Mganga Mkuu wa Kituo cha afya cha Namtumbo,Dr Ernest Malekela akipokea sehemu ya msaada wa vyandarua toka kwa maafisa wa NMBMkuu wa Kitengo cha Mahusiano benki ya NMB Shy-Rose Bhanji akimkabidhi sehemu ya msaada wa magodoro Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Namtumbo Dr Ernest Malekela, ikiwa ni msaada toka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Namtumbo Mwinyi Khatib na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Thomas Kilongo.
Meneja wa NMB tawi la Namtumbo Bw. Mwinyi Khatib akitoa pole kwa baadhi ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika kituo hicho.
Maafisa wa NMB (shoto) Thomas Kilongo ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Kusini pamoja na Shy-Rose Bhanji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano benki ya NMB wakipokea shukrani toka kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Nambehe mara baada ya kukabidhi Madawati ya madarasa wawili ya shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. enyi viongozi wetu walafi.... tunaomba saaaana hiyo misaada iwafikie walengwa kama ilivyokusudiwa na sio muitoe kwa upendeleo na manyanyaso kama vile nyio ndo mliotoa

    ReplyDelete
  2. Hizi ni pesa zetu walipa kodi so tunaomba tutendewe haki kwani NMB too much kupendelea sehemu za kupeleka hiyo misaada.

    Vijana tuamke wafanyakazi maofisini tunatozwa kodi nyingi na TRA (Tax) lakini muwekezaji anapewa msamaha wa kodi kwa vitu anavyoingiza nchini'' hivi bado tunafanywa wajinga huku tunapiga kura kuchagua viongozi wanaotunyonya watu wa hali ya chini.

    Kweli kwa nini hili lisilalamikiwe JAMANI HEBU KAKA MICHUZI SAMAHANI KWA USUMBUFU NAOMBA HII SWALA TULIANGALIE KUPITIA HII BLOG YA JAMII.

    BY MKEREKETWA

    ReplyDelete
  3. hongereni sana nmb kwa misaada kwa jamii. kila leo mko maeneo tofauti tofauti, hadi kusini mmefika? niwapongeze tu kwani tandahimba kunahitajika sana misaada ni wilaya ambayo iko pembezoni kweli mwa nchi.

    ReplyDelete
  4. safi sana nmb kwa kufika mpaka namtumbo. Huko ni mbali jamani nmb mnastahili pongezi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...