Msanii Ras Nas a.k.a Nasibu Mwanukuzi ambaye ni mshindi wa tuzo ya msanii bora wa solo (pekee) wa Smiling Faces alipandisha mzuka katika shoo la kufa mtu lililofanyika El Genaina Theatre, Cairo, usiku wa kuamkia leo. Wakati flani ilibidi kraudi ivamie steji manaake palikuwa hapatoshi kujiachia baada ya muziki kupamba moto. Ras Nas na kikosi chake kilifanya shoo mbili wikiendi hii katika miji ya Beirut na Cairo katika tamasha la Spring Festival 2010. Wasanii toka nchi 15 walishiriki. Wanamuziki wa Ras Nas walikuwa Chuck Frazier (USA), Larry Skogheim (Norway), Uriel Seri (Ivory Coast), Karlos Rotsen (Martinique) na Dag Pierre (Sweden). Akiongea kwa njia ya mtandao toka Vienna aliko transit kabla ya kuelekea Oslo, Norway, usiku huu, Ras Nas amesema ameridhika na jinsi muziki wake ulivyopokelewa na akirejea tu Oslo atatunga World tour itayompeleka sehemu zingine kibao duniani.
mashabiki wakichenguka na muziki wa Ras Nas Cairo

Hapo ndo unaona jinsi gani wabongo tulivyo wabinafsi,kwenye kundi lake hakuna mbongo mwengine ina maana wanamuziki wa bongo hakuna anayeweza kuendana na muziki wake?
ReplyDeleteKwa hatua aliyofikia ilikuwa ni wakati muafaka kwake kuwainua wanamuziki wa nyumbani wakaitangaza nchi kikamilifu,jamani kwa nini tusiwe kama wenzetu wa Afrika magharibi ambao wakipata fursa kama hizi basi watafanya kila namna kuwasaidia wenzao waliowaacha na ndio maana wametapakaa dunia nzima, hata kama ulikwenda kwa ugumu haina maana usiwasaidie wenzio. Tenda wemw malipo kwa Mungu
sasa we mdau unapozungumzia ubinafsi!wa wabongo,unashangaza sana,lazima kwanza uelewe tatizo la wabongo wenyewe wanapomuona bongo mwenzao amefanikiwa!badala ya kumuhunga mkono, wanataka kumdidimiza ili akomoke.Pili kama wanamziki wenyewe wa kibongo hawapendi kumpa support sasa yeye afanyeje? ni bora asonge mbele na wanamziki wa mataifa mengine ambao wanao mkubali
ReplyDelete