Na ripota wa Mahakamani
wa Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesho inatarajiwa kusoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba.
Hukumu hiyo dhidi ya kesi ya utumiaji mbaya wa madaraka inayomkabili Liyumba, inatarajiwa kusomwa na jopo la Mahakimu wa mahakama hiyo linaloongozwa na Hakimu Edson Mkasomongwa.
Liyumba ambaye anasota rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu, kesho anatarajia kujua hatima ya kesi yake hiyo.
Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.
Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.
Upande huo wa mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na kesi hiyo.
Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.
Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.
Baada ya kumaliza usikilizwaji wa ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010 ambayo ni kesho.

FREE Liyumba
ReplyDeleteduuh..kazi ipo!!hiyo kesho...!
ReplyDeletejamni, sijui hiyo kesho itakuwa..lool!!
ReplyDeleteMichuzi, unabana maoni. Lakini ukweli ni kwamba huu wote ni mchezo wa kuigiza tu. Ni changa la macho tu. ushahidi uliotelewa dhidi ya Liyumba ni wa kumsafisha. Bado serikali haijawa serious na ufisadi. na bado safari ni nedfu sana. Bana tu lakini huo ndo ukweli. Kesho Liyumba will be a free man. Amini usiamini. Wala huhitaji kuwa Jaji kujua hivyo....
ReplyDeleteHakuna kesi ya kujibu hapo..Ni viini macho na usanii mtupu tu ndugu zangu..Karibu tena uraiani Liyumba tuendelee kutesa..You are free man!..teh teh
ReplyDeleteWadau wa mambo ya sheria.. kesho Liyumba yuko huru. Kama hakuwa na shitaka la kujibu katika kuitia hasara Serikali??? ni madaraka gani aliyotumia kama mkubwa wako wa kazi alikuwa akikuingilia?????
ReplyDeletekaka michuzi ni ccm !! mbona unabana comments
ReplyDeleteHUU NI UPUUZI MTUPU NA KUPOTEZEANA MUDA. HIVI KOSA LA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA LIKO KATIKA KIFUNGU GANI CHA SHERIA??! HILO SI KOSA LA KINIDHAMU?! SIJUI MAHAKAMA IMEKUWA INASIKILIZA KESI KWA SHERIA GANI MAANA SIONI KABISA NA WALA HUHITAJI KWENDA SHULE KUONA HAMNA KESI...ILA WAWEZA KUSHANGAA BONGO HII!
ReplyDeleteMZAWA
Bongo tambarare wajameni!!! RUSHWA KWA KWENDA MBEREEEEEE, HAFUNGWI MTU HAPOOOO...HEHEEEE! KAZI IPO. DUU! WELCOME BACK TO THE SOCIETY MKUU WETU!!
ReplyDeleteweraweraaaaaaaa liyumba,karibu mtaani tuendelee kula bata,du umesota sana mtu wangu,come back baby!
ReplyDeletemambo ndio hayooooo! ngoma lazima ichomoke leo, huu ndio mchezo wa serikali kujifanya imepitia process zote kumbe ..... haya leo njio leo, mbeleko zenu tu kuselebukaaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteMICHUZI ACHA KUBANA COMMENTS KAMA UNAONA HATUNA UHURU WA KUCHANGIA TUPENDAVYO TOA MWONGOZO WA NINI KINARUHUSIWA NA NI KIPI HAKIRUHUSIWI,
ReplyDeleteToKA LINI MTU MWENYE PESA AKAFUNGWA TANZANIA?
ReplyDeletekesho ndiyo siku liumba atakuwa huru yani hakuna kesi hapo yuko huru kesho kukuche arudi kwake akaenjoy full kiyoyozi in ze house
ReplyDelete