Hawa ndio warembo wataochuana
katika kinyanganyiro cha kumtafuta Miss Kilimanjaro 2010

Na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii, Kilimanjaro

Miss Vodacom Kilimanjaro anatarajiwa kupatikana juni 12 mwaka huu katika mashindano yatakayowashirikisha warembo 12 watakaochuwana kuwania taji hilo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Scorpion Promotion and Entertainment inayoandaa mashindano hayo,Jackline Chuwa amesema kuwa maaandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yamekamilika na kwamba yatafanyika katika ukumbi wa Club La Liga,mjini Moshi.

Chuwa amesema kuwa mrembo wa kwanza katika mashindano hayo atazawadiwa laptop ya kisasa yenye thamani ya shilingi laki nane na fedha taslim shilingi laki tano ambapo mrembo wa pili ataondoka na kitita cha shilingi laki saba na nafasi ya kusoma full Secretariat huku wa tatu
akipata laki tano.

Mshindi wa nne atapata laki tatu na sabini elfu,ambapo wa tano atapata shilingi laki mbilina nusu na kwamba washiriki wengine wote waliobakia watapata kifuta jasho cha shilingi elfu hamsinikila mmoja.

Amesema kuwaonyesho hilolitasindikizwa na wasanii kama Chege,Offside trick,Boda 2 Boda na Bendi ya Serengeti ambapo amewataja wadhamini wakuu wa mashindanohayokuwa ni Vodacom,TBL na Mr Price.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2010

    hao warembo wafundishwe 'colour coding', nguo nyekundu na nyeupe, viatu bluu, kijani, brown . .angalau nyeusi kidogo!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2010

    Wamependeza kweli wasichana wa watu lakini walipopigia picha weeee.....yaani pako simple kweli...Hayo majani yana weeds kishenzi...Kwanini kama walijua watafanyia photo shooting yao hapo wasipatengeneze kidogo.

    Tunapenda vitu simple sana hiyo ilikua kazi ya masaa mawili tu. Wangewavalisha hao wadada raba na kuwaambia kushughulikia hiyo sehemu within a minute...Kwanza ingewasaidia kwa afya zao pia...Mazoezi sio lazima kuajiri watu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2010

    Vimwana wa nguvu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2010

    mrembo wakweli afananishwe rangi ya uso na magoti.
    Tazama kitu kile cha kinigeria kilishowahi kuibuka kidedea miss world.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2010

    jamani vimwana wamependenza. narudi bongo kuoa. ukapera leo mwisho. dada wa pili kutoka kulia. moyo wangu umekudondokea.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2010

    Hii budget ya shindano lao ni ndogo sana. The thing looks so cheap..Watapata muwakilishaji mwenye ubora hapo kweli aje auwakilishe ulimwenguni? Hebu angalia yule wa kule mfupiiii..Wanajua requirements za haya majambo international kweli ama wanatania...Sio vipaji, brain na sura yako tu ndio vinauza bali hata appearance. Height muhimu kwenye haya majambo....

    AFASHALI SHULE YA UREMBO IMEFUNGULIWA LABDA WATAFUNDISHA DARASA LA INTERNATIONAL BEAUTY 101

    ReplyDelete
  7. Aaaa!
    We Michuzi MAGUMASHI wewe unatuyzinguz wewe.

    Nenda kule kwa Mroki uwone anavyotupa Snepu za hao maMiss za uhakika.

    Wacheni kutubania bania. Wengine siye hizi ndio starehe zetu kama nyie starehe zenu za BWAWA la MAINI

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2010

    kilimanjaro jmni mko nyuma sna yani since miaka hiyo mpk leo apart frm top 5,da rest ni 50,000 embu wekeni changamoto,nilishiriki Miss Kilimanjaro mwaka 2002 imagine zawadi kwa washindi wa sita na d rest ni da same mpk leo,ndio maana washiriki ni wachache hakuna motisha,waandaaji liangalieni sual hili kwa upya.!othrwise mtaishia kupata warembo wacokuwa na vigezo kila kukicha.!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...