Ilikuwa ni Furaha ya Ushindi kwa Tanzania , hata walioshindwa Timu ya AUSRIA walionyesha uungwana..
Timu ya Tanzania kabla ya mchezo na Timu ya The World- UNICEF

Timu ya Tanzania iliyoshiriki ligi ya Inter Embassies, mjini New Delhi, India imetolewa kwa taabu sana katika mashindano hayo yaliyoanza Ijumaa, Februari 26 kwa kuibamiza Timu ya AUSTRIA jumla ya mabao 10 - 1 katika mchezo uliochezwa katika kiwanja cha great Complex - NOIDA.

Katika mchezo huo wa kwanza, ulishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini India Engeneer John Kijazi sambamba na maofisa mbalimbali.

Timu ya Austria ndiyo ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Tanzania kabla ya kumiminiwa mvua ya magoli hayo.

Katika Mchezo wa Jumamosi Timu ya Tanzania iliingia uwanjani kucheza na Timu ya The World - UNICEF ambapo ilitoka sare ya bao 3 -3 na Jumapili ilicheza tena na Timu ya RUSSIA katika kundi 'A'.

Kwa matokeo hayo, Timu ya Tanzania na AUSTRIA zimetolewa katika hatua ya makundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ati yatolewa kwa tabu lakini si imetolewa ??

    ReplyDelete
  2. Mbona MGOSHI Frank Kiondo huonekani???Au kamati ya Ufundi Mgosi?

    Salaam toka Quebec

    ReplyDelete
  3. we anony wa kwanza stop hatin'.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...