Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge Mkoani Manyara ,Wilaya ya Babati , (wa pili kushoto ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Mhe. Juma Kapuya (Tanzania Bara) na ( wa pili kulia ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana (Zanzibar) Mhe. Asha Abdallah Juma akishuhudia uwashaji wa Mwenge huo.
Wazee wa Mji wa Babati Wakimtunuku silaha za jadi na mavazi ya jadi kuashiria kuwa anakaribishwa kuwa mwenyeji wao Mkoani Manyara ,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mwenge.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Shekifu(wa kwanza kushoto) akiimba wimbo wa Taifa akishirikiana na Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein wa pili kulia wakati wa uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati.
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Frederick Sumaye anaonekana akisoma Gazeti ya Nchi yetu wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati na wa kwanza kushoto ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Mhe. Juma Kapuya akiangalia Chipukizi wakionyesha michezo mbalimbali.
Ngoma ya utamaduni kutoka Hanang wakiburudisha wananchi waliojaa kusherehekea uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara ,Wilayani Babati.
Chipukizi wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Manyara Wilayani Babati wakiangalia na kushuhudia uzinduzi wa Mwenge Mkoani mwao.

ni bora ialalishwe tuu hii staili ya kuweka mkono kifuani wakati wimbo wa taifa unaimbwa manake wengine wanaweka wengine wamenyooka kama mshumaa wengine mikono nyuma alimradi kila mmoja na staili yake na wimbo uishe bongo bwana mh!
ReplyDeleteKama kuna mdau humu ndani aliye karibu na hawa watu wa utamaduni jamani naombeni mfikishe ujumbe huu: HAILETI MAANA KAMA WASANII WANACHEZA NGOMA ZA KIENYEJI/ KIAFRIKA HALAFU WANAVAA NGUO ZA KISASA/KIMAGHARIBI PAMOJA NA KOFIA (CAP)!!
ReplyDeleteHivi jamani wimbo wataifa ukiimbwa huwa tunaweka mkono kifuani au tunaweka mikono chini na kusimama kwa ukakamavu?naona watanzania tumekazana kuiga hadi viongozi wakakosea embu muangalie huyo Shekifu..Boring
ReplyDeleteNi jambo la aibu sana kwamba chipukizi wamefundishwa kuimba wimbo wa taifa wakiwa wameweka mkono kifuani. Mkuu wa mkoa ametoa mfano. Hii ni mara ya pili globu ya jamii imeanika watu hawajui wanatakiwa kusimama vipi wanapoimba wimbo wa taifa, mara ya kwanza ilikuwa wabunge wakijiandaa kwa mechi.
ReplyDeleteAibu kweli!
Nauliza tu, hivi hizi sare za mwenge ni lazima ziwe za style ya bangos, manake naamini baada ya hiyo shughuli haziwezi kuvalika mahali pengine popote.
ReplyDelete