......................................mdau ndani ya mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  55. UPUUZI MTUPU................!Kukosa shughuli.

    ReplyDelete
  56. Hivi huyu mashaka John ambaye anasemwa ndo awe rais, ameshaoa? Mimi namtaka hata akishaoa nitakuwa mke wa pili. Ikulu kutamu hata ukiwa mke wa kumi. Wivu nitavumilia tu

    ReplyDelete
  57. HE HE HE!!! MMEMSAHAU KANUMBA THE GREAT YEYE AWE WAZIRI WA UTAMADUNI NA MICHEZO.

    ReplyDelete
  58. hizi comment ni kiburudisho tosha ni kucheka tuu msichulie siriazi kihivyo huyu us blogger kaamua kuchekesha watu lol!!

    ReplyDelete
  59. ndani ya hiyo cabinet awemo Magufuli, Mwandosya, Kilango, Mwakyembe, Pinda.

    ReplyDelete
  60. Hiyo safu ya mawaziri umenikosa MIMI...Mmbeba Maboxxxxxxxxxxxx - Waziri wa NISHATI MPYA na RASILIMALI ZA WATANZANIA

    ReplyDelete
  61. Huyu Mashaka kafanya nini kwa nchi hii hadi afikiriwe uraisi. Acheni upumbafu. Kuna vijana wadogo ha UDSM. Ngoja muda usogee sogee muwaone. Lakini mimi namuunga mkono sana John Mnyika. toka CHADEMA njoo CCM utawale nchi

    ReplyDelete
  62. WAGOSI WA KAYA NDIO WAPEWE AU ANKAL MICHUZI. PAZI.

    ReplyDelete
  63. tumwombe mugabe aje asaidie kuongoza na tz.na asiachie labda kifo ndio kimwachishe

    ReplyDelete
  64. Mie siongelei ambayo hayatatokea!
    Mh.Kikwete hangátuki na ndiye rais wa 2010 kuendelea.

    Jon masahaka anastahili kugombea uenyekiti wa mtaa nyumbani kwetu utegi katika uchaguzi ujao.

    Mwanakijiji anastahili kurudi nyumbani na kugombea uwenyekiti wa baraza la wanahabari na sana sana kwenye siasa labda aanze na udiwani Kyela au Miswungwi.

    Mch.Kakobe aombe kazi kuwa mwakilishi wa 'Fingure of God' Tanzanian chapter.

    Mh. Z.Kambwe aache siasa kabisa awatafute washauri wanataaluma (sijui kama us bloger anaweza) kumshauri juu ya research proposal yake kwa ajili ya masomo yake ya Uzamili.

    ReplyDelete
  65. Ukiangalia baraza letu kubwa la mawaziri ni Dr. John Pombe Magufuri peke yake ambaye kazi yake inaonekana. Hata udokta wake sio feki.

    ReplyDelete
  66. rais wa nji hii mweshimiwa mrema anafaa sana kuwa rais kwani ndiye mwenye uchungu na nji hii

    ReplyDelete
  67. Hakutakuwa na uchaguzi mwaka 2015.Please note this, kisha weka kwenye diary, halafu tuongee zaidi mwaka 2012/3, Mungu akipenda.

    ReplyDelete
  68. JK amelea sana mafisad. Kwenye orodha ya wote waliotajwa majina yao,

    Mwakyembe na Magufuli wanafaa jkuongoza nchi.

    JK tumemchoka ameendekeza sana ufisadi, na kuomba omba nje ya nchi. Sijaona maendelea yake hata chembe.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  69. MIMI NAPENDEKEZA MAGUFULI.......

    ReplyDelete
  70. Duu! Ya mzee wa Kiraracha umenikumbusha mbali. CCM wamemchosha mpaka anatamani kurudi. Siku hizi anahubiri sera zote za CCM huku akiwa mwenyekiti wa TLP, yale mawazo mapya aliyokuwa nayo enzi zile hana tena.

    ReplyDelete
  71. J.Kikwete ndiye rais;
    Mh. wewe shughulike na yafuatayo:

    1. Muungano wetu wacha ufe; tuwe na mkakati wa kuwa na muungano wa aina nyingine kama shirikisho au jumuiya tu. Hakuna lawama hapo!

    2. Punguza kabisa idadi ya Wabunge & Mawaziri

    3. Agiza Usalama wa Taifa, Takukuru, Polisi na Mahakama wenyewe kushughulikia wahujumu uchumi, wala rushwa, majambazi na wagombea watakao tumia rushwa. Hakuna huruma kwa watu hao.

    4. Wape vijana na wazee (wapya) wasomi na wenye maono nafasi katika mawizara, Tume , Bodi na Taasisi za serikali hata kama ni katika wale walikuwa nje ya nchi. Tunahitaji mabadiliko ya attitude katika kufanya kazi na kutekeleza sera za maendeleo siyo tu kuziandika.
    Hakuna huruma kwa asiye ajibika na wananchi wanachoka kusikia majina ya mawaziri & makatibu wakuu wa zamani sana.
    Safi sana uendelee kuongeza nafasi kwa wanawake!

    5. Kuanzia sasa anza kuchekecha ili baadaye uunde timu ya watu 5 waaminifu kabisa, wasomi, wazalendo, wenye hekima ya hali ya juu, wenye maono na wenye mitazamo mipana wasio na chembe za ukabila wala udini na si lazima kwamba wote watoke CCM; Hao ndio wawe washauri wako hata katika kukushauri juu ya kujaza nafasi mbalimbali. Mh. nakuahidi kuwa kwa kufanya hayo tutaanza ukurasa mpya na utashangaa jinsi tutakavyoanza kupiga hatua za maendeleo katika nyanja mbalimbali ingawa si kwamba itatokea usiku mmoja.

    Na ikiwa hivyo unikumbuke nililolisema hapa leo katika blogu ya michuzi.

    Tutaendelea kutoa ushauri kama utatakiwa.

    Ni mimi kijana Gaye mjukuu wa Ngoho

    ReplyDelete
  72. Crazy Tanzanians(including myself). Tutaendelea kusifia wezi hadi kufa kwetu.Kama unabisha anzia na aliyetoa hii habari hadi wachangiaji wake walivyojituma kuandika upuuzi mtupu.
    I prefer Dictators like Gadaffi to rule our country na si watu wa CCM ambao daima wapo kulinda maslahi ya chama hata kama yataigharimu nchi yetu. Na watanzania tunaridhika na kuishabikia CCM chama kilichopotea uelekeo na misingi ya kuanzishwa kwake. Ningeshauri wa re-brand hiki chama na kuondoa zile alama za jembe na nyundo na kuweka Noti na gari za kifahari kwani ndio alama z viongozi wetu ambao leo hii wanapigana ili kuongeza majimbo ya uchaguzi kisa ukumbi haujai!Nilitaraji wabunge wangepunguzwa kama Dar es Salaam kuwa lundo la wabunge ambao hawana hata mchano wowote kina Idd Azani, Keenja na Zungu nk mi sioni hata la maana wanalofanya sio bungeni wala mitaani hawaonekani. Kama Keenja ndio mzigo tu wala hana la maana analofanya na watanzania leo wanaweka madarakani watu kama hawa wakiamini kutakua na maendeleo Tanzania. Sahauni hili ikiwa tutaendelea kuweka mizigo tu bundeni na kisha mawaziri. Labda uwaziri uwe ni kazi ya kuajiriwa na sio kupeana kama ilivyo sasa.

    ReplyDelete
  73. jk anafaa kuwa mkuu wa kitu kama kampuni ya entertainment sio raisi

    ReplyDelete
  74. bora ze komedi wawe mmoja wao raisi na wengine mawaziri au angalau mzee small awe raisi

    ReplyDelete
  75. TZ ni viongozi wanajua kupiga domo tuuu hkn vitendo. wabunge nao badala ya kukosoa na kurekebishana kwa manufaa ya walipa kodi na walala hoi, wanachojua ni kilinda allowance zao!! tunaitaji damu mpyaa, sio kupendekeza watu toka tunazaliwa mpk tuaelekea uzeeni wanangangania madaraka,kuanzia enzi Mwalimu mpk enzi ya JK wote muda wao umepita, waache vijana turekebishe nchi yetu, JK aliianza kwa gia kuubwaaa , sasa tuliiii keshalewa madaraka, tuwe na makini jamani, mfumo wote wa bunge, viongozi, na power tunazowapa, zirekebishwe ili wakosolewe inapohitajika. waliopendekezwa woteee awana sifa hata mmoja

    ReplyDelete
  76. SHIGONGO WAZIRI WA HABARI,
    FRANK MACHOZI WAZIRI WA BURUDANI AKISAIDIANA NA JUMP AROUND,
    MAMA BALOZI WAZIRI WA WANAWAKE NA WATOTO,to be cont....

    ReplyDelete
  77. juu ya nini hukuweka jina langu?? ntashusha bei ya umeme, maji bure, sherehe zote za ndoa bili kwangu, daladala zote mia mia, hospitali huduma bure ukiwa na kadi ya chama changu, ntasimamia chanjo ya malaria kwa wajawazito na watoto chini ya miaka 15 nk nk. NANI ANABISHA???

    ReplyDelete
  78. Ni DR. JOHN POMBE MAGUFULI TUU.

    ReplyDelete
  79. RAIS NI JOHN MASHAKA. AU MPAKA DILI ILITOKEE, TENA DILI LA NGUVU, VINGINEVYO WAFUASI WA NABII WAKUBALI VIJISENTI

    ReplyDelete
  80. Bora tuikabidhi nchi kwny ufalme wa mungu.
    Raisi: nabii J mwingira
    makamu wake: sheikh mkuu juma shaaban
    waziri mkuu: mama Getrude Rwakatare
    waziri wa fedha: sheikh yahaya
    waziri waulinzi najeshi lakujenga taifa: mzee wa upako A. Lusekelo
    waziri wa nishati na madini: Z Kakobe
    waziri wakatiba na sheria: sheikh mtopea
    waziri wa habari na michezo: mchungaji mtikira
    hapo kutakuwa hamna fisadi mkono waheri naupako hii nchi yakupewa watu wa mungu tu si vinginevyo

    ReplyDelete
  81. Khaaa!!! kweli nimekubali JK hana mpinzani nchi hii pamoja na kashi kashi zote za ufisadi hakuna hata mmoja anayefikiliwa kiukweli kuongoza labda mbowe na zitto kwa tabu ya ukakasi wa kutaja majina ya kifisadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...