Habari ya leo ankal,
natumaini u mzima wa afya tele. Pole sana na kibarua kizito cha kufanya dunia kuwa kijiji. Ubarikiwe kwa hilo na Mungu akutie nguvu ili libeneke liendelee mbele.
Baada ya salamu ningependa unitundikie tujiombi twangu ili wana libeneke wanisaidie. ningependa kujua kama bongo kuna vyuo ambavyo wanatoa external degrees za uk au marekani katika level za shahada ya kwanza na masters katika fani za computer na management.
natanguliza shukrani,
Ni mimi mdau sambukile.
natanguliza shukrani,
Ni mimi mdau sambukile.


wee uko wapi, andika basi halafu tutakujulisha. Unaposema external programme una maana gani. External programme inapatikana sehemu yoyote. Kama upo bongo unaweza kusoma shahada yoyote ya Kompyuta na management. Lakini sema kama kuna sehemu ambazo wanatoa tution hapa bongo kuhusu hizo degree.
ReplyDeleteMjinga Nguruwe
Vyuo vinavyotoa shahada za nje kwa pale Bongo viko kadhaa. Kwa haraka haraka nakumbuka IFM wanayo hiyo program na vya Uingereza na India. Vingine utavijua ukienda pale kuulizia zaidi.
ReplyDeleteKuna chuo kikuu cha Marekani, jina limenitoka lakini wana chuo chao pale Maktaba (UWT road zamani) ambapo unasoma miaka miwili halafu unamalizia miwili chuo chao huko Marekani (Iowa state). Bei yao ni kubwa lakini unapata shahada ya kwao na unaweza kuhamia chuo chochote marekani kumalizia Bachelor's degree kwa kuwa shahada yao ya miaka miwili (Associate degree) inatambulika Marekani.
ReplyDeleteNadhani unazungumzia Waldorf college. Waldorf college imeuzwa mwezi wa kwanza kama sitakosea.. Hivyo kama hicho huko tanzania bado kipo watu waangalie wajue ni nini hatma yao kabla ya kujiunga au kama bado wakimaliza diploma zao zitakua credited sawa kama zamani....
ReplyDeleteKuna vyuo vingi vinavyotoa mazomo yao online ukijua kilicho halali ni cheaper sana tu na inakusaidia unafanya mambo yako na kusoma.....
Mimi nafanya master na chuo changu hakiko mbali sana ila nimeamua kuchukua online courses na tunakutana mara moja kwa week tu. Muda mwingi ni teleconference na video conference lakini yote ni kwa skype tu...
IFM wanatoa masters'ya IT na Business wakishirikiana na vyuo UK.
ReplyDeleteNenda Learn IT mtaa wa Lumumba Dar es Salaam. Lipia Pound zako kadhaa mitihani inaletwa kutoka UK.
ReplyDeleteAu chuo kingine kinaitwa Horizons nacho kipo mtaa wa Bibi Titi Lipia dola zako mitihani ya marekani ipo.
Institute for Information Technology wanatoa kozi za vyuo vya UK. Nafikiri walianza mwaka 1992 kama sikosei. Wasiliana nao kwa 0715 25 25 25 au email admin@iit-tz.com
ReplyDeleteCheki open university ya UK utaweza kupata unachotaka http://www.open.ac.uk/
ReplyDeleteKila la kheri