Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge Mkoani Manyara ,Wilaya ya Babati , (wa pili kushoto ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Mhe. Juma Kapuya (Tanzania Bara) na ( wa pili kulia ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana (Zanzibar) Mhe. Asha Abdallah Juma akishuhudia uwashaji wa Mwenge huo.Wazee wa Mji wa Babati Wakimtunuku silaha za jadi na mavazi ya jadi kuashiria kuwa anakaribishwa kuwa mwenyeji wao Mkoani Manyara ,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mwenge.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Shekifu(wa kwanza kushoto) akiimba wimbo wa Taifa akishirikiana na Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein wa pili kulia wakati wa uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati.Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Frederick Sumaye anaonekana akisoma Gazeti ya Nchi yetu wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati na wa kwanza kushoto ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Mhe. Juma Kapuya akiangalia Chipukizi wakionyesha michezo mbalimbali.
Ngoma ya utamaduni kutoka Hanang wakiburudisha wananchi waliojaa kusherehekea uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara ,Wilayani Babati.
Chipukizi wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Manyara Wilayani Babati wakiangalia na kushuhudia uzinduzi wa Mwenge Mkoani mwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2010

    ni bora ialalishwe tuu hii staili ya kuweka mkono kifuani wakati wimbo wa taifa unaimbwa manake wengine wanaweka wengine wamenyooka kama mshumaa wengine mikono nyuma alimradi kila mmoja na staili yake na wimbo uishe bongo bwana mh!

    ReplyDelete
  2. Mdau, BloomsburyMay 30, 2010

    Kama kuna mdau humu ndani aliye karibu na hawa watu wa utamaduni jamani naombeni mfikishe ujumbe huu: HAILETI MAANA KAMA WASANII WANACHEZA NGOMA ZA KIENYEJI/ KIAFRIKA HALAFU WANAVAA NGUO ZA KISASA/KIMAGHARIBI PAMOJA NA KOFIA (CAP)!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2010

    Hivi jamani wimbo wataifa ukiimbwa huwa tunaweka mkono kifuani au tunaweka mikono chini na kusimama kwa ukakamavu?naona watanzania tumekazana kuiga hadi viongozi wakakosea embu muangalie huyo Shekifu..Boring

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    Ni jambo la aibu sana kwamba chipukizi wamefundishwa kuimba wimbo wa taifa wakiwa wameweka mkono kifuani. Mkuu wa mkoa ametoa mfano. Hii ni mara ya pili globu ya jamii imeanika watu hawajui wanatakiwa kusimama vipi wanapoimba wimbo wa taifa, mara ya kwanza ilikuwa wabunge wakijiandaa kwa mechi.
    Aibu kweli!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2010

    Nauliza tu, hivi hizi sare za mwenge ni lazima ziwe za style ya bangos, manake naamini baada ya hiyo shughuli haziwezi kuvalika mahali pengine popote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...