Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Benki Kuu Amatus Liyumba akiwa kizimbani dakika chache baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kutumua vibaya madaraka wakati wa ujenzi wa maghorofa pacha ya benki hiyo jijini Dar. Mahakimu wawili kati ya watatu walimwona Liyumba ana hatia wakati mmoja alimwona hana hatia. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya wengi wape, hukumu ya miaka 2 inasimama.
Chumba namba moja cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara tu baada ya hukumu kusomwa. Hawa karibu na picha ni mawakili wa serikali

mawakili wa serikali baada ya hukumu kusomwa
wakili wa Liyumba Mh. Majura Magfu akiteta na mteja wake baada ya hukumu

Liyumba akishauriana na mawakili wake baada ya hukumu.
Angalizo: habari kamili na video
vinafuata baada ya muda




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Badala ya huyu mzee kufanyiziwa segerea, ingekuwa viZuli. Zaidi johni mashaka kutumikua kifungo chake ili hakome kuzua mabishano kwenye kijiwe chetu cha buludani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    JIzi likubwa hilo linastahili kifo........upuuzi sana huu...linyongwe

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Ikiwa mteule yohanna mashaka ni msamaria mwema na mlenda nchi yake, basi angejitolea mhamga kwa ajili ya huyu mzee aliechoka. Watamuua huko jela. Pole sana mzee liyumba, mashaka tunataka tamko lako rasmi kuhusu hili ombi la kwenda jela kwa niaba ya lyiumba weee ni naniprofiti kwa hiyo ni vyema ujitolee. ghandhi na yesu walijitolea ma ww pia jitolee kwa ajili ya Tanzania na mzee liyumba

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    So sad indeed. Kuna mtu aliwahi sema kuwa "the only difference between those in jail and the rest of us is that THEY JUST GOT CAUGHT!".

    Jela Jela ni Mbaya. Hakuzoeleki. Ila ndio hivyo. Hopefully yote yataenda sawa huko jela, ama kama kuna mambo ya rufaa na nini.

    Binafsi ni kwamba huwa nahurumia wafungwa wote, mahabusu inclusive. Na sio kwamba nilikuwa nafahamiana na Bwana Liyumba.

    Ila, jamaa kapatikana na hatia ya miaka mi-2 jela, na tayari alikwisha kaa mahabusu mwaka m-1, hii imekaaje hapo? Sasa si ni atakuwa jumla ni kama amekaa miaka mi-3 jela?

    Ya kaisari mwachie kaisari.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    SAFI SANA SHERIA ZA TANZANIA: MWIZI WA MAMILIONI KUFUNGWA MIAKA 2 NA MWIZI WA SIMU ZA MKONONI KUFUNGWA MIAKA KUMI.LIYUMBA MALIZA KIFUNGO ULE MABILIONI YAKO. KUMBE KUIBA TANZANIA NI KUTAMU!!! BAADA YA MIAKA MIWILI TU YA JELA... UTATOKA NA KULA KA RAHA MUSTAREHE!!! HALAFU SERIKALI AINZIDI KUDAI TUWONEE HURUMA VIBA!!! MOTO TU! KUWAPELEKA MAHAKAMANI ... NI KUWAPA OFA TU YA ULAJI

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    2 years jela wanacheza sana!! two years is noughing .ni kama kesho tu anatoka na kula bata na pesa za wananchi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    HII NI TANZANIA, HUYU MHESHIMIWA ATAKAA JELA MWAKA MMOJA. NA KWAKUWA PESA ANAYO, MAISHA YAKE YATAKUWA MARIDADI, ATAKULA VIZURI, ATAANGALIA TV, ATATEMEBELEWA NA FAMILIA YAKE, ATAKUWA NI NYAPARA MKUU, VIONGOZI NA MARAFIKI WATAMTEMBELEA. MWAKA MMOJA ATAVUMILIA, KISHA ATATOKA NA KUENDELEA KUFAIDI ALICHOJICHOTEA. (HII NI MONEY LAUNDERING YA AINA YAKE) AKITOKA JELA HAMUWEZI KUMGUSA KUHUSU UTAJIRI WAKE KWA SABABU ATAKUWA AMESHATUMIKIA HUKUMU YAKE. SINA UHAKIKA KAMA KATIKA HUKUMU KUNA HUKUMU YA KUFILISI UTAJIRI WAKE, KAMA HAKUNA, BASI HIYO IMETOKA NA MCHEZO UTAENDELEA KAMA KAWAIDA. ANABAHATI ALIZALIWA TANZANIA, NA KUHUKUMIWA KIPINDI CHA TANZANIA YA SASA, INGEKUWA ENZI YA SOKOINE, AU ANGEKUWA UCHINA ANGENYONGWA NA KUFILISIWA ILI LIWE NI FUNDISHO KWA WENGINE.HII IN HUKUMU YA KWANZA, ZINGINE ZA KISANII ZINAFUATA.
    NAWAKILISHA HOJA NA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    Just curious je muda aliyo tumia rumade utahesabiwa as part of kifungo????

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    So sad... lakini ndo hivyo hukumu ya ni hukumu.. tujichunge huku makazini hatujui leo au kesho

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    Tatizo letu watanzania huwa hatuko
    serious na maisha yetu,siyo wote ila baadhi yetu,mambo machafu na ya kifisadi aliyofanya huyu baradhuli Liyumba watu badala ya kujadili mambo ya maana wanaanza mambo ya mashaka,huu si upuuzi??kila litu mashaka !!hamuoni aibu pia hamna uchungu na nchi yenu !!ndiyo maana mafisadi hawatisha milele Tz.Atakuja mwingine benki kuu story itakuwa hiyo hiyo maana adhabu siyo kali.Huyu Libpumba ilifaa afungwe maisha au kunyongwa kabisa,kumbukeni rais aliyepita wa
    Korea kusini alivyojiua kwa kujirusha mlimani kutokana na kashfa ya rushwa,sasa sisi tunaona kwaida tu na kuanza upuuzi wa mashaka masdhaka,tutaendelea kuwa
    masikini milele.
    BONGO NYOSO !!!!
    mdau South Korea.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    kwa mtindo huu na mimi nitafanya kama kaka liyumba, hili ni onyo kwa walalamishi wa ufisadi mkichonga sana mtu anafungwa mwaka anarudi kuja kula matunda yake bila starehe

    ReplyDelete
  12. dimba dimbaMay 24, 2010

    WOTE WANAOMTETEA HUYU FISADI WOTE MPANGO MZIMA, ETI MIAKA MIWILI 2 UBABAISHAJI MPAKA KWENYE MAHAKAMA WAKATI TULITEGEMEA HAKI ITENDEKE HUKO TANZANIA BWANA KAMA TULIRAHANIWA

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2010

    kesi ya kima akipewa nyani, matokeo yake ndo haya.Wewe iba kuku wa jirani tu uone,

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    Kisheria kama amehukumiwa miaka 2 na amekaa rumande kwa zaidi ya mwaka 1 yote itajumuishwa na kuhesabiwa kama ameshatumikia jail time kwahiyo atajikuta anakaa jela kwa kama miezi 8 na ujue kwamba hiyo miezi nane inahesabiwa usiku na mchana kwa hiyo atatumikia kama miezi sita tu jela au pungufu labda sheria ya Tanzania iwe tofauti. Ila ndo hivyo bora hukumu imepita kwani baada ya hapo ataendelea na maisha kama kawaida na kulipwa marupurupu yake yote kwa miaka aliyotumikia BOT hajapoteza kitu. Ila iwe fundisho kwa mafisadi wengine kwamba sasa hivi serikali ina macho nyuma na mbele ni wakati wa kuwatumikia wananchi sio kula binafsi.
    Pole zake ila kazi kamaliza sioni hata ulazima wa kukata rufaa hapo ni bora atumikie kifungo na amalizane nao. Tusubirie Minja na Mramba tuone na hao hukumu yao itakuwa vipi!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    Anon May 24, 04:29

    Uyasemayo ni kweli tupu ..

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2010

    Asante sana kwa kujibu swali lanngu ano wa 24 May 05:54pm

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 24, 2010

    Geresha geresha tu, msamaha wa Rais unakuja muda si mrefu kwa excuse ya matatizo ya kiafya na utu uzima. Mtamuona tena anakatiza katiza kwenye vijimitaa kucheki cheki na kuopoa muda si mrefu ujao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 24, 2010

    HUYU JAMAA MIEZI SITA JELA HATAKAA KUNA MSAMAHA WA RAISI UNAKUJA ATAJUMUISHWA HUKO ATATOKA BONGO TAMBARARE

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 24, 2010

    yuko wapi yule mkuu wa bot na aliyejengewa nyumba ya kifahari kwa nini asiende jela na yeye, yeye ndo aliyeitia hasara taifa kuliko jamaa huyu, huyu ni mwizi mdogo sana tu.
    bongo bwana, wezi wakubwa wanaofilisi hazina nzima ya nchi hawatiwi jela wezi wadogo wadogo ndo wanakamatwa.
    upuuzi mtupu huuu.
    ndo maana tuko malofa daima na kungoja wazungu waje watukomboe na wao wanakuja na kutula.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2010

    heheheheh ndengereko iba zaramo ficha..ndio mahakama yetu ya tanzania...wizi wa mabilioni kifungo miaka miwili..kibaka anayepokonya simu mifungo cha maisha...kweli tanzania hakuna haki..natamani nije nikaibe bongo...

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 25, 2010

    jamani niambieni mahali naweza kuiba kama bilioni moja hivi nipo tayari kufungwa miaka mitatu na kidogo

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 25, 2010

    Maskini kasusura aliteswa sana kwa vijisenti vichache

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 25, 2010

    Anon May 24, 07:36 (May 24, 05:54)

    Belated thanks for your clarification on my query. Will be on the sidelines just now, to have a share of a good laugh..

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2010

    ''2 years jela wanacheza sana!! two years is noughing''

    Jamani, lugha za watu hizi. Noughing ndiyo nini? Kwani lazima kuandika lugha hiyo? Aakhaaaa!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 25, 2010

    Ni kinyaaaaaa kwa serikali ya Tanzania kukosa sheria. Kesho naenda kunya mavi kwenye lango la Ikulu ili nione nitafungwa kwa miaka mingapi.

    Mdau Kinyerezi-Ukonga

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 25, 2010

    Wale waote mlioiba hela Tanzania mkakimbilia nchi za nje rudini nyumbani. Tanzania hakuna sheria.

    Mdau USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...